GJHariohay
JF-Expert Member
- Oct 24, 2013
- 1,041
- 1,161
Magufuli Tumekukosea Nini??
Nayaandika haya kwa machungu makubwa sana.
Ulituomba kura, uliongea kwa uchungu sana ukidai unahitaji kuwasaidia Watanzani, ulilia hadi machozi majukwaani, uliishiwa mpaka sauti kwa kueleza machungu yako uliyokuwa ukiyapata kwa sababu ya umaskini, uduni wa maisha, Ajira kwa Vijana, Elimu kwa mtoto wa Maskini, mateso ya wamachinga, Mama ntilie , wakulima, wafugaji, wavuvi , wafanyabiashara n.k.
Hakika tuliona neema kwako kipindi kile, tukajua Israeli sasa ameshuka Tanzania.
Mh Magufuli nayaandika haya kwa machungu mno, maisha yamekuwa mabaya sana mtaani, vijana wanazagaa tu, kila mtu amebaki kutafuta kifungua kinywa na ili mradi tumbo lishibe, wasomi wanalia kila kona ya nchi, vijana wengi wamekondeana, hawana afya, watu wana stress kila mahali, sio watumishi wa Mungu, sio wafanyabiashara, sio wanafunzi, sio wafugaji, sio wakulima, sio machinga wala mama Ntilie. Vijana wanaonekana wazee kabla ya umri, stress zimejaa kwa kila famili nchi nzima, Tatizo ni nini , tumekosea wapi Ndugu yetu Magufuli,,,,,,,
Matukio ya mauaji, utekaji, ujambazi, majanga yenye sura ya kukomoa yamekuwa kawaida tena maskioni mwa Watanzani. Roho ya mtu kutolewa kwa sasa imekuwa kawaida na kutolewa majibu marahisi tu "Watu wasiojulikana"
Sio viongozi , sio raia, sio wasanii, sio vijana wala wazee wanapotezwa kila uchwao, ni wapi Magufuli tulipokosea??
Maisha yameturudisha miaka 70 nyuma enzi za mkoloni ambapo Mtu mweusi anachukuliwa kama sio Binadamu, hana haki yeyote katika maisha yake. Hakika vijana ambao tuna maono ya kuwa na maisha yetu binafsi kwa ajili ya baadae tayari tumepoteza direction ya maisha kabisa, Vijana tunaogopa hata kuoa, umri unaenda, sijui tutakuwa Taifa la namna gani.
Magufuli umeyaharibu maisha, vijana wengi tumesoma lakini hatuna mchango wowote kwa Taifa letu, tumekaa mitaani, tunaomba Mungu usiku na mchana Miujiza itokee tule tushibe tulale, matumaini ya wazazi wetu kwetu hayapo tena. Kweli sijui tumekosea wapi kwako Mzee wetu.
Tunaishi kwa maisha ya wasiwasi, hakuna mwenye uhakika wa kesho yake, sijui kwanini umeshindwa kuelewa hii hali mpaka sasa, Najua kiyoyozi , misafara ya kifahari ya magari zaidi ya 200 ambayo yamezingirwa kwa mitutu ya Bunduki pengine yanakufanya usielewe nini kinaendelea nje, tunaomba uelewe tayari nchi haina mwelekeo wenye matumaini yeyote. Hakuna sera rafiki inayoonekana mpaka sasa, najua unaweza kupata huu ujumbe lakini bado ukasema kwa lugha yako ile ya kiyunani, " FANYA KAZI".
Magufuli tunaomba uelewe hakuna binadamu mkamilifua, wote tumekuja kwa njia moja na kwa njia moja tutaondoka, haijalishi mwingine alikuwa Rais, waziri n.k , elewa manung'uniko haya hayataishia kwenye kizazi hiki tu, Vizazi zaidi ya 3 vitanung'unika juu yako hata ukiwa kaburini, Watoto watalia, wataomboleza kwa ugumu wa maisha wanaopata wengine hawatosoma na kufikia ndoto zao sawa sawa, wengi watasema. "maisha yalikuwa magumu sana ningesoma vizuri mimi"
Ujumbe huu nimeuandika nikiwa na machungu sana, Taifa linapita katika mapito magumu mno, hata uhuru wa kuabudu unanyimwa na utawala wako, Yalifanyika maombi mengi sana kukuombea, viwanjani, makanisani, misikitini mpk chini ya miti. Lakini kumuombea mgonjwa kwa ibada na imani imekuwa shida leo kisa ni wa itikadi tofauti, Naomba Israeli akutembelee katika hili na anene kwa njia zote nawe.
Magufuli kumbuka hata wewe hauna hati miliki yeyote ya Kuishi duniani milele, jambo hili limekuwa chukizo mbele za Mungu wetu, nakuomba sana Moyo wako usijae kiburi wala ulimi wako usiwe mwepesi wa kunena, matendo yako mengi yatalipwa hapa Duniani, Mbinguni ni sehemu ya kukamilisha tu matukio yako ya hapa.
Magufuli tambua kwamba unyanyasaji unaotufanyia Mungu atakunyanyasa sawa sawa na kiasi cha kila chozi linalodondoka hapa.
Naendelea Kumuuliza Mungu juu ya Utawala huu, utawala wenye kiburi, majivuno, ubabe na kila aina kwa raia wake.
Natamani nione nchi iliyojaa Upendo, uvumilivu, Heshima, Ubinadamu, Haki, Utawala wa sheria, Uchumi imara na Utajiri wa nafsi, mali na Roho. Nchi ya kumcha Mungu.....n.k
Naomba sana Ujumbe huu ukufikie kwa muda uliopangwa na Mungu.
Hakuna sababu ya kuniita mchochezi, nimeysema yaliyoujaza moyo wangu, sitaki kuona naendelea kusononeka, natamani ningepata hata nafasi ya kukueleza haya lakini nimeona hata huku huwa unapitia sana, kama si wewe basi wasaidizi wako.
Ahsante
Niite ; GOODLUCK