kwa yoyote anaeweza saidia

kwa yoyote anaeweza saidia

Hafidhibrahim

Senior Member
Joined
Nov 4, 2014
Posts
142
Reaction score
32
habar ndg za mapumziko, napenda chuku fulsa
hii kuwaomba ndg jamaa rafik pia, mm ni dereva
nmekuja kwenu najua kuna naweza pata msaada.
km kuna m2 anaweza nikabidh gar nikamletea
hesabu suzuk(kirikuu) au townace au noah na
ata km gar ya nyumban kumuendesha tajir au
kaz za kupelekea watt shule np tayar np dar
mawacliano 0713844841 ahsante
 
habar ndg za mapumziko, napenda chuku fulsa
hii kuwaomba ndg jamaa rafik pia, mm ni dereva
nmekuja kwenu najua kuna naweza pata msaada.
km kuna m2 anaweza nikabidh gar nikamletea
hesabu suzuk(kirikuu) au townace au noah na
ata km gar ya nyumban kumuendesha tajir au
kaz za kupelekea watt shule np tayar np dar
mawacliano 0713844841 ahsante

mtu akukabidhi gari yake kirahisi rahisi tu siyo??

unayo leseni?

cheti cha udereva unacho?

umesomea wapi?

Elimu yako?


unazungumza kiingereza?



upo wapi? unaishi wapi??


una mdhamini?

kazi yake?

kipato chake?

anaishi wapi?

muajiriwa wa serikalini??



Jibu hayo maswali hapo Juu kwanza kama kweli unahitaji kazi.
 
mtu akukabidhi gari yake kirahisi rahisi tu siyo??

unayo leseni?

cheti cha udereva unacho?

umesomea wapi?

Elimu yako?


unazungumza kiingereza?



upo wapi? unaishi wapi??


una mdhamini?

kazi yake?

kipato chake?

anaishi wapi?

muajiriwa wa serikalini??



Jibu hayo maswali hapo Juu kwanza kama kweli unahitaji kazi.

Duhhh,huku sasa kukatishana Tamaaa mkuu.Hii ndio hali ya sie vijana wa Ki TZ
Nahisi ameandika vizuri,Muungwana unaweza kumuelewa tu,na kwa vile hujakumbwa na shida ndio maana umemripukia hivyo.Ila uandishi tu unakuonyesha ni kwamba amehangaika vya kutosha.Sio kila Dereva mzuri yupo njiani ila kuna drivers wengine wazuri sana na waaminifu sana ila hawajapata gari za kukabidhiwa kuendesha wapoa kama day workers tu.Hii kazi ni Sawa na Serikalini,Sio kila muajiriwa serikalini au Sector binafsi ni Mtendaji mzuri licha ya kwamba Interview alifanya vizuri,ila wapo watu Kibao uraiani ni wazuri mno kuliko wao.

Mie naamini ameandika vizuri ila ni suala la kujazia tu,ni kwamba karibia kila post humu mara nyingi huwa haikamiliki kwa 100% kutokana na muhitaji.Ila sio mbaya ku generalize ila pia kama vijana tupeane Moyo,likiwa halijakufika huwezi jua.

We unamuuliza eti mdhamini kipato chake?huu utani sasa
Kiingereza?Haya maswali kama vile anaomba kazi UN?

Na declare interest kwamba ni mfanyabiashara wa gari hizo Carry(Virukuu).Na Mwezi ujao mwishoni naingia kwenye Noah Inshallah kuangalia na huko
Sina Driver hata mmoja aliena mdhamini wa Serikalini.

Vitu muhim sio vyote kama ulivyoweka hapo juu:-

-Driver kuwa na Valid License tu inatosha,maana lazima atakuwa alikuwa approved na Traffic.Muhim ni wewe kuichukua ile copy na kwenda nayo kuihakiki tu na kule utakuta Data zake zote na kama ni fake utajua tu.Mfumo wa sasahivi upo kisasa zaidi.

-Mdhamini
Mdhamini anaweza kuwa mtu yoyote mwenye mali isiyohamishika,yenye thamani sawa na Gari yako,na pia mtu anaweza kujidhamini mwenyewe kama anamali isiyohamishika yenye thamani ya gari husika,kama Nyumba,Mashamba nk.
Mie Drivers wangu wote wamedhaminiwa na familia zao,Mmoja amedhaminiwa mpaka na bibi yake.
Namna ya uhakiki,kwanza Drivers wengi na wote kwa upande wangu walikuwa wawazi sana,na ilinipa wepesi mno kufuatilia na kama ni mjanjamjanja utamjua mapema sana tu.

-Mwanasheria Hatua baada ya hapo ni kumkabidhi Mwanasheria ili mambo mengine yafuate,ili kuhakiki mwanzo hadi mwisho wa mhusika pamoja na vielelezo vyote.Suala la mwanasheria watu wanalikimbia sana ila ni bei rahisi sana hawa watu kwenye kazi hii ukizingatia kwamba unaweka pesa nyingi njiani.Ila muhim uwe na Mwanasheria wako wa kudum yaani kama Mwanasheria wa Familia vile,hapa utamtumia utakavyo na yeye atajenga imani kwamba anamteja wa Kudum.
Ila kama leo huku kesho kule,basi kila unapoenda unapigwa bei ya Mteja ingia mteja toka.

-Serikali ya Mtaa
Hatua hapo juu Mwanasheria hushirikisha Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa kwa hatua zaidi

-Kisha ni kukabidhi gari na kuombeana Mungu kazi iwe Salama
Na muhim zaidi kwa sie matajiri,tuwe katika maombi yetu ya mali zetu,basi tuwe tunawaombea hawa Madrivers au waajiriwa wetu kwamba kazi zao ziende salama na wao wapate wateja wengi ili na wao familia zao ziboreke.Na pia kuwaombea Usalama wao wakati wa kazi zao na majukum yao kwa ujumla.Mie huombea Drivers wangu woote kila Sala ya Alfajir.Maaana wakipata wao na mie ndio nimepata,na wakifanikiwa wao zaidi na mie ndio Baraka zaidi napata kwa Mungu.Ukimuombea mwenzio kwa mungu apate zaidi basi mungu anakubariki mara nyingi zaidi.Ila hili gum sana kwetu,tunapenda Drivers wawe watwana tuuu,mwisho siku tunaona Drivers wote pasua kichwa.

Ila kabla ya Hapo:Ushauri ni Kwamba Drivers na wao ni Binaadam
Hakikisha kwamba kama hali inaruhusu basi mfungie kifaa maalum katika stystem ya GPS CAR TRACKING SYSTEM,ili kulinda mali yako na kumlinda yeye Pia.
Wapo Drivers wanatekwa na Majambazi,sasa hii itakufanya kujua Gari yako ipo wapi,maana zile zina detect hadi speed ya gari,eneo lilipo,nakama ametoka nje ya Dar basi system itakuambia kwamba yupo nje ya Dar na njia aliyopo.Maana majambazi baadhi yao hupiga route ndefu,sasa System pia inakupa uwezo wa ku access kuzima gari ukiwa na Sim yako tu kama hizi Smart phones au Computer yako yenye Internet Access.

Sasa unaweza kulizima gari na hata wafanye nini hawawezi kuliwasha,maana watahamaki,sasa kama ni Majambazi basi wataiacha gari wakimbie,maana watajua ime detect.

Na pia kuna Mini Cameras nimeziona hapa Dubai kwamba unaweza kuifunga bila kujulikana.
Sasa kama uki combine vyote basi hata wakikimbia picha zao na maongezi yao yote yananaswa.Na kuna Option ya Mini Speaker ndogo sana nimeona pia unaweza kuifunga na ku command endapo unaona hatari

Na Kampuni nyingi zenye kufunga TRACKING SYESTEM zote zinafanyakazi na Jeshi la Polisi,sasa wakiona hilo tu basi ukitoa taarifa kwao wanai Search gari ilipo na kutoa order kwa Polisi kwamba gari fulani ipo sehem fulani umbali fulani,inaenda kwa wastan wa speed fulani,ili waifuatilie.Ni mfumo mzuri saaana.

Tatizo ni moja tu,kwamba Watu wengi sana tunaamini kwamba kwenye NOAH,au CARRY matukio hayo hayawezi kutokea,ila siku ikitokea utakuwa umeishachelewa kujifunza,na BIMA hailipi kwa mzembe.Chukua hatua mapema.Mfumo huu hadi Kwenye Bodaboda unaweza kuwa fixed.Ukikimbia gharama basi unaweza kujuta baadae,waswahili wanasema Majuto ni Mjukuu wa Comedy Tanzania

Kwamie nahisi hayo ni mambo ambayo ndio muhim zaidi.Ila wengine wazoefu mnaweza kujazia.Maana Mie pia binaadam sina ukamilifu.Nimetumia uzoefu wangu kama mie binafsi.
 
ahsant kk kwa kutupa ushaur na pia mm ni dereva na km kuna m2 atanikabidh gar bac mzamin wng ni wazaz wng na driving licence yng ipo ata km ukinikabidh gar nkaacha licence yng kwa uhakika
 
ahsant kk kwa kutupa ushaur na pia mm ni dereva na km kuna m2 atanikabidh gar bac mzamin wng ni wazaz wng na driving licence yng ipo ata km ukinikabidh gar nkaacha licence yng kwa uhakika

Hembu nipe machache juu ya haya yafuatayo.
-Hesabu ya Carry ni kiasi gani kwa wiki
-Hesabu ya Townace Tani moja ni kiasi gani kwa wiki
-Hesabu ya Noah ni kiasi gani kwa wiki
-Umewahi kufanyakazi au umeona tu kwamba zinafanyakazi basi ukipewa utaingiza pesa.
-Wazazi wako wanamiliki nini kisichohamishika

Upande wa Driver wa familia:-
Je mshahara kiasi gani,hapa usiweke nauli,weka mshahara tuu,kwa muono wako,licha ya kwamba najua inategemea na majukum,ila lazima utakuwa na kiwango chako cha chini kichwani

Haya yatasaidia wengine,maana mie tayari nimo kwenye mfumo,na sihitaji Driver kwa sasa
 
suzuk carry kwa cku f20 kwa wik 140k townace kwa cku f30 kwa wik 240k na noah kwa cku f50 kwa wik 350k na km ntafanya kaz kwa m2 akanipa kwa cku f7 kwa mwez 200k ahsanten na wazaz wana nyumba na viwanja
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom