"Kwani mume tatizo?"

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
93,478
119,291
Sasa bana...jana nikiwa katika pilikapilika zangu hapa mjini nikakutana na dada mmoja mrembo sana. Nikawa nimemsahau maana alikuwa kabadili mtindo wake wa nywele na alikuwa kavaa tofauti na nilivyozoea kumwona.

Mara nyingi huwa nikimwona huwa kavaa sare za kazini kwake. Anafanya kazi kwenye moja ya migahawa 'upscale' hapa mjini [Dar]. Basi ikabidi anikumbushe yeye ni nani na huwa tunaonana wapi. Aliponikumbusha tu kumbukumbu zangu zikarudi fasta sana.

Sikutegemea kabisa kuwa angenikumbuka. Ila pia sishangai kivile kwa sababu huwa nikienda hapo kazini kwake yeyote yule ambaye huihudumia meza yangu [na mara nyingi huwa ni yeye] huwa namwachia 'tip' ya nguvu.

Kwa vile jana alikuwa hayupo kikazi, alinichangamkia kuliko ilivyo kawaida. Halafu nadhani alikuwa chini ya ushawishi wa kilevi. Nilihisi alikuwa amekunywa pombe kidogo.

Baada ya soga kidogo akaniomba namba yangu. Nikastuka aliponiomba.
Nikamwuliza 'lakini si una mume wewe?'
Naye akanijibu 'we Ngabu nini bana kwani mume tatizo'? Hebu nipe bana hiyo namba yako'. Ikabidi tu nimpe namba yangu.

Baadaye nikaanza kumwonea huruma huyo mumewe. Na sijui hata kwa nini nilimwonea huruma. Sijui ndo uzee umeanza kuniingia...maana enzi nikiwa shababi badala ya huruma ningekuwa nachekelea tu kumpa mchuchu namba yangu.

Hapa nilipo naisubiri simu yake. Alinipa sharti kuwa ni yeye tu ndo atanitafuta na kwamba mimi nisimtafute. Hiyo ni kwa sababu ya hali yake ya kindoa....Simulizi ya hili tukio iende kwa wale wote wanaoamini wanawake, hususan wake za watu, ni waaminifu........
 
Back
Top Bottom