CONTROLA
JF-Expert Member
- Sep 15, 2019
- 6,939
- 22,989
- Acha mazoea yaliyozidi na kuvuka mipaka na Watumishi/wafanyakazi wako
Mfano unaweza kukuta mfanyakazi anamtania boss wake "boss demu wako anakuita" na anajua fika boss wake ana mke na watoto.
Huu utani wa namna hii sio mzuri na haufai,yapo mazoea ya aina nyingi ila cha kuzingatia awe na mipaka.
- Kukaa ofisini/dukani na Mfanyakazi
Yawezekana una duka moja na huna mahali pa kwenda basi nashauri dukani toka kaa hata huko nnje ya duka muache dukani akae yeye wateja wakija aongee nao yeye.
Kukaa na boss mbele yake kunampotezea ujasiri wa kuongea na mteja.
Mfano: Mfanyakazi wa kike then mteja kaja wakiume Moja ya mbinu ya mfanyakazi wako ili yule mteja anunue kitu ni kuji bebisha kwake na kum bembeleza.
Sasa boss unapokuwa eneo la tukio unamfanya mfanyakazi ashkndwe tumia tekniki za kazi kwa kukuogopa utamchukuliaje nk nk.
- Zawadi
Heshima ya kupitiliza ni ile unaingia kazini mfanyakazi anakusalimia shikamoo, unatoka nje ukirudi ndani anahisi kama hajakusalimia anakusalimia tena.
Hapo fahamu tu kuwa unaogopwa.
ili kutengeneza/kuimarisha mahusiano mazuri kati yako na team yako si mbaya kama mara moja moja ukawa unawapa zawadi staff wako.
Zawadi inaweza kuwa chochote ambacho kipo ndani ya uwezo wako. Hata kama wewe ni mama ntilie uwezo unao wakuwapa wafanyakazi wako zawadi.
Unaonaje siku 1 ukajitoa fahamu ukawmbia wafanyakazi wako wajipikie Chakula wanachotaka wa kula kuku ale, paka ale,mbwa ale wape pesa wakanunue mahitaji yote wayatakayo sio kila siku unawalisha ugali wali ugali wali.
Kama una duka la nguo unaweza jitoa ufahamu tu siku ukamwambia mfanyakazi achague nguo anayotaka avae.
Mfanye ajisikie raha na bahati kupata boss kama wewe, unaweza mlipa mtu mshahara mdogo ila kutokana na jinsi unavyoishi naye ukajikuta anadumu kwako hadi unashangaa.
- Mapumziko
Wape/mpe wafanyakazi wako mapumziko hata kama yeye atakwambia sijachoka "usimsikilize" ni muongo hawezi kukwambia kachoka hata siku 1 maana anajua utamuona lege lege hivyo basi Mapumziko ni lazima na sio ombi, wape nafasi wapumzike,wape nafasi yakufanya mambo yao,mfanye ajione kuwa nae yupo huru na si kwamba ni MTUMWA mpe uhuru kabisa.
Mueleze faida za kupumzika maana kusema ukweli kuna wafanyakazi hawataki Off wapo kama vile marobot ni vizuri saawa mtu afanye kazi ila hapana isizidi bwana hata yeye ni binadamu anahitaji kusaidiwa kupumzishwa.
- Mavazi
Yawezekana una duka hata la kawaida una kijana wako m1 mtafutie tshirt 1 ya form six rangi flani iwe ndio sare yake ya kazini.
Chini avae suruali/skirt,nl vyvyte ila juu hakikisha mtu yeyote anaefanya kazi kwenye ofisi yako ana utambulisho wa sare, kuna faida sana eneo hili.
Tumeshazoea kuona wahudumu wa bar tu ndio wana sare lakini nani kasem sare ivaliwe na wahudumu tu?
Sare ya kazi inatakiwa iwe kila mahali hvyo na wewe kama unapenda kuwa Boss/mwajiri unaejillewa usikubali wafanyakzi wafae watakavyo wanapokua eneo la kazi.
- Kuajiri Ndugu
- Mahusiano ya kimapenzi ofisini