Kwako Mwakyembe: Uwanja wa Ndege DIA Hauna ulinzi, Omba omba wavamia...

Mlaleo

JF-Expert Member
Oct 11, 2011
13,388
9,758
Takribani miaka miwili hivi tokea niache kuwaona askari polisi wakifanya ulinzi au patrol katika parking za uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere Dar Es Salaam Sasa hivi imekuwa n Hatari zaidi Jana tu tarehe 22/9/2012 saa tisa alasili nimeshuhudia Raia akilalamika kuwa Kaibiwa Nembo ya Gari lake aina ya BMW ya upande wa Mbele huk akilalamika na kushangaa kuwa hata Sensitive area kama uwanja wa Ndege kuna Wakora.. Nilistaajabu na kusogea kwenda kushuhudia wizi huo...

Mdau aliamua kwenda kuripoti kwa wahusika area ya Parking Japo wahusika walisikitika na mhusika mmoja akasikitika huku akilaumu Kutokuwepo kwa ulinzi wowote hapo uwanjani na akisema wamesharipoti sana kwa viongozi kuwa ulinzi unahitajika sana eneo hilo, basi kwa unyonge akaondoka huku akisema naenda kuwaita Polisi kwani wao ndio wahusika wa usalama hapo uwanjani...huku akilalama kuwa polisi wanakimbilia ndani ya uwanja na wanadeal na wageni waingiao tu huku nje wakiacha mtajuana wenyewe. Pamoja na jitihada zake kuwatafuta polisi waliopangwa kwenye hilo lindo kushindikana akajisogeza pembeni hadi walalamikaji wakachoka kusubiri na kuondoka zao huku wakilalamika sana...

Hili ni jambo la kusikitisha sana kwani mwezi wa saba walipandisha gharama za kupark gari hao nje ya uwanja kutoka tsh 500 hadi Tsh 1000 sioni sababu zozote za kuwafanya askari au uongozi kushindwa kjuweka ulinzi.. Bila kusahahu kuna Omba omba wanazunguka hapo kwenye Magari yanapo park na hao omba omba huwafuata abiria na wawasindikizaji na wageni kuwaomba chochote kitu nilikuwa na wageni kutoka Ne walisikitika sana kwa hali hiyo kwani ilaleta Bad image ya Tanzania...

Naomba Waziri akemee hili au auadabishe uongozi wa DIA kwani Umelala usingizi wa Pono...
 
Hii ni aibu kwa kweli, sijui Tanzania tunaweza nini maana hata eneo kama uwanja wa ndege ambalo ni muhimu sana kwa usalama wa nchi sasa limekuwa holela. Je sisi wananchi tunaweza kusema tupo salama? hivi sasa vibaka na vishoka ndio wenye nguvu.

Maeneo mengine muhimu nayo hakuna unafuu, tumeshuhudia hivi majuzi tu, wenzi wakishirikiana na polisi walikuwa katika harakati za kufanya wizi mkubwa sana, baada ya kushitukiwa asikari aliyefanikisha kutengua wizi huo ametekwa na wezi wanatishia bila kuwaachia waliokatwa na wao hawatamwachia askari wa bandari waliyemteka. Hapa ndipo tulipofikia, na bado tunaimba Tanzania nchi ya amani, huenda mimi uelewa wangu wa amani ni tofauti na viongozi wa Tanzania.
 
Inawezekana Polisi walishamsusia siku nyingi waziri husika pale alipotoa tangazo kuwa kunawatu wanataka kumuua so wamemsusia kila kitu
 
Sasa hivi hatuhitaji polisi kila mahali lazima tutumie ile dhana ya polisi jamii na ulinzi shirikishi kama wanavofanya Switzerland so tumeanzia uwanja wa ndege wa DIA tuone kama dhana hiyo itafanikiwa
 
Back
Top Bottom