Mindi
JF-Expert Member
- Apr 5, 2008
- 3,523
- 4,998
Leo asubuhi nilikuwa nasikiliza kipindi cha KUPAKA RANGI cha Magic FM, ambapo watangazaji walikuwa wakijadili suala la figisu iliyotokea katika uchaguzi mdogo Jimbo la Korogwe, ambapo tunaambiwa kwamba mgombea wa CCM ametangazwa mshindi kwa kupita bila kupingwa. baada ya kutolewa maelezo ya awali, nilimsikia Kibwana Dachi akisema kwamba anawashangaa CHADEMA, kwamba inakuwaje hawarekodi haya matukio, ili kuwe na ushahidi wa wazi kabisa. yaani kwa mfano katika tukio la Korogwe, wamrekodi yule msimamizi aliyesema kwamba hapokei fomu kwa maagizo maalum, mpaka ifikapo saa 10.00 jioni. na wapige picha jinsi walivyokuwa pale ofisini wakisubiri kurejesha fomu.
Suala ambalo nilidhani Kibwana Dachi ambaye anasifika sana kuwa ni mtangazaji mwenye taarifa nyingi sana, mwenye kumbukumbu nzuri, na mchambuzi mahiri, angeweza tu kusema mawili matatu kuhusu sakata hili, ambayo yangetoa picha kamili zaidi, kuliko kuwalaumu CHADEMA:
1) Kwanza kabisa, inabidi kujiuliza, hivi ni kwa nini tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, matukio ya aina hii yalikuwa nadra sana kutokea? maana tungetarajia miaka ile kwamba vyama vilikuwa havina uelewa wa taratibu za uchaguzi. lakini kinyume chake, miaka 26 baadaye ndiyo tunaanza kushuhudia matukio ya namna hii. ni wazi kwamba kuna tatizo kubwa hapa. Ama CHADEMA wamekuwa wendawazimu kabisaaa, ama kuna figisu inafanyika makusudi.
2)Serikali hii ya Awamu ya Tano haiheshimu wala kuogopa ushahidi, wala haioni aibu kufanya mambo hadharani. kwa mfano, wakati wa bomoabomoa ya Kimara, kuna wananchi walikwenda mahakamani, wakapata STOP ORDER kwamba wasivunjiwe nyumba zao. tulishuhudia tukio la kushangaza sana, ambapo wale ambao walibandika hizo STOP ORDER kwenye nyumba zao ndio walivunjiwa kwa ukatili zaidi. na kwa kifupi hakuna aliyepona kwa kuegemea amri ya mahakama. sasa wananchi walifanya nini baada ya kuona jambo hilo linatendeka waziwazi?
3) Joshua Nassari alirekodi video nyingi tu kama ushahidi kwamba wanao"guswa" na utendaji wa JPM, wanahongwa. ushahidi huo aliuanika katika mitandao kabla ya kuupeleka TAKUKURU. lakini Rais Magufuli alipompandisha cheo Mnyeti kuwa Mkuu wa Mkoa, TAKUKURU wakaachana na upelelezi wa tukio hilo kwa sababu za wazi kabisa kwamba Bosi hana mpango. kwa hiyo MKUU wa TAKUKURU angehatarisha cheo chake kama angeendelea na upelelezi dhidi ya "mchapakazi" huyu. sasa, ushahidi ulianikwa. wananchi walifanya nini?
4) Kumekuwa na matukio mengine mengi tu kama yale ya uchaguzi wa Kinondoni ambayo yalipelekea kuuwawa kwa mwanafunzi wa NIT. lakini hakuna ambacho kimefanyika na wengi sasa wamesahau.
Sasa swali langu kwa KIBWANA DACHI, anaamini kwamba ushahidi wa video wa matukio hayo kama ya KOROGWE, utasaidi kuifanya serikali iachane na mbinu hizi chafu dhidi ya upinzani?