Mwana Mtoka Pabaya
JF-Expert Member
- Apr 22, 2012
- 15,118
- 16,485
Asante Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa katazo lako juu ya matumizi ya SHISHA, lakini upande wa pili, WATANZANIA WANAKUFA.
Jana imetokea ajali, mabasi mawili ya kampuni moja yakigongana na kuua watu 29+ ikiacha majeruhi wasio na idadi. Nasema majeruhi hawana idadi kwa kuwa, inapotokea ajali hawajeruhiwi walioko eneo la tukio tu, kuna wahanga wengine wako maili elfu kadhaa kutoka eneo la ajali.
Mheshimiwa Waziri Mkubwa, jana Mheshimiwa Rais ametuma salamu za rambi rambi kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida, akiwaombea heri majeruhi wapone haraka na roho za marehemu ziwekwe mahala pema peponi. Haya yote ni matukio, naomba niende sasa kwenye nalotaka kukusihi.
Mheshimiwa Waziri Mkuu, RAMBI RAMBI tumezipokea...sasa TUNAOMBA TUMAINI. Hali ilikofikia sasa, kusafiri na basi Tanzania ni sawa na kuonja sumu. Roho zetu kwa muda wote wa safari zinakabidhiwa 'wahuni' wasio na maadili wazifanye waonavyo inafaa. Mnapoishia kututumia salamu za rambi rambi, serikali inafahamu yanayoendelea?
Kwa mujibu wa majeruhi na baadhi ya madereva, kilichofanyika jana ni mchezo wa kawaida tu kwa madereva wa kampuni ile, wao wakikutana husalimiana kwa kuwashiana taa ikifuatiwa na kubadilishana njia, wa kushoto anahamia kulia na wa kulia anahamia kushoto...jana salamu ikaingia dosari, ndugu zetu wamekufa na sasa zahma inahamia kwa yatima na wajane...TANZANIA BIMA NI KWA MWENYE BASI, miguu yetu majaliwa.
Mheshimiwa Waziri Mkubwa, mimi sijui serikali inasubiri afe nani kwenye ajali ya basi ndio serikali ione kuwa kila Mtanzania ana ROHO MOJA TU. Hawa wamiliki wa mabasi, si wenzetu kwenye vilio vya ajali na matokeo yake. Basi linapopata ajali, huyu hufidiwa na BIMA akaendelea na biashara zake. Hasara anayopata huyu, si sawa na Mama Tupele wa Mabibo Makutano anayevunjika kiuno akiwa njiani kwenda Mbozi kumjulia hali binamu yake. Kuna TUHUMA nzito kuwa, matajiri wa mabasi huwaamuru madereva wao 'IENDE IRUDI, INADAIWA MKOPO' na katika hili madereva hawana kauli kwani kwa kazi zisizo na mkataba, dereva asiyemfurahisha tajiri huwekwa kando gari akakabidhiwa mwingine 'mwenye kichwa chepesi' ili aende sawa na mkopo.
Unielewe Mheshimiwa Waziri Mkuu, sisemi kuwa ajali ya jana imesababishwa na wamiliki, lakini ni ukweli kuwa wamiliki ndio wanaopelekea uwapo wa WAHUNI KWENYE USUKANI kwa kuwa siku zote wao hutafuta cheap labour.
Mheshimiwa Waziri Mkubwa, moja kati ya mabasi yaliyogongana jana, halikuwa na muda mrefu tangu liandikiwe fine kwa kosa la mwendokasi. Hapa kuna jambo baya sana ambalo serikali halilioni. Fununu za barabarani zinasema, wamiliki huwalipia madereva fine wanapokamatwa kwa mwendo kasi...sisi roho zetu zinalipwa na nani ikiwa hata kulipwa bima ni mtihani mzito? Tanzania yetu inaeleweka kwa kiwango cha elimu na ufahamu, TIRA wako na wahanga wa ajali au wako ofisini wanasubiri mashtaka? Nani anawatetea wanyonge kwenye majanga kama haya?
Mheshimiwa Waziri Mkuu, siasa iondoke barabarani. Watu 30 kufa kwa pamoja si jambo jepesi kama ambavyo hili litaishia hewani. Amiri Jeshi asiishie kutuma salamu za rambi rambi, tunataka tumaini. Kama rubani wa ndege ndogo ya abiria anasomeshwa miaka, huyu anayekabidhiwa roho 67 kwa masaa zaidi ya 8 anapatikana kwa mtindo gani, au ndio survival of the fittest?
Mheshimiwa Waziri Mkuu, nimalizie kwa kurudia kukuomba, siasa iondoke barabarani. Roho zetu zinadhulumika serikali ikiwa kimya. Salamu za rambi rambi zinatosha, sasa tunaomba tumaini. Hatujaishiwa nyenzo wala rasilimali watu katika hili. Unakosekana UTASHI WA SERIKALI kuona hatufi kinyama kama ilivyotokea jana...ajali na zibakie za bahati mbaya sio hizi za mifumo mibovu tafadhali. Hili jambo Waziri Mkubwa, linahitaji zaidi ya hotuba.