Kwani kuwa "Great Thinker" Inamaanisha Kuwa Mpinzani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwani kuwa "Great Thinker" Inamaanisha Kuwa Mpinzani?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Elifasi, Jan 26, 2011.

 1. E

  Elifasi Senior Member

  #1
  Jan 26, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 180
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Evidence JF comments kila pahala: Mara nyingi mtu akipost comment au topic inayoonekana kuizungumzia serikali au mmoja wao (wa sasa au wazamani) positively comments zimekua zikirushwa kwamba si pahala pake (si jukwaa la kusafisha chama au hao). Najiuliza, conventionally au hata radically, fikira zilizotukuka ni lazima zisapoti hoja inayopinga serkali/chama/fisadi au kama kuna kitu positive anaweza kiibua na kutoa analysis, na iheshmiwe as long as ni mawazo yake.

  Vinginevo tuache kuiiita forum za great thinkers iwe ya great political oppositionists!!! Hili ni ANGALIZO na si kusapoti uovu au kusafisha. Nasapoti fikra si unguided, induced venomenous negativity! This way tutawaondoa wapayukaji na wapigadebe walioacha vichwa chooni na kuingia hapa na shingo pekeake!
   
 2. Trustme

  Trustme JF-Expert Member

  #2
  Jan 26, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,172
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  hapana! watu wanasema ukweli! hepu ongelea swala kuhusu mtu mzima Magofuli na utendaji wake kama watakupinga! na juzi juzi tumemwona mama Tibaijuka nae kaanza kuonesha utendaji wake! WATU WANAONA BWANA MEMA NA MABAYA! Ila nazo fikra za mtazamo wa mtu wa kisiasa nao upo sana kwenye JF! kwa hiyo hoja yako nayo ina ukweli. Nashukuru kwa post hii
   
 3. Drifter

  Drifter JF-Expert Member

  #3
  Jan 26, 2011
  Joined: Jan 4, 2010
  Messages: 1,968
  Likes Received: 668
  Trophy Points: 280
  Nafikiri usiumie kichwa sana kukutana na majibu yasiyo ya kistaarabu hapa. Kwa bahati mbaya, JF haina namna ya kuchambua bongo za wachangiaji wote ili kuhakikisha ni post za "Great Thinkers" tu ndizo zinazopata nafasi. Ndio maana kuna michango ya ajabuajabu utakutana nayo humu. Inahitaji uvumilivu tu. lakini ili tuweze kutoa maoni ya maana kwenye hoja yako, hebu toa mifano basi ya post za aina iliyo kwenye red hapo juu ulizowahi kupost au kuona zimepostiwa kisha zikajibiwa utumbo. Ingawa kwa tahadhari tu ni kwamba mahali ilipofikia serikali yetu na CCM yake utapata maumivu sana kujaribu kutafuta "positive outlook" ya taasisi hizo hata mitaani.
   
 4. Ernesto Che

  Ernesto Che JF-Expert Member

  #4
  Jan 26, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,117
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Elifasi, naomba utambue kwamba watu hapa (JF) wanajaribu kutoa maoni yao kama watanzania wengine, kuwa na mrengo wa kupinga maovu ya CCM ni haki yao au kuwa Great thinker ni kusapoti CCM? Kuna hoja tata nyingi ambazo serikali ya CCM imeshinda kuzishughulikia mf. Dowans, Richmond, Kagoda, Meremeta, Radar, Katiba, Wizi wa mali za Umma, uchakachuaji matokeo ya urais, meya Arusha, ufisadi UBT, Maliasili, TICS, Mramba na wezi wenzie, RA, EL. Sasa kwa utitiri wa mauvu haya unategemea wananchi watakuwa positive towards CCM na serikali yake? Ndio maana kila kona CCM inashambuliwa si hapa tu (mimi nashiriki ktk midahalo at ground level). CCM hawataki ku-deal na tatizo isipokuwa wanatafuta mchawi.
   
 5. d

  dos santos JF-Expert Member

  #5
  Jan 26, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 240
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  ni kweli ushabiki umezidi kuliko kuangalia hoja zitokewazo. Jadili udhaifu labda wa mwanasiasa wa upinzani uone matusi yake. Tatizo wapinzani ni kama malaika hawakosei na serikali kama shetan hana zuri hata moja
   
 6. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #6
  Jan 26, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Great Thinker ni mtu tu wa kawaida kabisa lakini mwenye mapenzi makubwa na udadisi wa mambo, matumizi ya ushahidi usio na shaka ama kwa kuthibitisha au kukataa madai fulani.

  Ni mtu mwenye kuvutiwa zaidi na maswali magumu kuliko majibu rahisi, haonei aibu hoja, uvivu wa kufikiri walana kwa sana kuachia hoja yenyewe uhuru wa kujiendesha yenyewe bila kulazimishwa mwelekeo fulani kwa nguvu.

  Walau unaweza ukaanzia hapo kujua maana GTs.
   
 7. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #7
  Jan 26, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,268
  Trophy Points: 280
  Ukitaka hoja za kuisifia serikali dhaifu na dhalimu kama hii, basi usipate shida nunuwa magazeti ya uhuru na mzalendo pamoja na habari leo. na pale facebook kuna page ya Jakaya Kikwete, basi jiunge huko wewe kazi yako iwe kusifia ujinga tu.
  By the way, hebu tutolee mfano mdogo tu, serikali hii ya ccm tutaisifia au kuisema vizuri kwa lipi?
   
 8. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #8
  Jan 26, 2011
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Kaanzishe forum yako basi yenye sifa unazozitaka. Hatujakuzuia..
   
 9. bluetooth

  bluetooth JF-Expert Member

  #9
  Jan 26, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 3,933
  Likes Received: 670
  Trophy Points: 280
  evidently ni kwamba hata kwenye society kuna makundi mbalimbali kama ya vyama vya siasa na hata magenge ya wahuni wa kukodishwa...JF is a forum...it stands to be hosting any member.., non member.., supporting groups.., political parties.. magenge ya wahuni .., achochezi.., pro government supporters.., pro ufisadi.., anti governmet groups, NGO's na kadhalika....

  please hesitate and be considerate...if you do not have interests in any of the posts supported by certain group ..., keep away..... wanasema pili pili ya shamba.............
   
 10. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #10
  Jan 26, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kuna baadhi ya vitu uwezi kuvizuia hata ufanye nini,ndio kama hapa jf uwezi kuzuia mtu asi comment,wewe kubaliana na hali halisi,kama ukichoka sign out, halafu sign in kwenye facebook.:suspicious::suspicious::suspicious:
   
 11. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #11
  Jan 26, 2011
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  avatar yako inatia kinyaa,kuna waislam humu tafadhali
   
 12. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #12
  Jan 26, 2011
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  sio jibu ,hayo ni mawazo yake tuyaheshimu,ukweli ni kuwa hayo aliyosema yana kaukweli fulani tuzingatie jamani
   
 13. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #13
  Jan 26, 2011
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Sio jibu ya swali gani? sioni cha kuzingatia hapa..ni upupu tu.
   
 14. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #14
  Jan 26, 2011
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Kwa hiyo afenyeje? hii sio forum ya kidini, kama hutaki kuepo hapa tafuta forums za wajahidina , zipo nyingi tu, hulazimishwi kuepo JF.
   
 15. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #15
  Jan 26, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,268
  Trophy Points: 280

  Kama ulikuwa tu unasikia neno mnafki basi usipate shida kujuwa mnafki anafananaje, jiangalia wewe kwanza utamjuwa mnafki ni mtu wa namna gani!
  sasa wewe hiyo Avatar yako hauoni kama vilevile inatia kinyaa? haujuwi kama humu kuna wayahudi? au ndio nyani halioni kundule?
   
 16. Bukanga

  Bukanga JF-Expert Member

  #16
  Jan 26, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 2,863
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  Nyerere na wanyonge "lakini linaloonekana zaidi machoni pa watu (watanzania) wenye matatizo makubwa ya uchumi, kama wanayoyapitia hivi sasa watu wengi waaminifu, ni kule kuanza kuonekana kwa matajiri kwelikweli ktk nchi maskini kama yetu" ndg. Nadhani suala la kuwa na mtizamo hasi kwa mwenendo wa nchi haukuanza leo na pia mtizamo chanya haukuanza leo, kwa hyo nadhani ni vema tukapingana ili kuweka mambo sawa otherwise wote tuwe kama kina Kibonde pamoja na kuona hakuna cha kusifia inawalazima japo kusifia "suti" za kina Membe et al na miwani zao.
   
 17. Drifter

  Drifter JF-Expert Member

  #17
  Jan 26, 2011
  Joined: Jan 4, 2010
  Messages: 1,968
  Likes Received: 668
  Trophy Points: 280
  Hapo ndipo watetezi wa serikali mnapopotea. Serikali haipimwi kwa kuhesabiwa "mazuri" au "mema" kama wengine mnavyopenda kusema. Serikali si mtu binafsi au "msamaria mwema". Inawajibika kikamilifu kwa wananchi. Kazi ya Serikali ni kutimiza wajibu wake kama ulivyoainishwa kwenye sera, mipango na miradi mbalimbali ya kitaifa. Ndio maana inakabidhiwa madaraka kamili juu ya rasilimali zote za umma na juu ya usimamizi wa sheria na taratibu za nchi. Kuonyesha chuo au barabara moja iliyojengwa na kututaka tutoe pongezi kwa "hayo mema" machache ilhali benki kuu imekwapuliwa mkwanja wa kutisha na sekta nzima ya nishati (umeme) imehujumiwa kichizi, n.k. ni uswahili na ubabaishaji wa hali ya juu.
   
 18. BULLDOZZER

  BULLDOZZER Senior Member

  #18
  Jan 26, 2011
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 103
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  great thinker ni mtu anayeweza kuyaona mambo katika mizani tofauti.
   
 19. E

  Elifasi Senior Member

  #19
  Jan 26, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 180
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nafikiri mawazo yako kama haya ndio chanzo cha tatizo. Kuna tofauti kati ya fikra za muuza bidhaa (no offence-mfano mhudumu wa bar), na meneja wa masoko wa TBL, na aliyefikiri formulae ya bia - anayoipigia debe marketing manager na anayeichomekea bili bar man/maid!!! Of course zote zimetumia ubongo kufikia hapo mpaka ukatoa NOTI iliyopauka ya Ndulu/JK. So, ishu si kuwa na mdomo wa kuongea ndo kila mtu akusikilize - ushu ni kunena. ishu si kufanya: ishu ni kuweka brain onto it! IF ya ain't thinker, huwez elewa Drifter!

   
 20. E

  Elifasi Senior Member

  #20
  Jan 26, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 180
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unaona, tatizo ndo hili.... Kama nsipotumia fikra, ningekujibu hivi: 'na wewe kama unaona hii post haiku-impress, kwanin usisome zngine uachane nayo, au uweke ya kwako"?

  Lakini kwa sababu nafikiri nakujibu hivi: think through then reply mazee, donk drink through!! Great thinkers are way ahead of ya.... if ya not! I am, take that as a compliment to you!

   
Loading...