Kwako Mh. Godbless Lema......

Kwako Mh. Godbless Lema......

PapoKwaPapo

JF-Expert Member
Joined
Jun 5, 2008
Posts
380
Reaction score
45
Heshima kwako mheshimiwa.
Kwanza kabisa natanguliza shukrani zangu za dhati kwako, kwa hamasa kubwa uliyoileta kwenye siasa za Tanzania hasa kwa vijana. Wewe ni kiongozi shupavu, ninaposema shupavu namaanisha shupavu kweli kweli. Huogopi kusema kile unachokimini popote pale na ndio viongozi wa namna hii tunaowahitaji hapa kwetu Tanzania.

Lengo hasa la waraka huu ni kukusifu na kukutia moyo kama mbunge mteule wa Arusha mjini na waziri kivuli wa mabo ya ndani. Kilicho nisukuma mpaka nikakuandikia waraka huu leo ni baada ya kusikia ulikuwa Tarime. Kuna watanzania wenzetu wameuwa huko kama waziri kivuli wa mambo ya ndani ukafanya lile linalotaki yaani kwenda kujua nini hasa kilicho tokea.

Kilichonishangaza mimi ni kwamba hata waziri mwenye dhamana ya mabo ya ndani hakujitokeza kutaka kujua ni nini kilichotokea huko. Hili kwako na Chadema ni goli la ushindi.

Nakuomba sana sana uwakumbushe mawaziri wengine vivuli wa Chadema watende kama ulivyo tenda, tunata kuona kwa mfano waziri kivuli wa afya anatembelea hospitali zetu za rufaa na kujionea jinsi zinavyofanya kazi na kuwa changamoto. Pia waziri kivuli wa ajira na vijana akitupa changamoto zake jinsi gani vijana watawezeshwa. Kila siku ninapoulizwa swahi hili huwa najibiwa nikasome ilani ya Chadema, ukweli ni kwamba si wote tuliopata hiyo bahati ya kusoma ilani yenu.

Huu ni muda wa kuonyesha chama chenu kipo tayari kushika madaraka. Godbless Lema waziri kivuli wa mambo ya ndani ameanza na wewe anza sasa.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Chadema.
Natanguliza shukrani zangu za dhati.
 
Hongera sana Mh. Godbless Jonathan Lema Mbunge wangu, nakumbuka wakati tuko katika harakati za ukombozi wa jimbo letu kutoka mikononi mwa CCM, uliwahi kutuambia kwamba wewe utakuwa mbele yetu, na sisi tuwe nyuma yako tusikuanguashe. kwa hili tumeshuhudia kweli uko mbele yetu na sisi tuko nyuma yako.

katika nchi hii sijawahi kuona kiongozi anapigwa na polisi kwa ajili ya kutetea maslahi ya wananchi wake, wewe umekuwa kioo, ulipigwa na polisi, ukawekwa ndani, ukadhihakiwa sana, lakini hukukata tamaa.
Mh. Lema wewe ni mzalendo wa kweli wa nchi hii, tunakutakia mema siku zote, tunakuombea mungu aendelee kukupa ujasiri ututetea watanzania wote tunakuhitaji.

Mungu ibariki Tanzania
Mungu ibariki Chadema
Mungu mbariki Godbless Lema.
 
Mh lema ni kiongoz shupavu asieogopa kitu chochote kutetea maslah ya wananchi wake na taifa kwa ujumla,hongera sn lema kaza buti safari bado ni ndefu.
 
mungu mbariki mja wako Godbless Lema kama jina laki linavyojieleza linyewe.kaka pambana watanzania wengi wako nyuma yako wanakuangalia wewe kama kiongozi wako usikate tamaa maana watanzania wengi ambao wanaelekea kukombolewa na wewe nao watakata tamaa nakutakia kila la heri upendo na neema zake mwenyezi Mungu ziwe juu yako.akupigania wanaokupinga waanguke na akujalie hekima na busara na akuondolee tamaa .

freedom is coming tomorrow
 
Na mimi nikupe pongezi zangu za dhati kamanda Lema, ulidhalilishwa ila hukurudi nyuma kwakuwa ulijua ni kipindi cha mpito kweli kimepita sasa twayaona yale uliyokuwa unataka yapiganiwe umeanza kuyatekeleza kwa vitendo unastahili pongezi kamanda,taifa hili limepata kiongozi imara atakaye kumbukwa milele tunakuomba uwalee vijana kama wewe vizuri ili waje kukuongezea nguvu siku za mbeleni,kama unavyo mkuza Nasari joshua na Kilewo tafuta wengine ili wawe wengi mkuu naomba watakao soma coment hii wakufikishie ujumbe wangu!! Tupo nyuma yako kama ulivyotuambia utakuwa mbele sisi nyuma wewe ni waziri tosha huyo waziri kamili ni waziri wa viongozi, mungu akubariki sana mungu aibariki Tanzania, mungu aibariki chadema
 
Nitamfikishia Mh. Lema salamu hizi leoleo na nitawarudia kuwaeleza atakachosema. Daima tutasonga mbele pamoja, tutakomaa pamoja , daima hatutorudi nyuma.
 
Aisee Lema charlii wangu, ujue umenifurahisha sana ulipowatembelea hawa macharlii wa Tarime, ukirudi Arusha kisusio kinakusubiri. Unajua serikali yetu imewafanya wananchi wake kama mbusi, yani wamesubiri wafe ili wakawasike, aisee waambie hao macharlii wa huko wasikubali kabisa. kasa buti saidi na saidi Lema.
 
Angalia wasije wakakutegeshea ajali kama kawida yao maana laana ya viongozi wanaojitolea ipasavyo kwa wananchi ilianzia kwa marehemu Edward Moringe Sokoine
 
mh.Lema kwa umri wangu sijaona mbunge shupavu kama wewe,mbunge alipigwa na polisi,nashukuru sana kwa mambo unayotuonesha waTanzania,tuko nawe daima pigania haki,wewe ni mpunge imara,shupavu,jasiri,mpigania HAKi kwa vitendo.mh.Lema songa mbele pigana ndugu,nakuombea wasijekukua hawa jamaa hasa kwa sayansi ya gizani.mungu akubariki tena na tena.usichoke kwani ukichoka wewe tutabaki bila mpiganaji.ubarikiwe sana.
 
nakupongeza bwana lema hasa kwa kuja hapa kwetu tarime na wewe ni shahidi umeona ukaribu wetu kwako na zaidi sisi atuwezi kukupa chochote lakini tunakuombea uzima na ulinzi kutoka kwa muumba wetu na azidi kukupa hekima na busara za kutuongoza watanzania tuko nyuma yako daima pambana kwa ajili ya kuokoa taifa letu kwa vizazi vyetu vya mbeleni, Mungu mbariki lema Mungu ibariki tanzania
 
mh LEMA tupo nyuma yako!! kaza buti vijana tutaitikia pale utakapotuita tutatoa msaada ktk kila ngazi ya mapambano kwa kweli chadema mmeniletea raha ktk maisha haya maguuuuumu saaaana. chadema is LAGER THAN LIFE ITSELF!!!!
 
Lema unakubarika. kama jina lako lilivyo toa baraka kwa wote usiogope cheo. nakumbuka maneno yako kuwa huna adress ya uoga. pamoja sana
 
always God will bless Lema .watanzania wote tunakushukuru sana hakika wewe ni taa ya ukombozi
 
always God will bless Lema .watanzania wote tunakushukuru sana hakika wewe ni taa ya ukombozi

Akiacha kuvuta lile jani akili yake inaweza kurudi vizuri vinginevyo anakipeleka cdm kaburini
 
Aisee ma chalii, mm nategemea kupata mtoto, akiwa wa kiume tu ntampa jina la Godbles mana mh. hyu ni role model wngu. Mambo yke ya ukweli acha akina Kagasheki anayeropoka tu kaa ajaenda shule,
 
Back
Top Bottom