Kwako mama, msichana au mwanamke, pata ushauri kuhusu uzazi

mis lemich

JF-Expert Member
Jan 25, 2017
207
176
Habari zenu wanajamiii

Napenda kukumbusha kwamba Tanzania inapambana sana na vita dhidi ya vifo vya mama na mtoto kabla na baada ya kujifungua.

Lakini suala hili bila ushirikiano wako wewe mwanamke au msichana uliye mjauzito bado suala hili litakua ni gumu.

Kwanza unapokua karibu na mwanamke mjamzito ni muhimu kumkumbusha kwamba ni muhimu sana kuwahi hospitalini kwa ajili matazamio ya maendeleo yake pale anakaribia kujifungua au kuona dalili.

Pili kuzingatia mahudhurio mazuri ya kliniki ili kuweza kujieleza na kupata ufafanuzi mzuri ya maendeleo yake ya ujauzito.

Tatu kuwahi kuwa karibu na kituo cha Afya endapo unaishi mbali.

Zaidi kuzingatia haya ambayo bado yamekuwa changamoto. TAFADHALI EPUKA KUUSUBIRI UCHUNGU AU MAUMIVU YA LEBA KUZIDI UKIWA NYUMBANI AU KUTUMIA DAWA ZA KUONGEZA UCHUNGU.

ZINAWEZA KULETA MADHARA KAMA KUPASUKA KIZAZI KWA UCHUNGU MKALI.
 
Back
Top Bottom