Linamo
JF-Expert Member
- Jan 12, 2011
- 9,976
- 24,498
Nianze kwa kukupa pole Lowassa,halafu nikuage.
Ulichokifanya Jana pale jangwani kimedhihirisha kabisa wewe ni msanii wa hali ya juu na bila shaka unaitendea haki taaluma yako ipasavyo, kwa hili nikupe hongera nadhani baada ya October 25 utajiunga na kina Ray na utasaidia tasnia ya filamu kufika mbali.
Lowassa umekosa sera umekuwa ukirudia yale yale kila kukicha.
Umati mkubwa uliookuwepo pale jangwani kwa siku ya jana ulikuja kusikiliza ilani ya UKAWA na walitaka kusikia kutoka mdomoni kwako ukahaidi utawafanyia nini, unasema unaleta mabadiliko,hicho ndicho walichotaka kusikia na si habari za babu seya, bilali na masheikh wa uhamsho.
Kuwaambia wananchi wakasome ilani kwenye website ni kuwakosea heshima na kutothamini muda wao. Ni wananchi wangapi wenye access ya internet?
Ndiyo wananchi tunataka mabadiliko lakini siyo mabadiliko ya kiini macho kama yako lowassa.
Hotuba yako imeshindwa kukidhi kabisa kiu ya wananchi, umekosa mipango umekuwa mtu wa kusemewa na wapambe wako,wewe ndiyo mtendaji tunataka useme wewe.
Chadema huu ndiyo mwisho wenu,baada ya uchaguzi tunawasahau kabisa kwenye ulingo wa siasa. Mmeamua kulamba matapishi yenu na kutaka kuwalazimisha watanzania walambe pamoja na nyie ila wengi tumejitambua tumevunja uaminifu wetu kwenu.
Kama Mbowe aliamua kuchenji gia hewani sisi tutachenji ardhini ifikapo October 25.
Siioni nafasi ya Lowassa na UKAWA baada ya uchaguzi.
Kwaheri Lowassa, kwa heri UKAWA.