Kwako Beno Malisa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwako Beno Malisa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Chaimaharage, Apr 17, 2012.

 1. Chaimaharage

  Chaimaharage JF-Expert Member

  #1
  Apr 17, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 211
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jana nimekuona Martin Shigella kwenye taarifa ya habari ya saa 2 usiku TBC1 ukitoa comments zako kuhusu kitendo cha aliye kuwa mwenyekiti wa UVCCM A-town Ndg.James Millya kujiondoa Magamba. Kauli uliyotoa ya kwamba falsafa ya kujivua gamba inaendelea ukieleza kuwa Millya alikuwa gamba kwa hiyo amepima na kujiondoa mwenyewe. Sasa nashindwa kuelewa kama kweli alikuwa gamba au la. Kauli yako inatofautiana na ya Mh.Mbowe ambapo yeye ameonyesha kuwa Bwana Millya wanamfahamu kwa muda mrefu na hana historia chafu kama mnavyotaka kutuaminisha.

  Kwa mtizamo huu ni wazi kuwa kwa tafsiri yenu mtu ni gamba iwapo ataonekana kuwa mshauri wa kukitaka chama kufuata misingi bora na ya haki katika utendaji wake na mengine mema yanayo fanana na hilo. Na ambao siyo magamba ni wale mafisadi walio kubuhu na kuonekana kupingwa na umma kwa ujumla wake. Watu hawa mmekuwa nao kwa muda mrefu pasipo kuwachukulia hatua yoyote.Hakika CDM hawawezi kutamka maneno yale iwapo mtu husika ni gamba halisia tofauti na tafsiri yenu. Nadhani time will tell ku justify kama kweli tuhuma zako juu ya Millya kuwa ni gamba ni za kweli. Sina wasi wasi kuwa aibu itakushikeni mbele ya safari.

  Na mimi pia napenda kutoa wito wangu kwa watu walio magamba ambao wanajiona safi na kukerwa na uchafu ulio kithiri humo tokeni. Tunawajua wamo wengi tu! ila hofu tu ndiyo inawaogofya kuchukua maamuzi. Ila najua muda utafika watatoka.Lakini katika hili napenda kutoa angalizo; wale wote wenye nia halisi ya kutaka mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi katika nchi hii ili kufikia ukombozi wa kweli wafanye sasa. Watakapo taka kujiondoa huko waliko kipindi cha chaguzi ndogo na mkuu tutakuwa na mashaka dhidi ya dhamira yao. watakapo enguana katika chaguzi za ndani kisha kukimbia hao siyo wana mageuzi halisia bali ni wachumia tumbo wenye njaa kali na maslahi binafsi.

  Kwa kumalizia napenda kusema hivi; MARTIN SHIGELLA, BENNO MALISA NA WENZIO KAMA VILE NAPE NI MAGAMBA HALISIA, HATA MKIJIVUA GAMBA HAMTO POKELEWA CDM KAMA MWENZENU. Iwapo mtapokelewa basi mtakaa kama miaka 10 mnasafishwa uozo ulio ndani yenu sababu sidhani kama fikra na mioyo yenu viko sawa na ni aibu kwa vijana kama ninyi kuwa na hivyo mlivyo na kutenda hayo mnayo tenda. Your future is vague. No light at the end of the tunnel.

  Masahihisho katika thread yangu;
  Jana fundi mitambo TBC1 alionyesha jina la aliye kuwa akihojiwa ni Beno Malisa lakini ki ukweli alikuwa ni Martin Shigella na siyo yeye. Lakini pamoja na yote fikra na mawazo yao ni sawa. Nawashukuru walio nisahihisha. Cha msingi ni kwamba concept ya ujumbe imefika. Gamba mmoja ni sawa na yote hata ukikosea kumtaja comment utakazo toa juu yao zinawagusa wote.
   
 2. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #2
  Apr 17, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Benno ni mtu wa aina ya " sizitaki mbichi hizi".
   
 3. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #3
  Apr 17, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  anasusa lakini cdm wameshatwaa
   
 4. Bundewe

  Bundewe JF-Expert Member

  #4
  Apr 17, 2012
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 401
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Aliyeongea sio BENNO ni comred REUBEN MARTIN SHIGELA, Katibu Mkuu UVCCM Taifa. Namfahamu sana huyu kijana, nilisoma naye, nafahamu udhaifu wake, hivi karibuni naye atatangazwa kuwa GAMBA, atavuliwa asipojivua mwenyewe.
   
 5. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #5
  Apr 17, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Sijakuelewa mkuu, Una maana MILLYA siyo kama NAPE NA MALISA na kwa maana hiyo karibuni atakwaa ulaji ndani ya Chama? je ni kweli kwamba MILLYA si gamba na kwa maana hiyo EL pia u msafi? duh! siasa bwana nooooooooma. Hivi siku NAPE na BENO wakitangaza kuhamia CDM na kupokelewa utafutia wapi ushududa wako huu kwa sababu nakumbuka CDM walimlaani sana MILLYA kuwa ni chanzo cha vurugu Arusha.
   
 6. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #6
  Apr 17, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Mkuu, hata Benno na Shigella pia wanakaribishwa ndani ya chama cha wazalendo CDM.
   
 7. j

  jossy chuwa Member

  #7
  Apr 17, 2012
  Joined: Apr 4, 2012
  Messages: 93
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ninachokiona nilitaraji na nataraji wengine kibao japo wanaweza kuja kama maji ya mafuriko ambayo yana contain takataka za kila aina cdm kazi yake kuchambua tu kwa maana ya intelijensia ya cdm ifanye kazi ya ziada ili kama kuna wanaokuja kwa maana ya kubomoa watiwe adabu mapema.. maana tusifurahie tu watu kuja bali tuangalie mbinu ni nyingi sana za kutokomeza mapinduzi ya kweli yanayoletwa na cdm. kusema kweli ccm hawataki tuamke ili watutafune wanavyotaka wenyewe. ukisema ukweli wa jambo lolote wewe ni adui hata kuuwawa si ajabu wala jambo kubwa.. nasisistiza umakini..
   
 8. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #8
  Apr 17, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Upo sahihi mkuu. Kinachotakiwa ni Chadema kuwafanyia intensive character assessment wanachama wote wapya bila kuwasahau na hawa waliopo tayari ndani ya chama.
   
 9. j

  juu kwa juu JF-Expert Member

  #9
  Apr 17, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 260
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  chai maharage.. Aliyeongea si beno ni shigella, kwa ondoa thread yako hapo juu maana hauko makini kaka au dada. Haina mashiko tena.
   
 10. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #10
  Apr 17, 2012
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  naikumbuka kauli ya millya,akisema riz1 aache kimbelembele,tumemchagua babake awe rais wala si riz1. Millya alikuwa kati ya wanaccm kiduchu wanaoweza kuifunda hadi familia ya ikulu,namkubali ole millya...hata nape hawezi kukemea uozo wa familia ya ikulu vingnevo kibarua kinaota nyasi aina ya kwekwe yani comelina bigalensis! Millya karibu kwa makamanda!
   
 11. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #11
  Apr 17, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  hakuna dini yoyote duniani inyomkataa mtu mwovu ilimradi akiri na kutubu na msamaha atapata.
  walokole wana usemi maarufu unowaita wale walioacha dhambi na kumrudia bwana kuwa wameokoka,hawaulizwi tena kuhusu dhambi zao mradi wamekiri na kuamini na kuachana na shetani.
  waislam nao hivyohivyo kila anaeamini na kuacha maovu akaamini na kusilimu vilevile hahukumiwi kwa dhambi za kale ilimradi hazirudii tena.

  TUJE KWENYE SUALA LA MAFISADI.
  CCM IMEOZA,KIIMANI CCM NI KAMA SHETANI NA UCHAFU WOTE UMO NDANI YAKE,KILA ALIYEPO CCM NI GAMBA,MZIGO,FISADI KAMA WAO WALIVYODAI JANA,MILLYA AMEOKOKA AU KUSILIMU KUANZIA JANA AMEACHANA NA DHAMBI AMEMWAMBIA SHETANI BAIBAI SASA YUPO KATIKA MAISHA MAPYA,MAISHA YA IMANI,YA KALE YAMEPITA NA SASA YAMEKUWA MAPYA.
  NAPE,MAKAMBA,SHIGELA,BENO,NA VIJANA WENZENU MLIOPO DHAMBINI TUNAWAOMBA MJIPIME MAISHA YA DHAMBI YANAPITA NA NI YA KITAMBO TU,MIKONO YENU IMEJAA DHULMA,DAMU NA JASHO LA WATANZANIA.
  JITAFAKARINI KAMA ALIYEKUWA MWOVU MWENZENO MILLYA MKAACHANE NA DHAMBI(CCM)NA KUMRUDIA MOLA(UKOMBOZI WA NCHI DHIDI YA DHULMA).

  ushauri kwa chadema si kila anayeingia ndani ya chadema kutoka ccm anafaa kuwa kiongozi kwa sasa,na wengine hawafai kuwa viongozi kamwe, msiwaonee haya waambieni ukweli kuwa watakuwa wanachama wa kawaida na wengine itabidi wafundisshwe uzalendo kwa nza,najua watoto wa vigogo hawatakubaliana nanyi lakini ni bora msimamie hilo.

  msiiache falsafa ya kurudisha madaraka kwa wanyonge kwa kuwapa nafasi watoto wao kama nasari,zito sugu nk.

  ccm tumeshajua kumbe gamba ni yeyote ambaye anapinga ufisadi kwani imshakuwa sera ya chama.
   
 12. iron2012

  iron2012 JF-Expert Member

  #12
  Apr 17, 2012
  Joined: Feb 16, 2012
  Messages: 358
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  swali ww unayehukumu upo safi mpaka moyoni au ni walewale
   
 13. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #13
  Apr 17, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Yaani Nape na Beno, kumsimanga milya ni vichekesho sana, labda niwakumbushe, kama nyinyi ni wapigania haki, basi lazima mtambue wapigania haki wenzenu, la basi mtakuwa wanafiki. Na hakuna njia ya kistaarabu kama unapoona mahala pananuka sana, na wakati unatafuta suluhisho, kuondoka hapo. Siamini maneno yenu, naona kabisa bila kusita kwamba yamejaa unafiki mtupu. CCM ni janga la Taifa. Unafiki, kujipendekeza na umbea, nawajua vizuri sana.
   
 14. nashy

  nashy JF-Expert Member

  #14
  Apr 17, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 679
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Shigela ni yule aliyesoma UDSM? very poor personality
   
 15. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #15
  Apr 17, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  aliyeongea na media jana alikuwa shigela sio malisa mkuu
   
 16. m

  matawi JF-Expert Member

  #16
  Apr 17, 2012
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 2,055
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  shibuda hawajamfukuza makusudi ili iwe reference so dont worry about chadema wako imara
   
 17. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #17
  Apr 17, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  milya anautaka ubunge wa arusha ndio mana ameenda chadema,akitoswa huko sijui atahamia chama gani tena
   
 18. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #18
  Apr 17, 2012
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  MILLYA SIKU HZ UNATUMIA HII ID??UMEENDelEA SANA MKUU
   
 19. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #19
  Apr 17, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Sasa hivi kwa ushauri tu Milya tumia avatar yako na picha yako. Kwani sidhani una nia yeyote mbaya humu JF.
   
 20. Bitabo

  Bitabo JF-Expert Member

  #20
  Apr 17, 2012
  Joined: Sep 27, 2011
  Messages: 1,896
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  Hivi huyu Shigella na Benno si ndo walileta vijana kwa mabasi Dodoma ili waanzishe fujo kama UVCCM ingefutwa??? JK akawaambia wasitishie amani na kama wakitaka kuondoka waende tu. Nakumbuka Benno aliwashiwa moto mpaka akanywea.

  kama ndo hawa ni bora wajiandae tu kuhamia ADC (bendera yao inafanana na M4C) maana JK huwa ni mzee wa visasi na kwa ujinga wao wa Dodoma, siku zao si nyingi
   
Loading...