Kwako Kaka yangu ,Albert Msando

Kwako Kaka yangu ,Albert Msando

Kwanza napenda kukupongeza sana,kwa jitihada na moyo wako wa kusaidia jamii yetu.Umekuwa mfano bora kabisa katika jamii yetu na kwetu vijana.

Tuliona ulijitoa kuchangisha milioni 5 ,kumsaidia Mh.Rais kulipa deni la yule mama yetu aliyefiwa na mama yake Muhimbili .Na hakika leo tumeona umekabidhi fedha hizo hospital ya Muhimbili ,hongera sana kaka yetu.

Ila ,Mimi napata kukufananisha na kijana mmoja mwenye huruma sana anaitwa *Kalukalanga* , Siku moja Kalukalanga alipita msituni akakuta nyumba moja ikiwa imejitenga, alivyopita njiani karibu na nyumba ile akasikia sauti ya wamama wakilia kwa uchungu waokolewe kutoka katika chumba kimoja ,chenye giza kidogo.

Kalukalanga akachungulia dirishani ukamuona mmoja wa mama akilia kwa sauti akihitaji maji ya kunywa, huku mama wengine wakiwa wamelegea sauti hazitoki kwa unyonge .

Kalukalanga alivyojaliwa huruma ,akakimbia haraka kutafuta maji , akiomba huku na kule kwa rafiki zake na majirani zake ili chupa lijae akampe maji mama yule .

Alijaliwa kuyapata akampelekea mama yule dirishani ,yule mama akanywa .Kalukalanga akaondoka huku akisema moyoni nimemsaidia mama yule.

Kalukalanga hakujali kuwa mama yule hayupo pekeake katika kile chumba, bali wapo wengi katika chumba kile ,ila sababu walikuwa wamedhoofu hawakuweza kutoa sauti zao ila sauti ya mama yule mmoja ilipaswa kubebwa na Kalukalanga kwa uzito zaidi kama sauti wakilishi ya wamama wote mule ndani.

Pia Kalukalanga alijua amempa msaada mama yule ,ila Kalukalanga hakuwaza nani atakaye mpa tena mama yule maji au chakula hapo baadaye ikiwa sehemu ile hakuna wapitanjia wengi.

Msaada mkubwa Kalukalanga angeufanya kupitia sauti ya mama yule mmoja,angetafuta namna ya kuwaokoa wale wa mama kutoka katika chumba chenye giza ,mateso na unyong'onyefu kuliko kumpa maji tuu na kuondoka kwa kufikiri ametoa msaada wa kutosha.Ndio ni msaada ila sio msaada wa kutatua tena kiu chake hapo baadaye ,ikiwa maji yenyewe alikunywa yote sababu ya uchache.

Watanzania ni maskini , mikakati imara ya kusaidia upatikanaji rahisi wa huduma ya afya kwa mfumo wa pamoja ili kusaidia wengi zaidi.Kuliko mmoja mmoja ! Yes ni vyema mama alipaswa kusaidiwa ila tunapaswa kwenda mbali zaidi ,msaada alioupata ,anaweza uomba tena kama akipata shida kama hiyo siku zijazo .

Kipato cha mtanzania kwa mwaka ni Mil.2.4

Pia ndicho kipato cha yule mama hospital ,ambapo kama hana ajira rasmi anapaswa awe na mil,1.5 kwa mwaka kulipia bima ya afya .

Ripoti ya Sikika inasema asilimia 80 ya watanzania hawana Bima ya afya. Sababu ya bei ghali ya Bima, tunawezaje kufikia Universal health Coverage (UHC) ifikapo 2030 kwa namna hii?

Lazima tuangalia namna ya kusaidia jamii yetu kupata huduma bora, rahisi na nafuu.

Mnaepuka majukumu msiulizwe maswali mengi kwa kujificha nyuma ya mgongo wa Bima ya afya ya jamii (improved community health fund) iCHF .

Mnajua changamoto ya mfuko huu ? ,Kwanza sio mpya , Sheria ya kuanzisha mfuko huu imetungwa tangu 2001 ,kwa sheria ya Bunge No.1 ya 2001 ,mnaweza kutuambia kiasi gani mfuko huu umeimarika ndani ya miaka 18 tangu 2001 ,Mfuko huu unachangamoto nyingi,ndio maana hata wananchi hawaujui .

Nitaziandika siku moja changamoto zake.

Ila tunapaswa kufikiria kwa mapana kusaidia jamii yetu , katika suala la afya na sio kuchangia mmoja mmoja , watanzania ni wengi wenye matatizo hayo.

Shukrani Kaka yangu ,Msando .

Abdul Nondo.
chuo kikuu ndiko ulikoenda kufundishwa kuandika hizi riwaya?
 
Ushapata ajira mkuu?.
Naona umepata bando la kuja kutusumbua huku.
Wewe ambaye sio kalunguyeye umemsaidia nani?/ au hauna cheo na wewe tafuta kiki jina likuwe maana na msando naye lilikuwa lengo lake.
 
Msando msanii na ametumia fursa vizuri hiyo milioni tano itampa mabilioni muda siyo mrefu
 
Unajua haya mambo bana, sisi wengine tuliotoka mbali na haya mambo ya siasa tunawachora tu. Yaani wewe Nondo sasa unampiga shule Msando! Anyway labda ndio maana hatufanani, endeleeni na porojo zenu!

Hivi Msando yule enzi zile(tuachane na sasa) na huyu dogo ungeweza kuwaweka kapu moja? Dogo ushauri wangu wa bure kwako, achana na watu, focus kwenye issues! Nimemaliza.
Kwanini umpangie mtu chakuwaza?
 
Jamani mwenye mawasiliano ya Kaka Msando anisaidie pengine aweza nisaidia na mie raia niliye chini ya rais mpendwa.

Asante
 
Dogo ana uwezo sana badala ya wahusika kumuona adui wanatakiwa kuanza kumjenga katika nafasi za serikari ya miaka 20 ijayo.

Mabeberu ya miaka 20 ijayo na yenyewe yatakuwa na werevu zaidi kushinda ya leo kuichallenge inataka watu wenye uwezo.

Let’s face it kwa TISS ya leo ukilinganisha na wenzetu kwenye mambo ya maslahi ya taifa ni ovyo bado wapo defensive badala ya kuwa wabunifu. You need clever people to do that job and this kid looks the part.
 
Yawezekana alberto msando amefanya kama huyu kalukalanga uliyemtolea mfano..lakini swali la kujiuliza ni leo tu msando amejitokeza kuisaidia jamii?vipi kuhusu wale watoto wa chuo kikuu cha Dar ambao walikosa ada na yeye akachangisha na mpaka sasa wanaendelea na masomo na wengine wamemaliza degree zao?lakini kingine wewe ambaye sio kalukalanga umefanyanini ili kusaidia jamii inayokuzunguka?
Ni upuuz kuwaza kua Albert anaweza saidia “Jamii kwa mapana”(sijui hata huyu dogo anamaanisha nini since idadi ya watu ambao anasaidia ni kubwa mno ku affect jamii nzima).
Msando kafanya sehemu yake,wewe Kalukalanga umefanya nini ndo swali.Usiwe tu unatoa changamoto sababu huamini anachoamini yeye kwenye siasa...
 
Mida mingine serikali inapoteza hela kuwasomesha watoto kama hawa, bora hela zingeelekezwa kwenye tafiti ambazo zinatija kuliko kudhamini vichwa kama hivi.
 
Kwanza napenda kukupongeza sana,kwa jitihada na moyo wako wa kusaidia jamii yetu.Umekuwa mfano bora kabisa katika jamii yetu na kwetu vijana.

Tuliona ulijitoa kuchangisha milioni 5 ,kumsaidia Mh.Rais kulipa deni la yule mama yetu aliyefiwa na mama yake Muhimbili .Na hakika leo tumeona umekabidhi fedha hizo hospital ya Muhimbili ,hongera sana kaka yetu.

Ila ,Mimi napata kukufananisha na kijana mmoja mwenye huruma sana anaitwa *Kalukalanga* , Siku moja Kalukalanga alipita msituni akakuta nyumba moja ikiwa imejitenga, alivyopita njiani karibu na nyumba ile akasikia sauti ya wamama wakilia kwa uchungu waokolewe kutoka katika chumba kimoja ,chenye giza kidogo.

Kalukalanga akachungulia dirishani ukamuona mmoja wa mama akilia kwa sauti akihitaji maji ya kunywa, huku mama wengine wakiwa wamelegea sauti hazitoki kwa unyonge .

Kalukalanga alivyojaliwa huruma ,akakimbia haraka kutafuta maji , akiomba huku na kule kwa rafiki zake na majirani zake ili chupa lijae akampe maji mama yule .

Alijaliwa kuyapata akampelekea mama yule dirishani ,yule mama akanywa .Kalukalanga akaondoka huku akisema moyoni nimemsaidia mama yule.

Kalukalanga hakujali kuwa mama yule hayupo pekeake katika kile chumba, bali wapo wengi katika chumba kile ,ila sababu walikuwa wamedhoofu hawakuweza kutoa sauti zao ila sauti ya mama yule mmoja ilipaswa kubebwa na Kalukalanga kwa uzito zaidi kama sauti wakilishi ya wamama wote mule ndani.

Pia Kalukalanga alijua amempa msaada mama yule ,ila Kalukalanga hakuwaza nani atakaye mpa tena mama yule maji au chakula hapo baadaye ikiwa sehemu ile hakuna wapitanjia wengi.

Msaada mkubwa Kalukalanga angeufanya kupitia sauti ya mama yule mmoja,angetafuta namna ya kuwaokoa wale wa mama kutoka katika chumba chenye giza ,mateso na unyong'onyefu kuliko kumpa maji tuu na kuondoka kwa kufikiri ametoa msaada wa kutosha.Ndio ni msaada ila sio msaada wa kutatua tena kiu chake hapo baadaye ,ikiwa maji yenyewe alikunywa yote sababu ya uchache.

Watanzania ni maskini , mikakati imara ya kusaidia upatikanaji rahisi wa huduma ya afya kwa mfumo wa pamoja ili kusaidia wengi zaidi.Kuliko mmoja mmoja ! Yes ni vyema mama alipaswa kusaidiwa ila tunapaswa kwenda mbali zaidi ,msaada alioupata ,anaweza uomba tena kama akipata shida kama hiyo siku zijazo .

Kipato cha mtanzania kwa mwaka ni Mil.2.4

Pia ndicho kipato cha yule mama hospital ,ambapo kama hana ajira rasmi anapaswa awe na mil,1.5 kwa mwaka kulipia bima ya afya .

Ripoti ya Sikika inasema asilimia 80 ya watanzania hawana Bima ya afya. Sababu ya bei ghali ya Bima, tunawezaje kufikia Universal health Coverage (UHC) ifikapo 2030 kwa namna hii?

Lazima tuangalia namna ya kusaidia jamii yetu kupata huduma bora, rahisi na nafuu.

Mnaepuka majukumu msiulizwe maswali mengi kwa kujificha nyuma ya mgongo wa Bima ya afya ya jamii (improved community health fund) iCHF .

Mnajua changamoto ya mfuko huu ? ,Kwanza sio mpya , Sheria ya kuanzisha mfuko huu imetungwa tangu 2001 ,kwa sheria ya Bunge No.1 ya 2001 ,mnaweza kutuambia kiasi gani mfuko huu umeimarika ndani ya miaka 18 tangu 2001 ,Mfuko huu unachangamoto nyingi,ndio maana hata wananchi hawaujui .

Nitaziandika siku moja changamoto zake.

Ila tunapaswa kufikiria kwa mapana kusaidia jamii yetu , katika suala la afya na sio kuchangia mmoja mmoja , watanzania ni wengi wenye matatizo hayo.

Shukrani Kaka yangu ,Msando .

Abdul Nondo.
Wewe zwazwa unaemuiga Zitto kwani umekatazwa kwenda kutoa msaada na wewe. Alafu embu mfuatilie huyo Msando kama huyu ndie mtu wa kwanza kumsaidia. Wivu mwingine wa kipuuzi sana. Kinachowauma ni nini na mtu katumia pesa yake? Tabia za kike hizo mpaka tunaanza kupata shaka na wewe, tabia zako hazina tofauti na Suphian yule wa Twitter
 
Kuchangisha pesa UMMA na Harambee zisizoisha ni kuwa na taifa la ombaomba bila watu kufanya wajibu wao.. yule mama anayechangiwa hakupaswa kuwepo katika hali ile kama watu katika nafasi zao wangewajibika.., na tutaendelea kuchangishana mpaka lini badala ya kuchangishana pesa za kupumzisha tatizo tuchangishane mawazo ya kuondoa tatizo.. (na kama sikosei kuna watu tunawalipa na wanakula kodi zetu ili walete mawazo mbadala ila wanchofanya ni business worse than usual)
Umeandika vyema kwamba wapo waliopaswa kutatua changamoto kama hii aliyokutana nayo Mh.Rais lakini wameshindwa kufanya inavyostahili, hata mimi nilishangazwa na kusikitishwa sana kuona hali hiyo nilijiuliza hivi maprofesa wote hao hapo muhimbili na wasomi wote wameshindwa kabisa kubuni namna ya kukabiliana na tatizo kama hili sababu sidhani ni mara ya kwanza inatokea, yaani wao hawana habari na uwezo wa waangalizi wa wagonjwa wao kiuchumi..kama wataweza kumudu gharama za matibabu ya mgonjwa wao???kama wanadhani si jukumu lao basi hata huduma yao si ile inatoka moyoni kusaidia watu! walipaswa wajue mambo haya, mgonjwa anapolazwa hospitalini kwao wanapaswa kuwa na details zote si za ugonjwa tu, hata background ya mgojwa kijamii na kiuchumi..anatoka wapi, nani amemleta, anajishughulisha na nini, nani wanamhudumia akiwa nyumbani nk, haya nayo ni sehemu ya tiba! Nitoe ushauri hata kwa msando, ipo hospitali moja sitaitaja kwa jina wao wana kitu kinaitwa Hospital Bed Fund..ni mfuko wa kusaidia gharama za matibabu kwa wale wote wanakuwa na vigezo vya kusaidiwa pale inapohitajika, ni mfuko unachangiwa na watu wote wakati wowote, hospitali inausimamia kiuendeshaji na kwa kweli unasaidia sana kupunguza makali ya kuuguliwa muda mrefu na hata pale mgonjwa inapotokea amefariki..Msando asiishie hapo vile amejitolea kumsaidia Mh. Rais kwa jukumu hili.
 
Hizi ni kanuni za njia.

1. Kusaidia jamii nzima ipate suluhu ya suala la afya ni bora kuliko kumsaidia mtu mmoja mmoja.

2. Kumsaidia mtu mmoja ni bora kuliko kutosaidia hata mtu mmoja.

3. Kutomsaidia mtu hata mmoja ni bora kuliko kumhatarisha mtu mmoja

4. Kumhatarisha mtu yeyote si bora zaidi ya kuhatarisha wengi

5.Kuonesha kitu kizuri zaidi kwa vitendo ni bora kuliko kusema maneno

6. Kumsifia anayefanya vizuri ni bora zaidi ya kukaa kimya

7. Kukaa kimya ni bora zaidi ya kumvunja moyo anayefanya vizuri

8.Kutoa bila matangazo ni bora zaidi ya kutoa kwa matangazo

9. Kutoa kwa matangazo ni bora zaidi ya kutotoa

10 Kutotoa ni bora zaidi ya kubadhiri cha muhitaji
 
Back
Top Bottom