Sabung'ori
JF-Expert Member
- Jul 19, 2011
- 2,166
- 1,249
...HIVI KWELI KISWAHILI HAKINA MANENO MATAM NA YENYE-MVUTO KTK MAMBO YA MAHABA?..
Hiyo labda kwa watoto wa siku hizi, sie wa zamani Kiswahili mwanzo mwisho, popote saa yoyote :]
Vipi unan'chekicheki kwa woga nini!
:]
Tatizo la kiswahili ni kuwa kinachotumika mitaani ni tofauti na kinachotumika vitabuni (mtazamo wa kiujumla).
Lakini kwenye mapenzi,maneno mengine yanakua kama yamepungua ladha ama yameongezeka ukali zaidi. Kuna maneno ya kiswahili kuyatamka mapenzini inakua ngumu kidogo hadi ukishikilie mahali,lol
(Hivi 'LOL' kiswahili utasemaje?)
Unaona sasa,kupasuka mbavu, kuvunjika mbavu ama kuangua kicheko?Hata Kiingereza nacho kiko hivyo hivyo. Njoo nikupeleke Bankhead au Mechanicsville tuone kama utaambulia chochote!
Unaona sasa...tatizo letu ni kudhani hayo maneno ya Kiingereza yalijileta tu yenyewe!
Napasuka mbavu (NM).
Unaona sasa,kupasuka mbavu, kuvunjika mbavu ama kuangua kicheko?
Mwisho wa yote ni Wakurya, wakiwa wanatongoza utawasikia wakisema " umeorewa au bado unapigapiga umaraya?"
yatajeni hayo maneno hapa km ambavyo mnatoa hiyo mifano ya lugha ya kiingerezaManeno ya Kiswahili yanajitosheleza kwenye mahaba na mapenzi kwa ujumla.
Tunachokosea ni kutaka kutafsiri neno la Kiingereza kuwa la Kiswahili.
Mtu atasema nikitaka kuita "baby" jee?
Kwani lazima umuite "baby"? Maneno ya Kiswahili ya kimahaba na kiuchokozi wa mapenzi yapo mengi, hakuna haja ya kuita "baby" wala "I love you"
Hivi wana JF kuna uhusiano gani kati ya hii lugha ya malkia na mapenzi?.Nimejaribu kufanya uchungunzi mdogo nimegundua kwamba CARD au SMS nyingi za mapenzi zimeandikwa/zinaandikwa kwa luga ya kiingereza.Utakuta mtu na mpenzi wake labda wote ni wasukuwa,w anyamwezi,wapale nk lakini bado ktk maongezi yao utasikia ...i miss you...i lov you...honey...HIVI KWELI KISWAHILI HAKINA MANENO MATAM NA YENYE-MVUTO KTK MAMBO YA MAHABA?...nawataadhalisha wapendanao...ukiona mtu anapenda sana kutumia luga ya mkopo,angalia isijeikawa ata hizo hisia anazotoa kwako amekopeshwa...