Kwani kuwa CHADEMA lazima uwe na chuki ya serikali?

Makusudically

JF-Expert Member
Feb 3, 2014
2,203
1,235
Nimekuwa nikifuatilia kwa karibu, kila mwanaCHADEMA ukimsikiliza anaongea lazima aishambulie Serikali, utamsikia akishambulia viongozi wa Serikali tena mashambulizi binafsi.

Mfano mashambulizi dhidi ya Makonda kuhusu uhalali wa vyeti vyake, mambo ambayo hayana tija kwa maendeleo na changamoto zinazowakabili Watanzania.

Kwani kuna ukweli hata kidogo kuwa Serikali hakuna zuri lolote ililolifanya tangu kuingia madarakani?
 
Watu wanataka vyeti wewe unaleta ngonjeera.

Weka vyeti mezani kwanza.

Kama mambo ya kuhoji vyeti hayana tija serikali isingefanya kazi ya uhakiki wa vyeti kwa watumishi wake.

Kama biblia inavyosema.(ingawa Mimi sio muumini wa dini yoyote) utafteni kwanza ufalme wa mbinguni na mengine mtaongezewa, basi wekeni vyeti hayo mengine mtafanikiwa.
 
Nimekuwa nikifuatilia kwa karibu, kila mwanachadema ukimsikiliza anaongea lazima aishambulie Serikali, utamsikia akishambulia viongozi wa Serikali tena mashambulizi binafsi. Mfano mashambulizi dhidi ya Makonda kuhusu uhalali wa vyeti vyake, mambo ambayo hayana tija kwa maendeleo na changamoto zinazowakabili Watz. Kwani kuna Ukweli hata kidogo kuwa Serikali hakuna zuri lolote ililolifanya tangu kuingia madarakani.?
Ambacho hujafuatilia ni kila anayeikosoa serikali humu anabandikwa jina la nyumbu na chadomo. Hebu fuatilia na hili kisha urejee kama wewe ni mfuatiliaji kama unavyojinasibu.
 
What a shame.. ....serikali ni cheti au daudi na cheti....kuna mambo ya kumshauri rais wako fanya hvyo na sio mbya kumwambie kuna mtumshi ana cheti cha mtu.
 
The Unknown, umedhihirisha wazi kwamba wewe huna hata cheti hata cha ngumbaru, yaani Elimu ya Watu wazima. Kama unabisha post cheti chako humu ndipo upate uhalalali wa kuhoji za wenzako.
 
Ni kwa sababu tangu tumepata uhuru tunaongozwa na chama kilekile, tatizo ni kwamba badala ya kusongambele tumebaki kama machizi katika nchi yetu,hatuna nafuu hata kidogo, maisha yanazidi kubana kama chupi ya ngozi kwenye jua kali, kila kukicha vitu bei juu, kodi, kila mwaka utasikia kila mtanzania anadaiwa,lakini kila wakati utasikia, tunawaomba wananchi mzidi kuwa wavumilivu, lakini kwanza ndio shilingi inazidi kuporomoka, kwa nini nisichukie?
 
Nimekuwa nikifuatilia kwa karibu, kila mwanaCHADEMA ukimsikiliza anaongea lazima aishambulie Serikali, utamsikia akishambulia viongozi wa Serikali tena mashambulizi binafsi.

Mfano mashambulizi dhidi ya Makonda kuhusu uhalali wa vyeti vyake, mambo ambayo hayana tija kwa maendeleo na changamoto zinazowakabili Watanzania.

Kwani kuna ukweli hata kidogo kuwa Serikali hakuna zuri lolote ililolifanya tangu kuingia madarakani?
Watu hawachukii serikali wanachukizwa na mambo ya hovyo!
 
Nimekuwa nikifuatilia kwa karibu, kila mwanaCHADEMA ukimsikiliza anaongea lazima aishambulie Serikali, utamsikia akishambulia viongozi wa Serikali tena mashambulizi binafsi.

Mfano mashambulizi dhidi ya Makonda kuhusu uhalali wa vyeti vyake, mambo ambayo hayana tija kwa maendeleo na changamoto zinazowakabili Watanzania.

Kwani kuna ukweli hata kidogo kuwa Serikali hakuna zuri lolote ililolifanya tangu kuingia madarakani?
Simple, mtu yeyeto anayethamini utawala wa sheria na democrasia atajiunga na CDM. MWOGA, mnafiki msigina katiba, sheria, taratibu and the like atakuwa CCM
 
Nimekuwa nikifuatilia kwa karibu, kila mwanaCHADEMA ukimsikiliza anaongea lazima aishambulie Serikali, utamsikia akishambulia viongozi wa Serikali tena mashambulizi binafsi.

Mfano mashambulizi dhidi ya Makonda kuhusu uhalali wa vyeti vyake, mambo ambayo hayana tija kwa maendeleo na changamoto zinazowakabili Watanzania.

Kwani kuna ukweli hata kidogo kuwa Serikali hakuna zuri lolote ililolifanya tangu kuingia madarakani?

Niwale wanaojitambuwa nakufaham ukweli

hakika madhila na dhiki zilizosababishwa na ccm huwezi kuipenda kamwe, isipokuwa WANAFIKI.
 
Nsikine, ulitaka tuongozwe na Chama gani?, au unataka tuongozwe na Chadema? Sisi wenzio tuko vizuri. Chizi ni wewe peke yako, NDIYO maana unataka tuongozwe na SACCOSS ya Wachagga. Utasubiri saaaaana.
 
Nsikine, ulitaka tuongozwe na Chama gani?, au unataka tuongozwe na Chadema? Sisi wenzio tuko vizuri. Chizi ni wewe peke yako, NDIYO maana unataka tuongozwe na SACCOSS ya Wachagga. Utasubiri saaaaana.
Umeuliza swali katika uzi wako na mudau kwa jina la Nsikine amekujibu,na katika post yake hajataja neno chizi sasa sijui wewe umelitoa wapi??
Pili kama ulikua na nia ya kuhitaji majibu katika uzi wako ungesoma alichokuandikaia Nsikine katika post yake kisha ungeuliza maswali kuhusiana na alichokuandikia,sasa mambo ya saccos yametoka wapi??
 
Uchumi wa hovyo utadhani tumetoka kwenye Vita, kila Mtanzania analia tu, Afya hovyo, Elimu Bashite kabisa, Njaa kila mahali, Sasa wewe ndugu unataka isifiwe kwa lipi labda, Kuondoa uhuru wa mawazo na Kukandamiza Wapinzani! !!
 
Back
Top Bottom