Kwahili nakubaliana na FAIZA FOXY

Kwahili nakubaliana na FAIZA FOXY

Zyamwelele

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2013
Posts
405
Reaction score
155
Baada ya kupitia uzi unaomuongelea mtoto wa miaka mitatu mwenye uwezo wa kufanya hesabu na kuongea kiingereza' nimepitia comment za watu tofauti lakini nachelea kusema naungana na Faiza Foxy kwamba huyo mtoto anaendeshwa na nguvu ya ziada.

Nasema hayo nikiwa na mfano hai' kama mtakumbuka Sheikh SHARIF IDD ilikuwa habari nyingine kabisa' yaani toka Yuko tumboni mwa mamaake inasemekana alikuwa anaongea (nasema inasemekana kwa sababu sijawahi kumsikia zaidi ya kuhadithiwa Tu)'' sasa Leo hii huyo Sheikh Sharif ni tapeli mwalijua hilo?

Kwa sababu kwa hali ya kawaida watu ambao ni 'majiniazi', 'ujiniazi' wao hauanzi kutoka kusikojulikana'. Yaani mtu baada ya kufundishwa kitu ndipo anafanya kwa kiwango cha juu na kuongeza vitu ambavyo mpaka mfundishaji anashangaa kuona', mpaka nafsi ya mtu muwezeshaji inakubali na kusema huyu mtu atakuwa na uwezo wa ziada.

Sasa huyo mtoto eti anafanya hesabu za Sekondari kafundishwa wapi? Na nani mfundishaji wake? Bora angekuwa anaongea kiingereza tu tungesema labda anasikia kutoka kwa watu wanaomzunguka, lakini hili la kusolve hesabu kuna ???? Nyingi Sana.

Majiniazi wengi ambao wana uwezo mkubwa hata kabla ya kupelekwa shule. Uwezo wao huonekana kwenye vitendo, mfano utaona mtoto anabuni kutengeza kitu fulani mpaka unayemuona unashangaa kajulia wapi? Lakini sio kufanya vitu vinavyofanywa kwa formula fulani kama hesabu.

Na watu wa namna hiyo hata asipopelekwa darasani au kufundishwa kitu anakuwa na uwezo mkubwa wa utendaji kwenye fani fulani, mifano mingi juu ya hilo mtakuwa nayo wenyewe!

Kwahayo machache nakubaliana na mtazamo wa FaizaFoxy juu ya huyo mtoto upo sahihi kabisa, anayebisha na abishe Tu!!

Tujitahid kumuomba Mungu atupe jicho la tatu; yaani tuwe na uwezo wa ziada wa kuyatizama mambo na sio kuamini kila unachokiona na kukiskia. Hivyo huyo mtoto ana jini ndilo linalofanya hayo yote.

YESU au Nabii ISSA mwenyewe alizaliwa kama mtu wa kawaida kabisa ila matendo yake ndio yaliyowafanya watu waamini kuwa huyu mtu sio wa kawaida.
 
Last edited by a moderator:
Hata nami nilikubaliana naye. Badala ya kufurahi na kujitangaza ni bora waende kufanyiwa naombi. Kama nguvu ni za giza basi itajidhihurisha na kama nguvu za Roho Mtakatifu itajulikana pia. Shetani hakupi bila kuchukua kikubwa zaidi maana kazi yake ni ku kill, steal and destroy. Lkn kama ni kutoka kwa Mungu basi itakuwa ni kwa nanufaa yake, familia, nchi na dunia nzima kwa sifa na utukufu wa Mungu.
 
Naona Kuna watu wanabishana nae Sana kwenye ule uzi' lakini hata hivyo anajitahidi kuwaelewesha!! Ila yupo sahihi Sana kwa Hilo.
 
Kwanza wote kwa pamoja mleta mada na faiza fox tukubaliane kuwa sheikh sharif nayeye alikuwa anaongozwa na majini kama ilivyo kwa huyu dogo.ndipo tuendelee na mjadala.

Maana anaweza kuja kukataa hapa huyu mama.maana si unajua huyu ni sheick?
 
Mimi nakubaliana kabisa juu ya hilo'' na ndio maana nimemtolea mfano.
 
Mimi nakubaliana kabisa juu ya hilo'' na ndio maana nimemtolea mfano.
wiki 2 zilizopita kuna mtoto alizaliwa huku morogoro maeneo ya turiani akaanza kuongea akisema kuna mvua kubwa itanyesha siku ya jumatatu na jumanne.na watu wasichote maji yake wala kuyatumia watakufa kisha yule mtoto akafa.matokeo yake mvua ikanyesha jumatano na hakuna aliyekufa
 
Waafrika sisi kweli hovyo kabisa ngoja agundue mzungu mwafrika karoga na anatakiwa kuombewa jamani hadi huruma kama ndo kila kitu mnawaza uchawi bas tumekwisha
 
Waafrika sisi kweli hovyo kabisa ngoja agundue mzungu mwafrika karoga na anatakiwa kuombewa jamani hadi huruma kama ndo kila kitu mnawaza uchawi bas tumekwisha
Umeelewa kinachozungumziwa lakini?haya huyo mtoto kagundua nini? Kuna mzungu alizaliwa akijua kuandika bila kufundishwa namna ya kuandika? Tusingekuwa na maswali kama angekuwa anafanya mambo ya kutengeneza vitu Fulani bila kufundishwa ILA hili la kusolve equation bila kufundishwa hata formula zake sio kipaji hicho kuna jambo.
 
wiki 2 zilizopita kuna mtoto alizaliwa huku morogoro maeneo ya turiani akaanza kuongea akisema kuna mvua kubwa itanyesha siku ya jumatatu na jumanne.na watu wasichote maji yake wala kuyatumia watakufa kisha yule mtoto akafa.matokeo yake mvua ikanyesha jumatano na hakuna aliyekufa
Sijaipata hii ilikuwaje?
 
Mungu anaweza kumpa ujuzi au elimu kiumbe yeyote amtakaye,na ndiyo maana mie toka mwanzo sikukubaliana na faiza foxy kusema kuwa huyo mtoto anaweza akawa ana jini ndiyo lenye kufanya hivyo. Japo najua uwezekano huo upo lakini hatuwezi kusema hivyo kwa haraka kwa sababu anaweza akawa hana tatizo la kijini na ikawa ni miujiza yake Mungu. Mfano huyo Sheikh Sharif,zidhani kama faiza foxy atakubali kuwa Sheikh sharif naye alikuwa na tatizo la kijini kama asemavyo kwa huyo mtoto.Wapo wataalamu wa mambo ya kijini wanaweza kujua kama huyo mtoto ana tatizo la kijini au sivyo hivyo.

Ni maoni yangu tu.
 
Last edited by a moderator:
Ivi vitu mbna vipo, au hamjasikia watoto wadogo chini ya miaka 10 wamehack server za NASA, FBI uko marekani.. Things which are almost impossible for an adult to do
 
Hata nami nilikubaliana naye. Badala ya kufurahi na kujitangaza ni bora waende kufanyiwa naombi. Kama nguvu ni za giza basi itajidhihurisha na kama nguvu za Roho Mtakatifu itajulikana pia. Shetani hakupi bila kuchukua kikubwa zaidi maana kazi yake ni ku kill, steal and destroy. Lkn kama ni kutoka kwa Mungu basi itakuwa ni kwa nanufaa yake, familia, nchi na dunia nzima kwa sifa na utukufu wa Mungu.

Sijui kama huyu jamaa alishawai kumpeleka hata kufanyiwa sala.
 
Back
Top Bottom