Kwanza kabisa, inabidi kujiuliza, hivi ni kwa nini tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, matukio ya aina hii yalikuwa nadra sana kutokea? maana tungetarajia miaka ile kwamba vyama vilikuwa havina uelewa wa taratibu za uchaguzi. lakini kinyume chake, miaka 26 baadaye ndiyo tunaanza kushuhudia matukio ya namna hii. ni wazi kwamba kuna tatizo kubwa hapa.
unaonesha kura ulianza kupiga 2015
Mapingamizi,mihuri sahihi na kuchelewa kurudisha fomu na kutoa vizingizo ni ugonjwa wa wapinzani
mwaka 2000,mgombea wa chadema alichelewa kurudisha fomu akasingizia kawekewa trekta!
Njelu kasaka,aliwekewa pingamizi kwa kuwa ana muhuri wa katibu wa jimbo chadema,badala wa wilaya,fasta siku hiyo hiyo ya mwisho akajiunga na cuf huko Lupa,akaishia kuchelewa kurudisha fomu
2018,chadema wanamleta Salum mwalimu kinondoni,kaulizwa unaishi mtaa gani anajiuma uma tu,ni busara ya tume tu,lilimrudisha kwenye kinyang'anyiro,akini hakujipigia kura
2018 chadema wanatuma wagombea udiwani wawili wawili huko mbeya,matokeo yake wote wamepoteza
2015,iliwachukua chadema dakika tisini kumsimamisha mgombea ambae hajui hata ubeti mmoja wa katiba,na walimtukana sana mpaka siku ya uteuzi wake
Mifano ni mingi,lakini kwa hiyo michache utagundua Tanzania hatuna wapinzani,tuna wapiga kelele tu
Wakati ccm wanateua mgombea na kurudisha fomu,kina mashinji walikua bize mitandaoni kuishambulia dreamliner kuwa imekufa mwanza