Kwako Mh. Ndalichako, Joyce.

Kwako Mh. Ndalichako, Joyce.

club6

Senior Member
Joined
Apr 11, 2014
Posts
157
Reaction score
61
Naitwa Shafir Zubail, mhitimu wa kidato cha nne 2010. Shule nimesoma ya serikali ya Kaigara Shule ya Sekondari, ila kulingana na hali ngumu ya kimaisha ya hapa nyumbani sikuweza kufaulu kuwndelea na ngazi ya juu.

Nimeteseka sana mtaani huku nikichanja na kuuza kuni mtaani, ile biashara haikunilipa kulingana na uduni wa familia yangu kwani licha ya kuwa mdogo, nilipaswa kutafuta chakula kwa ajili ya familia yangu kwani Baba yangu aliumwa sana kipindi hiko, kuanzia 2009 mpaka mwaka 2014, Mei ndipo alitoka hospitalini.

Baada ya kusota mtaani kwa muda mrefu bila ya maganikio kimaisha, February 2014 niliamua kuanza kusoma mtaani ili niweze kurudia mtihani wa kidato cha nne kwani nisingeweza kurudi shule maana tayari muda ushaniacha. Nimesoma kwa shida sana huku nikitafuta ada ya twisheni niliyokuwa nasoma. Mwezi Oktoba, 4, 2014 kaka zangu watatu walipata ajali na kupoteza maisha.

Hapohapo Baba yangu akapata stroke na kurudi upya kwenye maradhi. Sikuwa na uhakika na mwaka ule kulingana na matatizo ya nyumbani na ilhali tarehe 03/11 ndo tarehe iliyokuwa ya kuanza kufanya mtihani huo. Mwaka 2015 14, February matokeo yalitoka na nikafanikiwa kupata alama za kuniwezesha kufanya mtihani wa kidato cha sita.

Katika hali ya matatizo mengi huku nikitafuta ada ya twisheni, mwezi wa tano mwaka huu nikafanya mtihani sikubahatika kupata alama za juu ila nikabahatika kupata pointi zinazohitajika kwenda chuo kikuu. Nilijaza fomu za kuomba mkopo bila kukosea lolote kwani kwenye list ya watu waliokosea 10,027 jina langu halikuwepo(nilijihakikishia).

Wakati wa kuomba vyuo, nakumbuka niliomba tarehe 27/07. Nilibahatika kupata chuo cha Archbishop James University College (AJUCO), first batch jina langu ni la 877, na kwenye list ya TCU iliyotoka yenye majina 63,773 ya wanafunzi waliofahiliwa mwaka 2016/17 jina langu ni la 181.

Ada ya kulipa Archbishop James University College (AJUCO) ni kubwa sana kwangu (Ada Tsh 1,260,000/=, Administration fees Tsh 285,000/=, Hostel Tsh 400,000/=) kwani kulingana na maradhi aliyoyapata Baba, eneo kubwa la shamba ameshaliuza. Hivyo ameuza sehemu aliyokuwa amenipa ili nilipe mahitaji ya kwanza. Lakini pesa haitoshi hivyo ikanibidi niombe transfer UDOM.

Lakini cha kushangaza ni kwamba sijapata mkopo na maisha yangu ni magumu sana huku mtaani maana tayari nilikuwa nimeona nuru mbele yangu lakini nasikitika kwa masikitiko makubwa. Tafadhali, nisaidie mimi maana bila mkopo uwezo wa kujisomesha sitaupata kwani sitapata ada kwa ajili ya semester ya pili ya mwaka wa kwanza.

Samahani, Kiswahili na maelezo niliyotoa yamejikita kwenye lugha mama.

Nashukuru sana kwa kunielewa.
 
pole sana ndugu yangu....wengi wamekumbwa na adha kama iliyokukuta usiache kumuomba Mungu wako kwani naamini magumu unayopitia ni chanzo kikubwa cha mafanikio yako...usikate tamaa ndugu yangu...Mungu wetu ni muaminifu hawezi kukuacha ukataabika
 
Mama Ndalichako, Watanzania wengi wanahitaji msaada. Huu ni mfano wa mmoja wa waliojitolea kukueleza yanayowasibu. Hii dhana ya ukopeshaji na vigezo vinavyotumika kupata mikopo bado haijaeleweka miongoni mwa Watanzania. Tafadhali wasaidie hawa vijana ili waweze kujikomboa kielimu. Tusije tengeneza Taifa la mambumbu.
 
Duh pole sana mkuu naamin wahusika wamekusikia na watalishughulikia bt kuwa mvumilivu mdogo wang nae alinyimwa mkopo kwa kigezo cha P bt juzi usiku jina lake lilionekana limepewa mkopo so kuwa mvumilivu inshalah utafanikiwa
 
Pole sana mkuu, ila usikate tamaa mungu Yuko pamoja nawe, nahisi wahusika watakuwa wamekusikia
 
kama mwenyewe uko bungeni analijua hilo kwel ni tatizo kwa nini asiji udhuru huyu mama jamani maana hii wizara wana ichezea makida sana ona sasa vijana wana vo haha hi janga kubwa sana
 
Kama upo Dodoma nenda bungeni utasaidiwa jitokeze kwenye halaiki kaeleze Shida yako bungeni na nyaraka zote ulizoomba mkopo nenda zako

Nilijaza fomu, majina yametoka ya awali. Sisi tulioomba baadae majina hayajatoka. Niko mtaani kwa rafiki yangu, Morogoro maana Dodoma sina rafiki wala ndugu. Nikisema nitoe nauli tena kurudi nyumbani (Bukoba) sitapata ya kurudia
 
Nenda bodi ya mikopo ukawaeleze kwani kuna mshkaji wangu alfanya hivyo juzi wakamwelewa vizuri tu na tayari kashapata mkopo.Fanya hivyo nenda katika ofisi zao.
 
Nenda bodi ya mikopo ukawaeleze kwani kuna mshkaji wangu alfanya hivyo juzi wakamwelewa vizuri tu na tayari kashapata mkopo.Fanya hivyo nenda katika ofisi zao.

Ahsante mkuu, na sasa nauza simu ili kuokoa kimoja... Nashukuru sana kwa mchango wako
 
Pole sana kakaangu.
Uyu mama mungu anamuona tumuachie mungu.
Kiukweli wametunyanyasa.
 
Shule uwa inaanzwa alafu mwenye kuimaliza ni Mungu,haya mengine yatajisolve piga hatua kama wenzio wanavyokwambia ndugu,
 
Kama inawezekana nenda bodi ya mikopo makao makuu yao yapo mwenge dsm uwaeleze ukweli ulioambatana na nyaraka km zile za kuhama chuo na kuelekea udom nadhani watakuelewa, inshallah Mungu akutangulie na uweze kufanikisha ili badae usome kwa juhudi na maarifa na uweze kuikomboa familia yenu
 
Kama inawezekana nenda bodi ya mikopo makao makuu yao yapo mwenge dsm uwaeleze ukweli ulioambatana na nyaraka km zile za kuhama chuo na kuelekea udom nadhani watakuelewa, inshallah Mungu akutangulie na uweze kufanikisha ili badae usome kwa juhudi na maarifa na uweze kuikomboa familia yenu
Shukran sana mkuu. Mawazo yako nitatafanyia kazi
 
Back
Top Bottom