Abdul Nondo
JF-Expert Member
- Oct 28, 2016
- 515
- 2,875
Kwanza napenda kukupongeza sana,kwa jitihada na moyo wako wa kusaidia jamii yetu.Umekuwa mfano bora kabisa katika jamii yetu na kwetu vijana.
Tuliona ulijitoa kuchangisha milioni 5 ,kumsaidia Mh.Rais kulipa deni la yule mama yetu aliyefiwa na mama yake Muhimbili .Na hakika leo tumeona umekabidhi fedha hizo hospital ya Muhimbili ,hongera sana kaka yetu.
Ila ,Mimi napata kukufananisha na kijana mmoja mwenye huruma sana anaitwa *Kalukalanga* , Siku moja Kalukalanga alipita msituni akakuta nyumba moja ikiwa imejitenga, alivyopita njiani karibu na nyumba ile akasikia sauti ya wamama wakilia kwa uchungu waokolewe kutoka katika chumba kimoja ,chenye giza kidogo.
Kalukalanga akachungulia dirishani ukamuona mmoja wa mama akilia kwa sauti akihitaji maji ya kunywa, huku mama wengine wakiwa wamelegea sauti hazitoki kwa unyonge .
Kalukalanga alivyojaliwa huruma ,akakimbia haraka kutafuta maji , akiomba huku na kule kwa rafiki zake na majirani zake ili chupa lijae akampe maji mama yule .
Alijaliwa kuyapata akampelekea mama yule dirishani ,yule mama akanywa .Kalukalanga akaondoka huku akisema moyoni nimemsaidia mama yule.
Kalukalanga hakujali kuwa mama yule hayupo pekeake katika kile chumba, bali wapo wengi katika chumba kile ,ila sababu walikuwa wamedhoofu hawakuweza kutoa sauti zao ila sauti ya mama yule mmoja ilipaswa kubebwa na Kalukalanga kwa uzito zaidi kama sauti wakilishi ya wamama wote mule ndani.
Pia Kalukalanga alijua amempa msaada mama yule ,ila Kalukalanga hakuwaza nani atakaye mpa tena mama yule maji au chakula hapo baadaye ikiwa sehemu ile hakuna wapitanjia wengi.
Msaada mkubwa Kalukalanga angeufanya kupitia sauti ya mama yule mmoja,angetafuta namna ya kuwaokoa wale wa mama kutoka katika chumba chenye giza ,mateso na unyong'onyefu kuliko kumpa maji tuu na kuondoka kwa kufikiri ametoa msaada wa kutosha.Ndio ni msaada ila sio msaada wa kutatua tena kiu chake hapo baadaye ,ikiwa maji yenyewe alikunywa yote sababu ya uchache.
Watanzania ni maskini , mikakati imara ya kusaidia upatikanaji rahisi wa huduma ya afya kwa mfumo wa pamoja ili kusaidia wengi zaidi.Kuliko mmoja mmoja ! Yes ni vyema mama alipaswa kusaidiwa ila tunapaswa kwenda mbali zaidi ,msaada alioupata ,anaweza uomba tena kama akipata shida kama hiyo siku zijazo .
Kipato cha mtanzania kwa mwaka ni Mil.2.4
Pia ndicho kipato cha yule mama hospital ,ambapo kama hana ajira rasmi anapaswa awe na mil,1.5 kwa mwaka kulipia bima ya afya .
Ripoti ya Sikika inasema asilimia 80 ya watanzania hawana Bima ya afya. Sababu ya bei ghali ya Bima, tunawezaje kufikia Universal health Coverage (UHC) ifikapo 2030 kwa namna hii?
Lazima tuangalia namna ya kusaidia jamii yetu kupata huduma bora, rahisi na nafuu.
Mnaepuka majukumu msiulizwe maswali mengi kwa kujificha nyuma ya mgongo wa Bima ya afya ya jamii (improved community health fund) iCHF .
Mnajua changamoto ya mfuko huu ? ,Kwanza sio mpya , Sheria ya kuanzisha mfuko huu imetungwa tangu 2001 ,kwa sheria ya Bunge No.1 ya 2001 ,mnaweza kutuambia kiasi gani mfuko huu umeimarika ndani ya miaka 18 tangu 2001 ,Mfuko huu unachangamoto nyingi,ndio maana hata wananchi hawaujui .
Nitaziandika siku moja changamoto zake.
Ila tunapaswa kufikiria kwa mapana kusaidia jamii yetu , katika suala la afya na sio kuchangia mmoja mmoja , watanzania ni wengi wenye matatizo hayo.
Shukrani Kaka yangu ,Msando .
Abdul Nondo.