Mmanyema
Member
- Nov 14, 2016
- 25
- 26
Barua kwako mpenzi wangu
Mpenzi wangu,
Nikupendaye kwa dhati kutoka moyoni
mwangu,
Nakusalimia salamu ya huba iliyoambatana na
busu motomoto.
Mpenzi wangu nianze kwa kukushukuru sana
kwa barua yako iliyojaa huba ambayo
nimeipokea jana mchana nikiwa kazini. Niseme
tu nimefurahi sana mpenzi wangu kupata
barua yako. Siku zote barua zako huwa tiba
mahabuba moyoni mwangu. Kila niusomapo
mwandiko wako wa kimahaba huwa napata
liwazo la haja moyoni mwangu. Maneno ya
kwenye barua yako ni dawa isiyo na kifani
ndani ya moyo wangu. Kila mara najikuta
moyo wangu unaongeza maradufu upendo juu
yako.
Mpenzi wangu, usishangae kuwa nimepata
barua jana lakini nimechelewa kukujibu hadi
leo ndiyo nimeshika kalamu na karatasi ili
nikuandikie ewe malaika wa moyo wangu.
Nilipoipata barua yako nilitafakari kwa muda
mrefu mno hadi kujikuta nikitokwa na
machozi. Hayakuwa machozi ya furaha kama
yale yanidondokayo kila wakati nisomapo
maneno matamu kutoka kwako ewe mwandani
wangu. Maneno ya kwenye barua yako
yamenichoma moyoni mwangu mithili ya
mkuki wenye ncha kali tena iliyoiva vilivyo
kwenye tanuru la moto. Mpenzi wangu,
niliyekuchagua mimi mwenyewe kutokana na
hisia kali na mapenzi mazito sana niliyonayo
moyoni mwangu juu yako, amini bado
nakupenda sana.
Mpenzi wangu, nikakiri kwa yakini kuwa
nilikuahidi toka miaka mingi sana kuwa pindi
nitakapojaaliwa kupata kazi nitakuoa.
Nayakumbuka maneno ya ahadi niliyokuwa
nikikupa kila mara tulipokuwa tukipata
kaupenyo ka kuwa pamoja. Ahadi yangu bado
ipo pale pale mpenzi wangu. Moyo wangu,
kwa dhati kabisa, bado una dhamira ya dhati
ya kukuoa mpenzi wangu nikupendaye kuliko
chochote humu duniani, kuliko hata
niipendavyo nafsi yangu. Bila wewe mpenzi
wangu, dunia hii ina faida gani kwangu?
Mpenzi, nimetokwa machozi kwa sababu ya
uzito wa jambo lenyewe. Kwenye barua yako
umeandika jinsi unavyokata tamaa kwani sasa
ni mwaka moja toka nianze kazi lakini
sijatimiza ahadi yangu ya kukuoa. Mpenzi
unaona kama nakupotezea muda na
unaniomba kama sina haja nawe nikupe nafasi
uolewe na mtu mwingine ambaye hata leo hii
yupo tayari kuleta posa kwa wazazi wako. Sijui
niyaelezeaje maumivu makali ninayoyasikia
ndani ya moyo wangu.
Mpenzi wangu, niseme tu ukweli. Ninakupenda
mno kuliko hata maana ya neno lenyewe
upendo. Ninatamani sana hata sekunde hii hii
niwe nimeoana nawe. Lakini, kama
nikwambiavyo siku zote, ugumu wa maisha
hapa Dar es Salaam hususani kwangu mie
mfanyakazi wa kima cha chini ndiyo
unaonifanya nikose uthubutu wa kukuoa ewe
mpenzi wangu niliyekupa moyo wangu wote,
haraka iwezekanavyo kama ambavyo
nimekuwa nikikuahidi mara nyingi sana.
Mpenzi wangu, moyoni mwangu inaniuma
sana maana maisha magumu ninayoyaishi
hapa Dar es Salaam kwa kweli yanatishia kwa
kiasi kikubwa sana ustawi na uhai wa penzi
letu.
Mpenzi wangu, nikwambie nini ili ufahamu
kwa kiasi gani akili na moyo wangu vyatamani
kwa dhati kabisa kuishi nawe milele yote kadri
Mwenyezi Mungu atakavyotujaalia siku za
kuishi humu duniani. Nikwambieje ili ufahamu
ni namna gani nalitamani pendo hili lidumu
humu duniani na baada ya hapo?
Mpenzi, maisha yangu mfanyakazi wa kima cha
chini ni magumu mno. Fikiria mpenzi wangu,
kamshahara kangu ambako ni kadogo mno,
kanapaswa kalipe kodi ya nyumba, umeme,
maji, matibabu, gharama za usafiri na
mengineyo chungumbovu. Mpenzi wangu
huwezi amini kuna wakati huwa nalazimika
kutembea kwa miguu kutoka kazini pale
Stesheni mjini hadi nilikopanga Mbagala
Kizuiani. Huwa inanigharimu masaa karibia
mawili nachapa tu mwendo tena wakati
mwingine mvua ikininyeeshea mwili mzima.
Sijakwambia tu mpenzi wangu, mara zingine
huwa nalazimika kushindia mlo mmoja ama
pengine nisile kabisa. We acha tu mpenzi
wangu.
Mpenzi, natamani ningekuwa na uwezo wa
kukufungulia moyo wangu uyaone yaliyo
ndani. Natamani mno tena kupita maelezo
kuoana nawe. Kinachonikwamisha mpenzi
wangu ni ugumu tu wa maisha ninaokabiliana
nao hapa mjini. Sikusudii kukuoa ili uteseke.
Sikusudii kukuoa ili nikushindishe njaa.
Siyakusudii hayo.
Mpenzi wangu, sikusudii kuuweka uhusiano
wetu rehani. Mpenzi sina namna niwezayo
kuibadili hali halisi kwa sasa zaidi ya
kulazimika kufanya kazi kwa bidii ili pengine
bosi wangu anione anipandishe cheo ama
kunipa nafasi ya kwenda kujiendeleza kielimu.
Lakini tatizo kazini kwetu kumejaa majungu
mno kiasi kwamba uchapakazi wangu
unanifanya nionekane kimbelembele. Kila mtu
ananiona nina kiherehere hadi nalazimika
kuwa mpole na goigoi kama wafanyakazi
wengine. Kwa mtindo huu sijui ni lini
nitafanikiwa kimaisha.
Mpenzi, kweli kabisa mbele ya Mwenyezi
Mungu, sitamani wala siombi uniache na
kuolewa na mwingine kwa sababu tu ya hali
yangu duni. Machozi yananitoka mno
kuyaandika maneno haya. Ninakuomba mpenzi
wangu univumilie walau kwa mwaka moja
mwingine pengine serikali itatufikiria na
kuamua kuboresha hali zetu. Chonde chonde
mpenzi wangu.
Mpenzi wangu, najaribu kukwepa kuufikiria
mtihani mkubwa unaokukabili kwa sasa.
Mapenzi ya kweli ama maisha bora. Najaribu
tu kupambana na wivu moyoni mwangu.
Najaribu kutamani kuvivaa viatu vyako na
kuchagua mapenzi ya kweli. Lakini sipungukiwi
imani.
Mpenzi wangu, najua nimekuchosha kwa barua
ndefu sana ambayo hata hivyo imeshindwa
kujibu swali lako la nitakuoa lini. Ninatumai
maelezo yangu pamoja na kutojibu moja kwa
moja swali lako, angalau yametoa mwelekeo
wa jibu.
Mpenzi wangu, natamani kusema mengi sana
zaidi ya haya. Najua hata siku moja dau tupu
haliendi joshi na maneno matupu hayajengi
nyumba. Ninaloweza kukwambia ni kuwa
ninakupenda mno, daima ninakuwaza wewe
kwa kuwa umetamalaki moyoni mwangu.
Wewe ndilo pambo la moyo wangu. Kwa huba
na mahaba yajazayo vibaba na vibaba, penzi
langu kwako limeshiba.
Nikupendaye daima,