Kwako Katibu Mkuu wa CCM

Kwako Katibu Mkuu wa CCM

Johnson Alex Otieno

Senior Member
Joined
Mar 14, 2013
Posts
176
Reaction score
61
Naomba kuchukua fursa hii kukuandikia katibu wangu juu ya mambo yanayoendelea kujitokeza kwenye kura za maoni za kuwachagua wawakilishi wetu katika nafasi mbalimbali za serikali ya mtaa hapa kata ya makutupora mkoani dodoma.
Kata ya makutupora imefanya kura za maoni kwa mitaa minne huku mitaa mingine ikishindwa kuendelea na mchakato wa kura za maoni.

Moja kati ya sababu zilizopelekea kutofanyika kwa zoezi hili ni viongozi wa CCM ngazi ya kata kuwa na wagombea wao mifukoni na kutokuzingatia maoni ya wananchi,mfano katibu wa chama kuwa na mgombea wake kwenye mtaa wa mji mpya,weyula na mtaa sekondari.Wakati huo huo mlezi wa chama (Diwani) nae ana wagombea wake kwenye mitaa tajwa.Mimi na wananchi wenzangu tunasikitishwa na tabia hii ya viongozi wetu kubeba baadhi ya watu na kupelekea kuharibu zoezi zima la kupata wawakilishi wa chama katika ngazi mbalimbali.

Aidha tunakerwa na tabia ya katibu mkuu kata ya kututisha kutufuta uanachama na kukupigia simu moja kwa moja kueleza mambo ambayo angeweza kushirikisha wananchi na Kuyatatua.

Tunaomba kata ya makutupora itazamwe kwa jicho la tatu kwani kumekuwa na tabia ya viongozi wa chama kuwachagulia wananchi viongozi hali inayoashiria kupanga safu za kupata madaraka katika chaguzi zijazo za mwaka 2020.

Aidha napenda kukujulisha kwamba kuna msuguano mkubwa kati ya Katibu mkuu kata na diwani wa kata juu ya nani awe mjumbe,mwenyekiti wa mtaa na nafasi zingine.
Tunaomba tusaidie kuondoa mkanganyiko huu maana unaashiria chama kuwa mikononi mwa watu wachache na wanaotuendesha kwa utashi wao si katiba wala kanuni za chama,jambo hili linapelekea chama kukosa wawakilishi wenye nguvu za kuleta maendeleo kwenye kata yetu ya makutupora.

Natambua wajumbe kutoka wilayani walifika hapa kujaribu kutatua kero zetu lakini hakuna walilofanya zaidi ya kula na kunywa katika moja ya bar zilizopo hapa.

Tunaomba wajumbe wako watumwe kutazama changamoto zetu na ikibidi zoezi zima lianze upya kwa maslahi ya wengi.
NB.Tunaomba mali za chama zihakiKiwe tena ili kuondoa ufisadi na matumizi mabaya ya mali za chama.
Hili ni kutokana na kukosekana kwa taarifa ya mapato na matumizi ya chama tangu uongozi mpya uingie madarakani.Naona kuna harufu ya matumizi mabaya ya mali za chama.
 
hii kazi ya uwenyekiti wa serikali za mtaa hauna mshahara lakini wagombea wanataka kuuwana kuna nini huko
 
Back
Top Bottom