Msemakweli Chakubanga
Member
- Dec 13, 2018
- 30
- 140
KWAKO THADEI OLE MUSHI.
Jana 12:15pm,29/12/2018.
Ndugu Thadei Ole Mushi ikiwa ni jina lako halisi au nickname ni zaidi ya miaka mitatu nasoma maandiko yako na kwa asilimia 80 ni kusifia Zitto, Lissu na kuandika kwa dhihaka kila kinacho fanywa na Chama au Serikali kuunga mkono hoja fifishi tu kubeza WanaCcm na kutia kauli za kuudhi dhidi ya wanaCcm hasa Vijana kwa kuwakebehi eti hakuna watu smart tena,hivi kama CCM hakuna watu smart mbona inafanikiwa kwa kujirekebisha yenyewe ndani kwa ndani.
Katika andishi fikra siamini kama upo katika hilo unalolisema la kukisaidia chama bali ni maoni yako pengine kwa kukosa uteuzi baada ya wenzako akina kimeta wa mpui kula shavu.
Katika fikra dhihirishi ya mawazo yako tunaweza kusoma kitu chonganishi na vurugishi sio kwa sababu huwa unakosea basi huwezi kupatia,hapana unaweza kupatia kwa asilimia 20 na ukakosea kwa asilimia 80.
Tofauti yangu Mimi Mwana CCM na wewe fake wa mitandaoni ukitumia jina fake ni mythical fallacy ambayo unatumia kupresent hoja dunduizi hasa za kuonyesha madhaifu ya CCM kwa Upinzani,kwa kutumia Ufahamu rasmi uliopo katika utaratibu(School of thoughts) hasa ndani ya CCM na jumuiya zake.
Chama chetu kina taratibu zake katika kukikosoa hivyo ni vyema ungejielekeza huko kwa kubainisha upungufu na hayo unayoyajengea hoja na kujiita "MwanaCCM" nadhani ungeeleweka na mchango wako kupewa umuhimu mkubwa.
Sidhan kama ufanyavyo mitandaoni ni sehemu muafaka...mawazo yako yanaweza kuchukuliwa kama propaganda tu dhidi ya Jumuiya za CCM mathalani UVCCM.
-Mzingo na Mviringo wa Maoni ya Mwanachama kwa Chama chake.
Kifalsafa na kiitikadi hasa ya Ujamaa ambayo Chama chetu cha CCM inaenenda,ni kusema ukweli daima na fitna kwetu mwiko,lakini tunayafanya kwa utaratibu tuliojiwekea ndani ya vikao vya CCM,na si kama kufungua ukurasa na kuanza kurusha vijembe,hapana.
Kitacho cha andiko hili ni kukufahamisha namna sahihi ya kufikisha ujumbe kama kweli unataka kukisaidia Chama chako pendwa cha CCM kama usemavyo.
Chama chetu kina taratibu zake katika kukikosoa hivyo ni vyema ungejielekeza huko kwa kubainisha upungufu na hayo anayoyajengea hoja nadhani angeeleweka na mchango wako kupewa umuhimu mkubwa.
Ndugu Thadei Ole Mushi hiyo mitazamo yako ungeipeleka katika vikao vya ndani vya Chama au vya UVCCM kwa andiko maalumu la kukisaidia chama,na kuepusha upotofu wa tunachokiona mitandaoni kama umekivunjia heshima chama na sidhani kama wanachama tutaweza kujifunza kwa vijembe na dharau za muaniko wako wa madhaifu yetu huku mitandaoni.
Binadamu ana tabia na aibu zake hivyo ukimuweka hadharani kwa kubainisha makosa au madhaifu yake mbele ya jamii ni kumnyong'onyesha na kumuua na kumfanya asifae kwa namna yoyote mbele ya jamii,iweje utoe siri za Baba ako na Mama mbele ya hadhara!? Ni dhahiri huna adabu.
Ndugu Thadei Ole Mushi sisi wanaCCM tunatoa michango inayojenga na si ile isiyo na tija na hasa yenye dhana vurugishi kutoka Chadema na Act,ilihali tunaweza kuandika.
-Falsafa,Mantiki na Muktadha wa andiko hili.
Naomba nieleze hupa kuwa, Mh Rais wetu Dr John Pombe Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wa Taifa wa CCM, amefanya kazi kubwa mno kwa kipindi kifupi cha utawala wake.
Serikali yetu imefanya kazi kubwa, Chama chetu CCM kimetekeleza Ilani ya Chama kwa vitendo. Lakini sio watanzania wote wanaona haya, wanaomchukia Mh Rais wetu na Serikali yake wapo na sauti zao zimesambaa kama sumu,hadi unajiuliza lipi jema kwao watu hawa.
Ukiwauliza sababu za kumchukia Mh Rais hawana, lakini ile sumu imefika mbali hasa katika mawanda mapana ya kimataifa. Tafadhali ndugu zangu tusiichafue nchi yetu kwa maslahi ya waliokuwa wakoloni wetu,wazungu ambao ni mabeberu katika nyanja ya maendeleo yetu, muhimu tunapoelekea 2020, tusidharau hizi kelele za akina zitto, lisu, nyarandu na wengine wote ipo nguvu ya siri,tuliona katika filamu ya Sarafina,wakati wakipigania Uhuru akina Sabela waliungana na makaburu kwa ujira wa kipande cha fedha,
Sina hakika kama kina Lissu,Zitto,Mbowe,Ansbert Ngurumo,na akina Chahali wakiwa wamejificha Ulaya wanapiga kelele za bure, lazima kuna nguvu wanayoitegemea.Ndugu Thadei Ole Mushi kama unavyojiita Mzalendo na MwanaCCM kazi ya uandishi wako uliyotakiwa kuifanya ni kuwaumbua pale tunapobaini mambo yao maovu na kuyashuhudia kwa umma kazi inayofanywa na Serikali yetu kutatua kero za Wananchi.
* Kumbukeni mabaya husambaa kwa haraka kuliko mema lakini daima mwisho wa siku mema ushinda uovu*
-Stakeholders Management,Damage Control,and Communication Management.
Mh Rais Magufuli amekuwa katika Uongozi hasa katika nyanja za kuwaweka pamoja wadau,kupata jibu la tatizo na Mawasiliano kwa lugha rahisi kwa washikadau na Wananchi kwa ujumla,Wapo watu, wanasema kuwa Rais Magufuli ametengeneza tatizo na kisha amelitatua, yaani ameleta kikokotoo cha kuwaumiza wafanyakazi na kisha amekifuta ili apate kiki ya kisiasa,ha ha haikuwa hivyo maana alisaini sheria isiyo na kanuni ya kikokotoleo.
Rais Magufuli aliposaini sheria hii ya mafao, haikuwa na kipengele chenye kikokotoo ambacho kimetugawa na kuleta mjadala mkubwa. Kikokotoo hiki kimewekwa kwenye kanuni, kanuni inatungwa na kusainiwa na waziri, na sheria haimuelekezi Waziri kutunga kanuni baada ya kushauriana na Rais. Sana sana Waziri anaweza kushauriana na AG, Wataalamu wa mifuko ya hifadhi, na watu wa ngazi yake na kutunga kanuni.
Kwa hiyo, kama kikokotoo hiki kiliingizwa kimahsusi kwenye kanuni, Rais hahusiki hata kidogo.
Mara nyingi Rais wa taifa lolote lile ni mtu mwenye taarifa za kutosha,Rais ndiye RAIA namna moja mwenye taarifa za kina kuhusu kila jambo kwenye nchi yake akipokea ripoti takribani kutoka taasisi zaidi za 50 zenye taarifa mahsusi kutoka katika kila nyanja, Rais ana taarifa za kutosha kuhusu masuala haya ya kikokotoo kuliko sisi wote tulioko mtandaoni na majumbani, na sote tunamjua Rais Magufuli ni mfuatiliaji, ana data na humdanganyi.
Kwa hiyo, Ndugu Thadei Ole Mushi kumsifia kwako Mh Esther Bulaya ni sawa na kumsifia mtoto anayekula bure nyumbani ikiwa Baba ndiye mtoa hela ya matumizi nyumbani,
Nikujuze tu Ndugu Thadei Ole Mushi ya kwamba suala hili ambalo Rais Magufuli amelitolea maamuzi jana, analijua na kulifahamu kuliko sisi sote. Mjadala wa kikotoo Mh Rais ameufikisha mwisho na hatutakijadili hadi mwaka 2023.
Ahsante 2018,Niwatakie heri ya Mwaka Mpya 2019,Mungu mbariki Rais wetu,John Magufuli,Mungu ibariki Tanzania.
Nikiishia hapa,Mimi ni,
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.