Kwako Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, majibu yako juu ya tume huru na mikutano

Abdul Nondo

JF-Expert Member
Oct 28, 2016
515
2,875
Pole na majukumu makubwa ya kujenga taifa letu.

Nimesikia majibu yako makuu mawili uliyokuwa unamjibu kiongozi mkuu wa kambi ya upinzani Bungeni Mh. Freeman Mbowe, juu ya zuio la mikutano na pia Tume Huru ya Uchaguzi.

Mh. Waziri Mkuu, mimi nitaanza na jibu lako la kwanza kuhusu zuio la mikutano kwa vyama pinzani.

Mh. Waziri Mkuu, umejibu kwamba hakuna zuio lolote la mikutano kwa vyama pinzani kufanya shughuli za kisiasa, badala yake kuna utaratibu tuu kwamba kiongozi anapaswa kufanya mkutano katika eneo lake analowakilisha au alilochaguliwa.

Mh. Waziri Mkuu, nchi yetu inaongozwa kwa mujibu wa sheria,ila katika majibu yako kuna ukakasi uliojitokeza uliposema "Kiongozi afanye mikutano katika eneo lake". Je huu utaratibu ni kwa mujibu wa sheria ipi ya nchi yetu?

Mh. Waziri Mkuu, tusome kwa pamoja sheria yetu ya vyama vya siasa ya 1992, kifungu cha 11(1)a

11 (1) Every party which has been provisionally or fully registered shall be
entitled,
a) to hold and address public meetings in *any area in the United Republic* after
giving notification to the police officer in-charge of the area concerned.

Maana yake "kila chama chenye usajili wa awali au wote kitakuwa na haki ya "kufanya mikutano ya wazi katika eneo lolote ndani ya jamhuri ya Tanzania", baada ya kutoa taarifa polisi.

Mh. Waziri Mkuu, naomba kuuliza ni lini serikali ilipeleka muswada Bungeni, bunge likafuta kipengele cha 11(1) kufanya mikutano eneo lolote la jamhuri na kuingiza kipengele au utaratibu wa kufanya mikutano katika eneo husika la kiongozi fulani? Kuna hiyo Sheria?

Mh.Waziri Mkuu, ukiwa mbele ya Bunge ulikataa kwamba serikali haiongozi kibabe, je utakubaliana na mimi kuwa serikali kutoa agizo linalokiuka sheria ya vyama vya siasa ni kuongoza kibabe?

Tume huru ya uchaguzi.

Mh. Waziri Mkuu tuje katika jibu lako la pili ulilomjibu Mh. Freeman Mbowe Bungeni juu ya tume huru ya uchaguzi.

Ulijibu kwa kusema Tume yetu ya uchaguzi ni tume huru, kwa mujibu wa katiba yetu ibara ya 74 ibara ndogo ya 7,11 na 12.Kwamba tume hii kisheria ni huru na haiwezi ingiliwa hivyo chombo huru hiki ndio tume huru.

Mh. Waziri Mkuu wetu, kutuaminisha kwamba tume yetu ya uchaguzi ni huru sababu imeandikwa katika katiba ni sawa na kutuaminisha Tanzania ni nchi ya kijamaa na kujitegemea sababu imeandikwa katika katiba katika utangulizi, pia katika ibara ya 9 ikiwa sio kweli, Tanzania sasa ni nchi ya kibepari kutokana sifa au sababu kadha zinazojulikana.

Mh. Waziri Mkuu, hivyo hivyo katika suala la tume huru, Tanzania haina tume huru ya uchaguzi sababu ya sifa na sababu kadhaa hapo chini zinazofahamika.

Mh. Waziri Mkuu ukisoma ibara hiyo ya 74 (1) inasema "Kutakuwa na Tume ya Uchaguzi ya Jamhuri ya
Muungano ambayo itakuwa na wajumbe wafuatao watakaoteuliwa
na Rais"

Mh. Waziri ukisoma hiyo ibara tu hapo juu,unapata kujua kabisa kwamba Tume yetu sio huru sababu Rais amepewa mamlaka yote na makubwa ya kuteua wajumbe, mwenyekiti pia makamu bila mchakato wowote wa kuchuja wajumbe hao kabla ya Rais kuteua, pia Rais ana mamlaka yote ya kutengua wajumbe bila mchakato wowote wa kuthibitisha sababu za hao wajumbe au mwenyekiti kutenguliwa, Uhuru wa chombo chochote haupimwi kwa kuandikwa katika katiba.

Uhuru wa chombo unapimwa kuanzia namna ya upatikanaji wa wajumbe wake na namna ya kuondoshwa ofisini wajumbe hao.

Mh. Waziri Mkuu, naomba nitoe mifano ya aina ya Tume huru tunayoizungumzia kutoka nchi 2 ndani ya Afrika.

1. Afrika ya Kusini
2. Kenya.

1. Afrika ya Kusini

Mh. Waziri Mkuu tukisoma sote sheria ya tume ya uchaguzi ya Afrika ya Kusini yaani Electoral commission act of South Africa No.51 of 1996. Inaelezea mchakato wa kupatikana wajumbe wa tume huru ya uchaguzi hadi namna ya kuwaondoa ofisini.

Kwanza kuna Panel iliyoelezewa kifungu cha 6(3), inayojumuisha wawakilishi kutoka mahakama (Jaji), tume ya haki za binadamu na sehemu zingine, Panel hii kwa mujibu wa kifungu cha 6(4) ndio inayopendekeza list ya wajumbe nane pendekezwa.

Ambapo hao wajumbe nane wanapelekwa katika kamati ya Bunge (Committee of national assembly) kuwa nominated alafu watakaopita wanapelekwa katika Bunge (National assembly) ili kupendekezwa kwa resolution ya wabunge wengi (Kifungu cha 6 kifungu kidogo cha 2 c na d ).

Baada ya hapo ndio Rais sasa anateua (designate) mwenyekiti na makamu kutoka katika wajumbe waliopitishwa na Bunge (kifungu cha 8), Ila tume yetu ambayo Mh.waziri mkuu unaita ni huru hatuna huu utaratibu mamlaka yote yapo kwa Rais, hivyo ana mwanya wa kuweka rafiki au jamaa zake, ndugu, makada wa chama, yeyote anayemuhutaji hivyo hawawezi kuwa huru hata kidogo.

Kuondoa wajumbe wa Tume (The removal).

Mh. Waziri Mkuu, Tume huru tunayoizungumzia hapa ni ile ambayo Rais hana mamlaka ya moja kwa moja ya kuondosha au kutengua wajumbe bila uthitibitisho wa tuhuma au sababu za kuwaondoa wajumbe hao.

Mfano, Afrika ya kusini katika sheria yao hiyo juu kifungu cha 7, lazima mahakama ya kikatiba ijiridhishe, kamati ya Bunge pia maamuzi ya Bunge kwa resolution ya wabunge wengi kwamba mjumbe au wajumbe wa tume wanapaswa kuondolewa au laa.Mwisho Rais anapewa taarifa ya tengua au laa.

Mh. Waziri Mkuu kwetu Tanzania ni tofauti ,tusome ibara ya 75(5) "Rais aweza tu kumwondoa katika madaraka Mjumbe wa
Tume ya Uchaguzi kwa sababu ya kushindwa kutekeleza kazi
zake, ama kutokana na maradhi au sababu nyingine yoyote, au kwa sababu ya tabia mbaya au kupoteza sifa za kuwa mjumbe".

Nani atajua kwamba sababu hizo za kuwaondoa ni za ukweli? Kwa namna hii wajumbe au mwenyekiti wa tume hawawezi kuwa huru katika utendaji wao.

Kenya.
Pia ukisoma katiba ya Kenya ya 2010 ibara ya 250 (2) a,b na c pia ile ya 251 (kuwaondoa wa wajumbe) hakuna tofauti sana Afrika ya kusini.

Hii ndio aina ya tume huru tunayohitaji Mh. Waziri Mkuu wetu Kassim Majaliwa

Shukrani sana

Abdul Nondo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu Abdul Nondo wewe ni nondo kweli kweli...na msemakweli ni mpenzi wa mungu ila hapa kwetu siyo...ya bayana tunayaficha ila yenye walakini ndiyo tunayaweka hadharani..hawachelewi kukuambia uthibitishe uraia wako kwa kuwailisha hati yako ya kifo japo ungali hai.
 
Husitegemee waziri mkuu atakuja kutoa majibu yatakayomuudhi bosi wake wa magogoni hata siku moja.

NB. Ile ripoti ya ajali ya ndugu zetu wa Morogoro ilishakabidhiwa kwa waziri mkuu ?
 
unadhani waziri mkuu ni wale wazee wako wa kigoma wanaosifiwa uchawi


USSR

Sent using Jamii Forums mobile app

Huyo waziri mkuu hafuati katiba inasema nini, bali anaangalia Magufuli anataka nini. Magufuli ndiye aliyepiga marufuku vyama vya siasa kufanya siasa nchi nzima, kwa hofu ya ccm kukutana na wakati mgumu. Hivyo huyo waziri mkuu hakuwa na uwezo wowote wa kuzuia anachotaka rais, au kuangalia katiba inasema nini.

Nimecheka sana waziri mkuu aliposema tume ni huru kwakuwa imeandikwa kwenye katiba. Lakini wakati huohuo ruhusa ya kufanya mikutano nchi nzima ni ruhusa iliyo kwenye katiba, lakini haifuatwi!
 
Nondo moyoni mwangu unaniaminisha kuwa una uchungu na hii nchi. Sina wasiwasi kabisa na hilo ila shida kubwa sana uliyonayo ni moja Siasa za Tanzania ni kama comedy kwa maana hakuna mwanasiasa wa kweli kuanzia ccm mpaka Act.

Wote ni matapeli. The only way ya kufikia ninyi kizazi kipya kule mnakotaka mfikie mnatakiwa kuachana na hayo makapi ama jipenyezeni mchukue hatamu kwenye uongozi.

Wengine tulikua tunapiga chapuo kama ninyi miaka hiyo kabla hamujazaliwa tukaishia kurudishwa nyuma na viongozi wetu ambao mpaka sasa baadhi ndiyo viongozi wakuu upinzani.

Mabadiliko yaanzie huko upinzani washaurini viongozi wakiwa kwenye vikao vya maana kama kubadili katiba wasipende kususia vikao.

Kenya wslitwangana ngumi South Afrika wanatolewa kwa nguvu vikaoni Tanzania wanavaa suti nyeusi wana sign attendance kupata pesa halafu wanatoka nje. Unawezaje kumsusia fisi mfupa ukidhani takuachia?
 
Back
Top Bottom