Kwako mkurugenzi mkuu wa NIDA

Kwako mkurugenzi mkuu wa NIDA

Hawa NIDA ni janga la taifa, kwasababu kila unapoenda unadaiwa kitambulisho cha taifa au nakala yake au namba yake, lakini NIDA wanashindwa kutoa hata namba za vitambulisho tuu, na ukweli hawasemi wanasema tuu njoo wiki ijayo kila siku
Hivi niwaulize huyu mtu anayeitwa NIDA hana dini.Mbona karibu Watanzania karibu millioni 30 wanalalamika tuuu, kila kukicha,mara utamsikia huyu anasema nimeshindwa kufungua akaunti nida hajanipa kitambulisho,nimeshindwa kupata leseni, huyu nida hajanipa namba,mara nimeshindwa kuomba mkopo nida janipa kitambulisho n.k.Naomba niwashauri,huyu NIDA si mmoja sijui ni mwanamke au mwanaume,si unajua umoja ni nguvu.Wooote mnaomdai huyu mtu, nendeni mahakamani mfungulieni mashtaka ya usumbufu na kurudisha maendeleo ya wenzake nyuma kama sio kuyasimamisha kabisa.Au mfuateni mkamateni piga,piga,piga mwachieni na vitambulisho vyenu.Sasa ukienda uhamiaji Leta Nida,Polisi leta Nida,Bodi ya mikopo,leta Nida.Wewe Nida hawa watu wote wakikulaani utakufa.Na ili usife wape wanchokudai.Tena wengine wamesema uliwaambia wakulipe 200SHILINGI wakutumie meseji utawapa sijui ni namba sijui ni kitambulisho.Weeengi wakakutumia ukala zote mpaka leo wanakusubiri kwani uliwaambia utawajibu,siku nyingi zimepita.Wee NIDA unatakaje.N,gombe wanapiga kelele ngoja niwatupie majani nitarudi ili niendelee kuzungumzana wewe NIDA.
 
Nadhani hawa watu wa NIDA kuna kitu kinawasumbua na hawako tayari kuwaeleza Watanzania ukweli,na kwa ukimya huo tutawazidi kuwasuta sana.
Yaani suala la mtu kupata namba ya kitambulisho tu limekuwa gumu sana,utadhania haya mambo tunayafanyia nchi nyingine. Lkn wanapofanya hivyo,wajue kuna taasisi hasa za binafsi km vyuo vya udereva vinaathirika sana. Inaeleweka mtu haruhusiwi kuanza practical ya mafunzo ya udereva unless amepata leaner licence. Na ili apate hiyo leaner licence ni "lazima" awe na aidha kitambulisho chenyewe au namba yake. Hapo akifika NIDA iwe ni danadana....sasa hivi vyuo vitaendeshaje kazi zake km si kuumizana taratibu??
Binafs pia naomba tamko la Mkurugenzi wa NIDA
Kwa ninavyo elewa mimi namba ya kitambulisho inapatikana kwa wale walioanza ilo zoezi namaanisha kwa wale ambao wameshajaza form,ikagongwa muhuri wa serikali za mitaa ukaambatanisha na vyote vinavyoitajika then ukafika ofisini kwao ukalata usumbufu unaostahili baada ya hapo ukaitwa kwa namba ya kukusanya form ukaingia ndani,ukakutana na mtu wa migration ukamaliza taratibu zote,ukaenda sehemu ya kupiga picha,ukasaini then watakokuambia taarifa zako zimeshapokelewa ngoja baada ya mwezi mmoja kwa mfano!!Taarifa zako zikishatumwa head office na hatua za kutengeneza kitambulisho chako zikaanza hapo ndipo unaweza kupata namba na sio ukiingia tu website hapo tayari wanakupa namba.UNAPOPEWA NAMBA MAANA YAKE KITAMBULISHO CHAKO KIPO KIPO JIKONI BADO KUPAKULIWA TU NA LABDA KUTOKANA NA WINGI WA WATU WENYE MAOMBI KAMA YAKO NA MARA NYINGI MTANDAO UNAKUWA CHINI.!!
 
Kwa hiyo wewe ndo P.R.O wa NIDA

Kifupi NIDA kazi ilishawashinda.

Kuna watu wanafuatilia vitambulisho toka mwaka 2015 hadi leo hakuna kitu.
 
Mimi ni Mtanzania na ninatakiwa kupata pasi mpya ya kusafiri. Moja ya sharti ya kupata pasi hii ni kuwa na kitambulisho cha Taifa au kuwa na nakala ya kitambulisho baada ya kuwa na namba ya kitambulisho cha Taifa.

Tumeelezwa kuwa nakala ya kitambulisho (kama huna kitambulisho) unaweza kuprint kutoka kwenye website yenu.

Nimefuata taratibu zote ili nipate nakala ya kitambulisho lakini website yenu aidha ina matatizo au imesitishwa kutoa nakala hizi.

Ninaomba msaaada au taarifa itolewe kwa wananchi kwa wale ambao hawana vitambulisho vya Kitaifa ila wanazo namba ni utaratibu gani wafuate ili wapate nakala ya vitambulisho vya Kitaifa ili hatimaye waweze kukidhi sharti hili la kupata pasi ya kusafiria. Kwa kweli tunateseka sana.
Kama wamekupa namba nenda internet cafe wape hiyo number chap wanakuprintia ID wanaweka na lamination.
 
Mimi ni Mtanzania na ninatakiwa kupata pasi mpya ya kusafiri. Moja ya sharti ya kupata pasi hii ni kuwa na kitambulisho cha Taifa au kuwa na nakala ya kitambulisho baada ya kuwa na namba ya kitambulisho cha Taifa.

Tumeelezwa kuwa nakala ya kitambulisho (kama huna kitambulisho) unaweza kuprint kutoka kwenye website yenu.

Nimefuata taratibu zote ili nipate nakala ya kitambulisho lakini website yenu aidha ina matatizo au imesitishwa kutoa nakala hizi.

Ninaomba msaaada au taarifa itolewe kwa wananchi kwa wale ambao hawana vitambulisho vya Kitaifa ila wanazo namba ni utaratibu gani wafuate ili wapate nakala ya vitambulisho vya Kitaifa ili hatimaye waweze kukidhi sharti hili la kupata pasi ya kusafiria. Kwa kweli tunateseka sana.
Ebwana vp ulifanikiwa? namimi nataka ni print hiyo copy haifunguki lakin sehem zote nikijaribu za matangazo yao zinakubali.
 
Hawa wakurugenzi wa NIDA inatakiwa watumbuliwe wote binafsi sioni saba mtu ameshamaliza process zote na picha ameshapiga anambiwa akae siku 60 ndio akachukue kitambulisho
 
Back
Top Bottom