Nilufer
JF-Expert Member
- May 10, 2012
- 9,567
- 13,542
NAKUJIBU KWA KUWA UMENIITA NIKUJIBU.
Kwako YERIKO NYERERE.
Nimesoma andiko la mdogo wangu Yeriko Nyerere akimkosoa Ndg. Polepole Katibu, Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi baada ya press yake ya Jana tarehe 25,Mei,2017 na waandishi wa habari.
Katika andiko lako umelalamika sana mdogo wangu kwa uchungu mwingi lakini sikufikiria kama unaweza kutoa maneno ya hovyo kwa Katibu wangu.
Vita hii ni VITA DHIDI YA MTANDAO ULIOJIIMARISHA KUNYONYA UCHUMI NA RASILIMALI ZA WATANZANIA.
Vita hii inapiganwa kati ya Wazalendo na wasaliti wachache WALIOUNDA MTANDAO wa kufuja rasilimali zetu wakishirikiana na wanamtandao wenzao kutoka mataifa ya nje. Wasaliti hawa wachache kwa ushirikiano huo wameweza kuwa na utajiri mkubwa pamoja na kumiliki VIWANDA nchi za ughaibuni, CHINA, Kuwait, Dubai na kwingineko. Kundi hili wanajiita WANAMTANDAO na kiongozi Mkuu ni EDWARD NGOYAI LOWASA. Pia wapo MBOWE, SUMAYE, NDESAPESA n.k.
Kukuthibitishia hilo LOWASA Mwaka Jana mwezi wa 7 alitoa kauli inayosema "Marafiki zangu mlioko CCM tuendelee kushirikiana" hawa sio just marafiki ni WANAMTANDAO.
Kauli nyingine alipoulizwa mwaka 2015, pesa hizo anazotumia kuzigawa kama njugu kutafuta URAIS anazitoa wapi akasema anatoa kwa Marafiki zake........ Who are they? Ni WANAMTANDAO hao ndani na nje ya NCHI.
ILI UNIELEWE NGOJA NIKUPE FLASH BACK.
Anyway labda nikuelekeze hivi, katika historia ya nchi hii mwalimu aliweka misingi ambayo lengo lake lilikuwa kuwajengea watanzania spirit ya uzalendo kwa nchi yao. Nina imani wakati misingi hii inawekwa ulikuwa haujazaliwa bado.
Wakati wa kuweka misingi hii hakukuwa na CHADEMA, wala CUF wala NCCR mageuzi, wala UKAWA. Baba yake mbowe alikuwa ccm na LOWASA alikuwa chipukizi ccm. 90% ya unaowaona upinzani walikuwa CCM. Katika kuweka misingi hii wapo waliopinga akiwepo George Mbowe na wenzake na hawa walikuwa vibaraka vya wazungu katika kuhakikisha Nchi inakubali UBEPARI na KUUWA UJAMAA.
Kikundi hiki cha watu wachache sana ila wenye nguvu kutoka ULAYA MAGHARIBI,(Kifedha na Kiuchumi) kwa kutumiwa kwao kama vibaraka walifanikiwa kuuondosha kabisa UJAMAA miaka ya 1990 wakati huo hatukuwa na upinzani.
UBEPARI uliwaharibu watu wengi waliokuwa karibu na rasilimali za taifa, uliwaongezea uchu wa kujilimbikizia Mali pamoja kujinufaisha wao binafsi. Mambo haya yalipingwa na wanaccm walioupenda UJAMAA toka miaka ya 1990 ambayo UBEPARI ulishika hatamu kama unavyoona leo vijana tunaopinga vitendo vya kifisadi na RUSHWA tukiongozwa na Rais wetu Magufuli, Katibu wa Uenezi na Itikadi wa CCM Ndugu Humphrey Polepole.
Kwa kuwa walikuwa wameshikilia madaraka kundi hili lilifanikiwa ku - suppress wale wote wanaoimba na kujifanya wajamaa na ili maisha yako yawe rahisi ilikuwa lazima ujipendekeze kwao na kuungana nao. Waliiba kwa ajili ya kujinufaisha wao binafsi lakini watanzania wengi walishindwa kuongea juu yao kwa kuwa walikuwa na nguvu ya madaraka.
Kwa waliozaliwa miaka ya 1990 kama wewe wakati haya yanatokea hawakuwa na utashi wa kutosha kuyaelewa(walikuwa watoto). Mambo haya yaliongezeka na UBEPARI ukajiongezea wanachama wake na ndipo tulipoanza kushuhudia Keki ya taifa inamegwa bila huruma na vijana walijipendekeza kwa mabepari haya ili tu wapate mabaki ya hizo keki.
Mambo haya yakawa wazi na wanachama wa UBEPARI wakawa wengi na wizi ukawa njenje hata watoto wadogo wakasikia habari hizi na kwa kuwa walikuwa na nguvu na walishikilia madaraka hakuna alieweza kufanya lolote; lakini bado wanaccm WAJAMAA mimi nawaita (MASALIA)walikuwa na imani ya kuishika dola siku moja na kuirudisha nchi mahala pake.
Leo wajamaa wameishika Dola na sasa nchi inarudishwa katika misingi yake. Kuna vita kubwa ya mabepari hawa na wajamaa na wanatumia hujuma za kila namna kuhakikisha wananchi wanaupinga UJAMAA. Toka mapasuko wa maslahi katika mambo hiyo ya WANAMTANDAO wakati wa kuwania Uraia 2015 wengi wao wameonekana wakikiama Chama Cha Mapinduzi na kuhamia CHADEMA huku wakipokelewa kwa nderemo na vifijo na wanachama wenzao walioko humo.
Kuna Mbinu wanaitumia baada ya kuona RAIS MAGUFULI AMEWASHIKA PABAYA. Mbinu hiyo ni kuwaandaa vijana kama Yeriko Nyerere ili kuhakikisha hakuna umoja wa kitaifa katika mambo ambayo yana maslahi mapana ya kitaifa. Hawa hupewa pesa kidogo sana kuzifanya kazi hizo.
KWA NINI WANALENGA KUVURUGA UMOJA WA KITAIFA?
1) Katika umoja kuna NGUVU
2) Katika umoja wa kitaifa kuna USHINDI Dhidi ya hawa maharamia wa rasilimali za nchi.
3) Katika umoja wa kitaifa UONGO NA UKWELI VITAJITENGA
4) Katika umoja wa kitaifa WATAJILIKANA NANI NI WASALITI.
5) Katika umoja wa kitaifa tutaondosha kabisa tabaka la WANYONYAJI N.K.
6) katika umoja wa kitaifa Maslahi ya Taifa yatapatikana na yatalindwa.
Hivyo basi mdogo wangu YERIKO nakushauri hii agenda ni kubwa sana kuliko uwezo wako wa kufikiri na kuandika. Wanaokutumia wanataka wakutoe nje ya mstari na utumike kuwatoa wengine nje ya mstari ili AGENDA hii kubwa ya kitaifa kurudisha Rasilimali za Taifa kutoka kwa wanyang'anyi hawa isifanikiwe.
Epuka kutumiwa ungana na Rais Magufuli kuikomboa nchi yako.
Hii AGENDA sio ya KISIASA ni ya KITAIFA ...........UTANZANIA KWANZA MENGINE BAADAE.
USIKU MWEMA WAZALENDO WOTE
CHIKAWE JR.