Kwani Love Connect ni jukwaa la nini?

Kwani Love Connect ni jukwaa la nini?

Ukweli1

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2013
Posts
550
Reaction score
333
Heri ya Mwaka mpya wana Jamii Forums. Ni Busara kama tutaitumia hii fursa ya kuuona mwaka 2015 ni vyema na kua na msaada kwa watu. Unaweza kuwa msaada kwa kuongea kwa Hekima au kukaa kimya. Sio kila kitu unatakiwa kucomment. Naunajifariji kuwa ni sawa tu ni uhuru wa kuongea wakati kuna wanaoumia na comment zako. Baadhi ni ndugu zako, mtoto wako au hata yule wa mtaani kwenu ambaye unatamani sana uongee naye. Unarudi Nyumbani kwako unashangaa kwanini Ndugu/Mtoto wako hana raha kumbe wewe ulimuongelesha vibaya JamiiForums. Yeyote mwenye Smart phone au access to Internet anaweza kuwa member wa Jamii Forums.

Huu Mwaka badilika kumbuka kuwa unaweza fikisha ujumbe wako kwa njia sahihi kama utaamua. Itakuwa ajabu sana kama nitaenda kwa Ofisi ya mwanasheria kuomba ushauri wa afya, maana kama ninatatizo la Afya basi bora niende moja kwa moja kwa Daktari. Ninanukuu kutoka Title inayokaribisha hapo juu "Forum: Love Connect Unatafuta mchumba? Mpenzi? Hili ndilo jukwaa sahihi." Aliyekuja hapa kasoma hapo juu na akaamua kuja kutafuta mchumba/mpenzi kama hapafai waambie waanzilishi JamiiForums wapafunge hapa.

Kama unatoa ushauri/angalizo toa kwa upendo tu mwenye macho ataona. Kama hujafanikiwa hapa jua kuna waliofanikiwa na wapo kwenye Ndoa zao. Usi (generalize) mambo ya watu walioko JamiiForums ni hao hao walio mtaani kama Jamii Forums kumeharibika basi hata mitaani. Jamii Forums ni kama mitandao mingine au mtaani, kama humjui mtu unatakiwa kuwa mwangalifu sana maana sio kila mtu mwema. Toa ushauri wako kwa kujali hisia za aliyeanzisha post.

Kama ambavyo siku hizi baadhi ya ujumbe hatuandiki tena barua za posta tunatumia whatsapp, massege, email na kupigiana simu hii haimanishi kuwa tumekuwa guu zege kwa kutokwenda posta inamaanisha tumebadilika kuendana na maendeleo. Kama watu unaona wanaokuja kwa mtandao ni domo zege na wewe utakuwa na zege nyingi tu kutoka kwa hii mitandao, kono zege, guu zege nk.

Wengine wanapocomment wanania nzuri ya kushauri sema jinsi ya kufikisha ujumbe sio nzuri, na kuna wengine ni maksudi kuharibu jumbe za watu. 2015 jali hisia za wenzio. Kwa anayetumia JamiiForums kwa mahusiano kumbuka kuna watu wenye nia mbaya. Ni vizuri ukachukua tahadhari katika kuanzisha mahusiano, sio siku ya kwanza wewe picha, namba ya simu kila kitu, nenda hatua kwa hatua, msome mtu ukiona taa nyekundu zinawaka simama, usikimbize mambo.

Kuna watu wanajua kudanganya ila machale yatakujisha tu. Mara nyingi watu wanaumizwa kwa sababu hawazitii instincts (machale) yao. Ndio utasikia mtu anasema alihisi tu kuna tatizo mahali na unajiuliza kwa nini aliendelea na huo uhusiano. Machale yakikucheza kama kuna kitu hakiko sawa usizimishe instincts na kupita na taa nyekundu chukua tahadhari punguza speedy, lasivyo kila siku utakuwa umeumizwa wewe tu.

"follow your heart but trust your instincts "

"The human heart is the most deceitful of all things"

Absolutely you are right dear. Thanks!
 
Ulicho sema ni kweli,mtu anatafuta mchumba anajibiwa kanisani kwako hayupo? haaaaaa
 
Back
Top Bottom