Kwako Harmonize, chukua ushauri huu

maatope

JF-Expert Member
Sep 19, 2013
1,424
957
Kwanza hongera,show ya mtwara wewe ndiye ulikuwa star,ndugu yetu aliiingia akiwa amelewa kabisaaa mapombe sijui ecstacy anajua mwenyewe kaka ulivyoimba nyimbo za lucky dube kwanza hongera ulini suprise kwa ulivyojitahidi kuimbakiingereza,najua ulimeza maneno na background yako ya maisha ulipofika sio haba.

Ila najua wasafi festival itaenda Nairobi mwezi december,kule kenya wewe ni celebrity a list tafadhali usiimbe zile nyimbo a english live,kwa mfano nyimbo ya lucky dube DADDY WHEREVER YOU ARE REMEMBER ME, ulikuwa unatamka DADDY WHELEVER YOU ARE LEMEMBER ME.

Ni shida ya matamko unayo hata kwa kiswahili,ukifanya hilo kosa wakenya wata ku slam vibaya sana ,mazuri yao yote wataweka pembeni maanake najua KWANGWARU lazima ikalishe uhuru park sio wakenya wote wanapenda jinsi nyie wadogo zetu wa kitanzania mlivyokamata soko la kenya ndo maana siku hizi vitimbwi vingi,mara steji mbovu aslay kanguka,mara wewe harmonise haulipwi hela ya show unazuiliwa hotelini sasa mnawafata tena kwao na festival yenu narudia tena,usiiimbe live nyimbo za english ukiwa Nairobi,imba hata sina makosa ya les wanyika
 
Ushauri mzuri kwa manufaa yake mwenyewe.

Diamond kapanda amelewa (kama ni kweli) yafaa managers wake wachukue hatua mapema
 
Back
Top Bottom