Kwako Dr.Ayoub Rioba Chacha

Mimi kanifundisha mwaka jana SAUT japo bado sijamaliza somo la Ethics ( GRS ). Jamaa ni zaidi ya MTAALAM au FUNDI katika masuala ya Media and Journalism. Na kama hatobadilika basi nina uhakika TBC itabadilika na tutajivunia nayo.
Akiibadilisha TBC kibarua chake kitaota nyasi si unakumbukaya Tido Mhando
 
Nilikuwa nasoma makala yake kwenye gazeti la raia mwema, dah, tata yuko vizuri sana, tena nilijiuliza inakuwaje mtu kama Ayoub Ryoba akose hata ubunge kama sio uwaziri kutokana na uzalendo wake kwa nchi yake? Kwa kweli kwa uteuzi huo nampa pongezi JPM, tena Ayoub Ryoba angefaa kuwa waziri wa habari kabisa.
 
Mimi kanifundisha mwaka jana SAUT japo bado sijamaliza somo la Ethics ( GRS ). Jamaa ni zaidi ya MTAALAM au FUNDI katika masuala ya Media and Journalism. Na kama hatobadilika basi nina uhakika TBC itabadilika na tutajivunia nayo.
Mkuu Ayoub Ryoba si alikuwa UDSM, sasa huko SAUT Mwanza alifikaje?
 
Ni kiongozi mzuri,hana madharau,mshauri mzuri. Mwanzoni miaka ya 1990 alikuwa Ilboru kwa A-level,HGL. Nilikuwa kiongozi wake wa bweni,Oldonyo. Alikuwa anatupiga shule O-level. Baadaye akachaguliwa kuwa katibu wa shule,Mr. Bango,enzi ya Mr G.Mushi,mkuu wa shule (jina la utani Mr Bino...G. Binaisa). Huyu mzee alikuwa mkali Sana kwa nidhamu.
 
Umenikumbusha mbali... acha ayoub afanikiwe tu
 
Natamani huyu bwana apewe Uhuru ili mvuto wetu wa kuisikiliza TBC urudi kama chombo cha utangazaji cha taifa
 
Mkuu Ayoub Ryoba si alikuwa UDSM, sasa huko SAUT Mwanza alifikaje?

Aliyekuambia SAUT ipo Mwanza tu ni nani? SAUT ipo Dar na ni ya Wanafunzi tu wa Masters na PhD japo wanatoa sasa Kozi za Journalism kwa ngazi za Certificate na Diploma. Ipo Msimbazi center karibu na Kanisa la Katoliki. Ningemaliza mwaka huu ila kuna mambo fulani yaliingilina hivyo naweza kumaliza mwaka huu au nikahairisha tena hadi 2017. Nimemaliza almost 75% nimebakiza Proposal na Dissertation tu huku nikiwa na Vimeo vyangu viwili vya kumalizia nami nivae Joho. Niombee mkuu.
 
Nakumbuka Dr Ayoub Ryoba aliwahi kumhoji Dr Magufuli wakati tukikaribia kwenye uchaguzi ilikuwa nadhani 2010 au 1995, wote hawakuwa na ma Dr kama ilivyosasa ila Dr Magufuli alikuwa waziri wa Ujenzi, Baada ya mahojiano wakati wanahitimisha, Ayoub akamtakia kila la kheri kwenye uchaguzi na ndipo Ryoba akaulizwa na Magufuli, nyumbani ni wapi ka mara mbili jamaa alipotezea ka hajaskia
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…