Kwako Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa

Mwana Mtoka Pabaya

JF-Expert Member
Apr 22, 2012
15,118
16,470
Asante Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa katazo lako juu ya matumizi ya SHISHA, lakini upande wa pili, WATANZANIA WANAKUFA.

Jana imetokea ajali, mabasi mawili ya kampuni moja yakigongana na kuua watu 29+ ikiacha majeruhi wasio na idadi. Nasema majeruhi hawana idadi kwa kuwa, inapotokea ajali hawajeruhiwi walioko eneo la tukio tu, kuna wahanga wengine wako maili elfu kadhaa kutoka eneo la ajali.

Mheshimiwa Waziri Mkubwa, jana Mheshimiwa Rais ametuma salamu za rambi rambi kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida, akiwaombea heri majeruhi wapone haraka na roho za marehemu ziwekwe mahala pema peponi. Haya yote ni matukio, naomba niende sasa kwenye nalotaka kukusihi.

Mheshimiwa Waziri Mkuu, RAMBI RAMBI tumezipokea...sasa TUNAOMBA TUMAINI. Hali ilikofikia sasa, kusafiri na basi Tanzania ni sawa na kuonja sumu. Roho zetu kwa muda wote wa safari zinakabidhiwa 'wahuni' wasio na maadili wazifanye waonavyo inafaa. Mnapoishia kututumia salamu za rambi rambi, serikali inafahamu yanayoendelea?

Kwa mujibu wa majeruhi na baadhi ya madereva, kilichofanyika jana ni mchezo wa kawaida tu kwa madereva wa kampuni ile, wao wakikutana husalimiana kwa kuwashiana taa ikifuatiwa na kubadilishana njia, wa kushoto anahamia kulia na wa kulia anahamia kushoto...jana salamu ikaingia dosari, ndugu zetu wamekufa na sasa zahma inahamia kwa yatima na wajane...TANZANIA BIMA NI KWA MWENYE BASI, miguu yetu majaliwa.

Mheshimiwa Waziri Mkubwa, mimi sijui serikali inasubiri afe nani kwenye ajali ya basi ndio serikali ione kuwa kila Mtanzania ana ROHO MOJA TU. Hawa wamiliki wa mabasi, si wenzetu kwenye vilio vya ajali na matokeo yake. Basi linapopata ajali, huyu hufidiwa na BIMA akaendelea na biashara zake. Hasara anayopata huyu, si sawa na Mama Tupele wa Mabibo Makutano anayevunjika kiuno akiwa njiani kwenda Mbozi kumjulia hali binamu yake. Kuna TUHUMA nzito kuwa, matajiri wa mabasi huwaamuru madereva wao 'IENDE IRUDI, INADAIWA MKOPO' na katika hili madereva hawana kauli kwani kwa kazi zisizo na mkataba, dereva asiyemfurahisha tajiri huwekwa kando gari akakabidhiwa mwingine 'mwenye kichwa chepesi' ili aende sawa na mkopo.

Unielewe Mheshimiwa Waziri Mkuu, sisemi kuwa ajali ya jana imesababishwa na wamiliki, lakini ni ukweli kuwa wamiliki ndio wanaopelekea uwapo wa WAHUNI KWENYE USUKANI kwa kuwa siku zote wao hutafuta cheap labour.

Mheshimiwa Waziri Mkubwa, moja kati ya mabasi yaliyogongana jana, halikuwa na muda mrefu tangu liandikiwe fine kwa kosa la mwendokasi. Hapa kuna jambo baya sana ambalo serikali halilioni. Fununu za barabarani zinasema, wamiliki huwalipia madereva fine wanapokamatwa kwa mwendo kasi...sisi roho zetu zinalipwa na nani ikiwa hata kulipwa bima ni mtihani mzito? Tanzania yetu inaeleweka kwa kiwango cha elimu na ufahamu, TIRA wako na wahanga wa ajali au wako ofisini wanasubiri mashtaka? Nani anawatetea wanyonge kwenye majanga kama haya?

Mheshimiwa Waziri Mkuu, siasa iondoke barabarani. Watu 30 kufa kwa pamoja si jambo jepesi kama ambavyo hili litaishia hewani. Amiri Jeshi asiishie kutuma salamu za rambi rambi, tunataka tumaini. Kama rubani wa ndege ndogo ya abiria anasomeshwa miaka, huyu anayekabidhiwa roho 67 kwa masaa zaidi ya 8 anapatikana kwa mtindo gani, au ndio survival of the fittest?

Mheshimiwa Waziri Mkuu, nimalizie kwa kurudia kukuomba, siasa iondoke barabarani. Roho zetu zinadhulumika serikali ikiwa kimya. Salamu za rambi rambi zinatosha, sasa tunaomba tumaini. Hatujaishiwa nyenzo wala rasilimali watu katika hili. Unakosekana UTASHI WA SERIKALI kuona hatufi kinyama kama ilivyotokea jana...ajali na zibakie za bahati mbaya sio hizi za mifumo mibovu tafadhali. Hili jambo Waziri Mkubwa, linahitaji zaidi ya hotuba.
 
Mkuu unaniliza eti... kuna wakati nawaza labda ni UGAIDI au maana sielewi. Mungu nakushukuru kwa kunilinda.
 
Mimi sielewi, hivi ukiondoa ajali za barabarani, kuna janga gani lenye kuondoa roho za watu kwa mkupuo hapa Tanzania? Kikizuka kipindupindu, attention ya serikali inapatikana, lakini mbona huu ugaidi wa kwenye lami unatumaliza?
 
Mods, hili sio jambo la kisiasa. Siasa ndio imetufikisha hapa. Tangu madereva waanze kudai mikataba ya kazi ni siasa tu imefanyika. Hakuna msingi unaojengwa wa kuona ajali zinapungua, mambo yale yale na kampeni za zimamoto. Ukifika mwezi wa 12 utawaona SUMATRA na Polisi bize sana na wauza tiketi na udhibiti barabarani unakuwa wa kiwango cha juu, ikipita hiyo tunaendelea kuuliwa...siasa kwenye roho zetu.
 
Daaah kwa kweli waraka nzuri sana, naamini ID ya PM humu jf imeshaona huu waraka na sasa anatafakari lakuongea. Soon ata-respond
 
Asante Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa katazo lako juu ya matumizi ya SHISHA, lakini upande wa pili, WATANZANIA WANAKUFA.

Jana imetokea ajali, mabasi mawili ya kampuni moja yakigongana na kuua watu 29+ ikiacha majeruhi wasio na idadi. Nasema majeruhi hawana idadi kwa kuwa, inapotokea ajali hawajeruhiwi walioko eneo la tukio tu, kuna wahanga wengine wako maili elfu kadhaa kutoka eneo la ajali.

Mheshimiwa Waziri Mkubwa, jana Mheshimiwa Rais ametuma salamu za rambi rambi kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida, akiwaombea heri majeruhi wapone haraka na roho za marehemu ziwekwe mahala pema peponi. Haya yote ni matukio, naomba niende sasa kwenye nalotaka kukusihi.

Mheshimiwa Waziri Mkuu, RAMBI RAMBI tumezipokea...sasa TUNAOMBA TUMAINI. Hali ilikofikia sasa, kusafiri na basi Tanzania ni sawa na kuonja sumu. Roho zetu kwa muda wote wa safari zinakabidhiwa 'wahuni' wasio na maadili wazifanye waonavyo inafaa. Mnapoishia kututumia salamu za rambi rambi, serikali inafahamu yanayoendelea?

Kwa mujibu wa majeruhi na baadhi ya madereva, kilichofanyika jana ni mchezo wa kawaida tu kwa madereva wa kampuni ile, wao wakikutana husalimiana kwa kuwashiana taa ikifuatiwa na kubadilishana njia, wa kushoto anahamia kulia na wa kulia anahamia kushoto...jana salamu ikaingia dosari, ndugu zetu wamekufa na sasa zahma inahamia kwa yatima na wajane...TANZANIA BIMA NI KWA MWENYE BASI, miguu yetu majaliwa.

Mheshimiwa Waziri Mkubwa, mimi sijui serikali inasubiri afe nani kwenye ajali ya basi ndio serikali ione kuwa kila Mtanzania ana ROHO MOJA TU. Hawa wamiliki wa mabasi, si wenzetu kwenye vilio vya ajali na matokeo yake. Basi linapopata ajali, huyu hufidiwa na BIMA akaendelea na biashara zake. Hasara anayopata huyu, si sawa na Mama Tupele wa Mabibo Makutano anayevunjika kiuno akiwa njiani kwenda Mbozi kumjulia hali binamu yake. Kuna TUHUMA nzito kuwa, matajiri wa mabasi huwaamuru madereva wao 'IENDE IRUDI, INADAIWA MKOPO' na katika hili madereva hawana kauli kwani kwa kazi zisizo na mkataba, dereva asiyemfurahisha tajiri huwekwa kando gari akakabidhiwa mwingine 'mwenye kichwa chepesi' ili aende sawa na mkopo.

Unielewe Mheshimiwa Waziri Mkuu, sisemi kuwa ajali ya jana imesababishwa na wamiliki, lakini ni ukweli kuwa wamiliki ndio wanaopelekea uwapo wa WAHUNI KWENYE USUKANI kwa kuwa siku zote wao hutafuta cheap labour.

Mheshimiwa Waziri Mkubwa, moja kati ya mabasi yaliyogongana jana, halikuwa na muda mrefu tangu liandikiwe fine kwa kosa la mwendokasi. Hapa kuna jambo baya sana ambalo serikali halilioni. Fununu za barabarani zinasema, wamiliki huwalipia madereva fine wanapokamatwa kwa mwendo kasi...sisi roho zetu zinalipwa na nani ikiwa hata kulipwa bima ni mtihani mzito? Tanzania yetu inaeleweka kwa kiwango cha elimu na ufahamu, TIRA wako na wahanga wa ajali au wako ofisini wanasubiri mashtaka? Nani anawatetea wanyonge kwenye majanga kama haya?

Mheshimiwa Waziri Mkuu, siasa iondoke barabarani. Watu 30 kufa kwa pamoja si jambo jepesi kama ambavyo hili litaishia hewani. Amiri Jeshi asiishie kutuma salamu za rambi rambi, tunataka tumaini. Kama rubani wa ndege ndogo ya abiria anasomeshwa miaka, huyu anayekabidhiwa roho 67 kwa masaa zaidi ya 8 anapatikana kwa mtindo gani, au ndio survival of the fittest?

Mheshimiwa Waziri Mkuu, nimalizie kwa kurudia kukuomba, siasa iondoke barabarani. Roho zetu zinadhulumika serikali ikiwa kimya. Salamu za rambi rambi zinatosha, sasa tunaomba tumaini. Hatujaishiwa nyenzo wala rasilimali watu katika hili. Unakosekana UTASHI WA SERIKALI kuona hatufi kinyama kama ilivyotokea jana...ajali na zibakie za bahati mbaya sio hizi za mifumo mibovu tafadhali. Hili jambo Waziri Mkubwa, linahitaji zaidi ya hotuba.
Asante sana ndugu yangu, kwani umenigusa sana, mimi ni senior driver. Lakini nasikitika sana tena zaidi ya sana, hawa madereva wenye matendo kama hayo wanaisababisha fani yetu kuonekana sio taaluma kama taaluma nyingine, kama vile:- Rubani, Tabibu na n.k. Kama ulivyotangulia kusema kuwa:-salam za rambi rambi kutoka serikalini sasa inatosha. Serikali inatuahidi kitu gani kuhusiana na usalama wa raia ktk sekta ya usafiri wa mabasi ya kwenda mikoani.
 
Rejea mgogoro wa mikataba ya kazi kati ya madereva na waajiri. Sekta ya uchukuzi/usafirishaji kwa kiasi kikubwa imekamatwa na hawahawa viongozi wetu wa kisiasa.
 
Kwa kifupi hao sio madereva, hao ni waendesha magari. Dereva ni sawa na rubani endapo akiwekwa kwenye mfumo sahihi na mazingira mazuri. Kwa ilivyo sasa, mazingira na mifumo ya ajira za waendesha mabasi ya mkoani, umeruhusu wahuni kuwepo kwenye fani.

Udereva umekuwa kimbilio la makapi wakati ilipaswa iwe kazi ya watu makini wenye uelewa mkubwa. Sasa tunayoyaona ni mwendelezo wa siasa kila sehemu. Tangu lile agizo la wamiliki kuwapa mikataba madereva litolewe, hiyo mikataba imeshatolewa?

Utani ni mwingi, ndio maana kwenye bandiko langu nimemuuliza Mheshimiwa Waziri Mkuu, MPAKA AFE NANI? Maana kwingineko tumeshaona, kuna tofauti ya kasi ya upelelezi akiuliwa fulani, tofauti na akiuliwa 'fulani', kwa hiyo labda na huku mpaka afe 'mtu fulani' ndio serikali ione namba za vifo kwa macho sawa na mwananchi.
 
Asante mleta mada, Hili ni jambo muhimu sana ambalo serikali inatakiwa kulipa umuhimu unao stahili ili kuwa dhibiti hawa madereva waovu
 
Asante sana ndugu yangu, kwani umenigusa sana, mimi ni senior driver. Lakini nasikitika sana tena zaidi ya sana, hawa madereva wenye matendo kama hayo wanaisababisha fani yetu kuonekana sio taaluma kama taaluma nyingine, kama vile:- Rubani, Tabibu na n.k. Kama ulivyotangulia kusema kuwa:-salam za rambi rambi kutoka serikalini sasa inatosha. Serikali inatuahidi kitu gani kuhusiana na usalama wa raia ktk sekta ya usafiri wa mabasi ya kwenda mikoani.

Wewe kama senior driver, ulikua na maoni gani juu ya serikali ifanye nini ili kuokoa roho na viungo vya ndugu zetu vinavyokatika kila kukicha..!?
 
Asante kwa swali lako ndugu, mimi kama Senior driver nashauli hivi kwa serikali: Serikali inatakiwa ihakiki mikataba ya madereva wanaoajiliwa na wamiliki wa mabasi pamoja na magari ya mizigo. Tatizo kubwa lipo kwa wamiliki wa vyombo hivyo,kwani utakuta wanaajili madereva ambao hawana sifa, ili kwamba wawalipe malipo kidogo (cheap labor) kuna baadhi ya madereva hapa mjini wanaweza kuwekwa mahabusu wiki moja mpaka mwezi mmoja usione ndugu, mke, rafiki yake yeyote kuja kumuwekea dhamana, sana sana utakuta ni m'miliki wa hilo gari katuma mtu. Huyo atakuwa ni dereva asiefaa kabisa, ni hatari!! utakuta dereva hana mke, hana watoto hana familia yeyote inayomtegemea, hajulikani anaishi wapi,kwa hakika dereva kama huyo hatakuwa dereva bora.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom