Kwaheri upinzani Tanzania

navy boi

JF-Expert Member
Mar 15, 2014
1,517
480
BYE BYE UPINZANI TANZANIA.

NAANZA kuona KIFO Kibaya kwa UPINZANI wa TANZANIA masikini ambao uliweza kuishi kwa kutegemea makosa na U DHAIFU wa SERIKALI,

SASA hivi RAIS akitoa HOTUBA inaungwa mkono na WATANZANIA wote na wanaijadili kwa muda mrefu huku kila HOTUBA ANAYOTOA ikileta MATOKEO ya moja kwa moja kwa WANANCHI mfano aliposema kuhusu ufinyu wa BAJETI wa MAHAKAMA baada ya siku amewakabidhi BILIONI 22, Amezungunza na wazee wa DSM kuhusu JENGO la WAZAZI MUHIMBILI tayari JANA MAOFISA wa WIZARA WAMEHAMA na leo kazi ya kuweka VITANDA inaendelea ili WAJAWAZITO walale humo nauonea HURUMA sana.

UPINZANI ndio maana kila SIKU unazungumzia suala la ZANZIBAR kama AGENDA kuu Sasa sijui baada ya MARCH 20 UCHAGUZI utakapokwisha sijui WATAONGEA nini MASIKINI,
WA JIANDAE tu turudisha VITI VYA UBUNGE mwaka 2020 kwa CCM WALIOVIAZIMA MWAKA JANA

ITAKUWA ni HUZUNI kubwa kwa UPINZANI wa Tanzania kila UKIHANGAIKA WANANCHI hawana muda nao WANASIKILIZA kasi ya RAIS tu katika FALSAFA yake katika KUPAMBANA na UFISADI aliyoipa jina la KUTUMBUA la MAJIPU .

bYE BYE UPINZANI TANZANIA.
 
Yako mambo mengi yanayopaswa kuzungumzwa na kutiliwa mkazo. Upinzani utakua na kuendelea kupanuka.
Poleni sana. Upinzani umekufa Tanzania. Alichotabiri Wasira ndicho kinachoendelea kutokea ijapokuwa na yeye amekufa kisiasa
 
Rudisheni mfumo wa Chama kimoja mbaki wenyewe.

Magu anatoka povu tu hata yeye ni jipu tena liko juu ya jipu.
 
Naweza kukuhakikishia kuwa wapinzani hawatakosa la kuzungumza hata kwenye serikali zilizoendelea kama Uingereza na Marekani au Canada, Australia, Sweden, etc upinzani una mambo tele na ajenda mpya kila siku sembuse hapa kwetu ambapo hata wajinga wana mambo tele ya kuikosoa serikali yao.
 
Strictly speaking,
Upinzani utakufa hadi kufikia 2020
Maana wapinzan hawajui kazi zao.
Wapinzan wanafanya kaz moja tu nayo n kuipinga serikali iwe inafanya kazi nzuri wao wanapinga tu.

Kwa style hio ya kusubiri kupinga kila
Had kufikia 2020
Watakosa vya kupinga
maana kila JPM anachoongea kinakuwa n amri ya serikali na kinatekelezwa mara moja
Hio imewashtua wapinzan wengi
Wamebak kutoka nje ya bunge na kuzomea tu.
 
Upinzani makini hauwezi kukosa cha kusema kutokana na madudu mengi yaliyofanywa na yanayoendelea kufanywa na CCM miaka nenda miaka rudi.
1. Katiba Mpya bado ni jipu
2. Ufisadi uliotukuka wa EPA, Tegeta Escrow, Ununuzi wa Boti ya Bagamoyo, Mabehewa Mabovu, nyumba za serikali, n.k
bado haujashulikiwa vizuri na Mh. Magufuli
3. Sheria za magazeti na mitandao ni vijipu uchungu
4. Mfumo bora wa Elimu,
5. Matatizo ya Zanzibar hayataisha baada ya uchaguzi wa Jecha isipokuwa maridhiano ya kijamii
6. Sera na mwelekeo wa biashara na uchumi bado hazijaguswa kwa kiwango cha kutosha ukiacha kodi
Hapa serikali bado inaangaliwa itafanyaje ktk utalii, madini na gesi, viwanda, n.k
7. Vita dhidi ya ujangili
8. Ujenzi wa taasisi za kuwajibika badala ya kujenga mtu mmojammoja

Kwa ufupi serikali ndio imeanza tu na bado tuko kwenye honeymoon. Ni mapema, au tuseme ni uchovu wa fikra kudai eti tayari matatizo ya Tanzania kisiasa, kiuchumi, kijamii na kiutamaduni yameshapatiwa ufumbuzi sahihi na wa kudumu!!!!!
 
Umesoma na kuzingatia maazimio ya Wazalendo jana? Utagundua upinzani una hoja nyingi sana za kuibana serikali
 
Upinzani hautakufa kamwe kwa sababu kila penye chanya hapakosi hasi. Uongozi wa CCM hauwezi kufanana kamwe na uongozi wa UPINZANI. Lazima kutakuwa na tofauti za hapa na pale katika utekelezaji wa sera fulani fulani.
 
mimi si mpinzani lkn upinzani hauwezi kufa.hayo yote yanayo fanywa na makufuli ndio yalikuwa yakisemwa na upinzani.ukumbuke upinzani ulisha tengeneza kizazi chake.
Tunaposema upinzani utakufa hatumaanishi wapinzan hawatakuepo.

Wapinzan watakuwepo lakin hawatakuwa na cha kusema.
Watanzania wote watakuwa wameiona kaz ya mh Magufuli
Na hakuna atakaewadanganya kwa lolote kwa chochote.

Kuzomea
Kutoka bungen hovyo
kukosa ustaarab
Matusi
Kulalamikia shanga
Na hiriz
N sehem tu ya
Kifo cha wapinzan
 
mimi si mpinzani lkn upinzani hauwezi kufa.hayo yote yanayo fanywa na makufuli ndio yalikuwa yakisemwa na upinzani.ukumbuke upinzani ulisha tengeneza kizazi chake.
Ni lini ulisikia upinzani wakiongea kuhusu kupinga ufisadi ktk kampeni zao? Tuwe wakweli!
 
Zanzibar imekuwa kimbilio la Vilaza
hahaha
Kimbilio la wewe mwerevu ni Bandarini tu.
Huyo Magu anatwaga maji kwenye sinia kwa sababu haelewi tatizo ni nini hapo bandarini kila siku yuko hapo hapo.

Priorities zake kwa taifa ni zipi?
 
Kimbilio la wewe mwerevu ni Bandarini tu.
Huyo Magu anatwaga maji kwenye sinia kwa sababu haelewi tatizo ni nini hapo bandarini kila siku yuko hapo hapo.
Sijui kama ww n Mtanzania
Au una sound mind
Kama mpaka leo hujajua priorities za mh Magufuli
Priorities zake kwa taifa ni zipi?
 
BYE BYE UPINZANI TANZANIA.

NAANZA kuona KIFO Kibaya kwa UPINZANI wa TANZANIA masikini ambao uliweza kuishi kwa kutegemea makosa na U DHAIFU wa SERIKALI,

SASA hivi RAIS akitoa HOTUBA inaungwa mkono na WATANZANIA wote na wanaijadili kwa muda mrefu huku kila HOTUBA ANAYOTOA ikileta MATOKEO ya moja kwa moja kwa WANANCHI mfano aliposema kuhusu ufinyu wa BAJETI wa MAHAKAMA baada ya siku amewakabidhi BILIONI 22, Amezungunza na wazee wa DSM kuhusu JENGO la WAZAZI MUHIMBILI tayari JANA MAOFISA wa WIZARA WAMEHAMA na leo kazi ya kuweka VITANDA inaendelea ili WAJAWAZITO walale humo nauonea HURUMA sana.

UPINZANI ndio maana kila SIKU unazungumzia suala la ZANZIBAR kama AGENDA kuu Sasa sijui baada ya MARCH 20 UCHAGUZI utakapokwisha sijui WATAONGEA nini MASIKINI,
WA JIANDAE tu turudisha VITI VYA UBUNGE mwaka 2020 kwa CCM WALIOVIAZIMA MWAKA JANA

ITAKUWA ni HUZUNI kubwa kwa UPINZANI wa Tanzania kila UKIHANGAIKA WANANCHI hawana muda nao WANASIKILIZA kasi ya RAIS tu katika FALSAFA yake katika KUPAMBANA na UFISADI aliyoipa jina la KUTUMBUA la MAJIPU .

bYE BYE UPINZANI TANZANIA.
POLE sana
Badala ya kushangilia tu yanayosemwa na wasaka tonge wa lumumba, tuliza akili yako uweze kuona Tathmini za kitaalamu. Elimu bado haijawa bure. Afya muhimbili ni sehemu ndogo sana ya nchi nzima. Bandari waliopitisha na wenye makonteina 11,000plus ukimya ni kiini macho kama JK.
Mikutano ya wakuu wa nchi, anakwepa nini? ZEC kama imepewa mamlaka yasio na mwisho ni mgongano wa maslahi na kwa sababu hiyo rais anaingilia, kinyume chake ni kulinda CCM.
 
Back
Top Bottom