Kwa yale tuliyoyaona katika ziara ya Rais kule Rukwa na Waziri Mkuu kule Morogoro, Tanzania tuna ombwe la uongozi

Ni ukossefu wa uelewa wa WaTzd, sera ya CHADEMA inazungumzia kanda za utawala.
Inatakiwa kuondoa utitili wa viongozi kama DC RC etc wanaoteuliwa na Raisi.
Taifa linaingia hasara kwa gharama zisizo na sababu.
Kudhibiti kila kanda iwe na utawala unaotokana na kuundwa na utawala wa kanda. Ni rahisi kusimamiwa maana wameajiliwa na kanda husika, ni answerlable kwa waliomwajili.
Nchi itasonga mbele, tuache mambo ya yena yena hatutakwenda popote!!
 
Ninaposema mifumo, maana yangu ni kwamba kwa mfano katika suala la kuhamia Dodoma. Tulimsikia Magufuli aliposimikwa kuwa Mwenyekiti mpya wa CCM kumrithi Kikwete, akitangaza kuhamia Dodoma. hapo Bajeti ilikuwa tayari imepita. ilitakiwa Serikali ilete muswada kuhusu ratiba ya kuhamia Dodoma na implication yake katika bajeti yetu. hilo halikufanyika. mfumo wa kufanya maamuzi ulidharauliwa. wala hakupitisha katika Baraza la Mawaziri. alitangaza tu basi.

Mfano mwingine ni katika kusimamia matumizi ya serikali. Magufuli ametuhumiwa kugawa fedha mwenyewe badala ya utaratibu uliopo. na anagawa kwa kufuata matakwa yake na siyo bajeti iliyopitishwa. matokeo yake ndiyo hizo 1.5 T na zingine ambazo zinakosekana. matokeo yake kwa kuwa CAG ni imara na thabiti, wanagongana, na kwa kuwa Magufuli ni mbabe, anamtumia Spika kumdhoofisha CAG, ikiwa ni pamoja na kupunguza bajeti yake kila mwaka. TAKUKURU nayo pamoja na serikali hii kujinasibu kuwa mpambanaji wa UFISADI, bado hawana ruhusa kupeleka kesi mahakamani, hadi ipitie kwa DPP. hayo ukiongezea na kubana bunge live, kubana maamuzi ya bunge, kwa kupita naibu spika ambaye ni mbunge mteule wa Rais, Kubana vyombo vya habari ambavyo ni MUHIMILI WA NNE katika utawala, utaona kwamba mifumo ya uwajibikaji na usimamizi inadhoofishwa. Rais anajirundikia madaraka na hataki kuhojiwa wala kukosolewa.

Tulizoea zamani serikali ikileta muswada, kutegemea na michango ya wabunge, inaweza kurekebisha. Siku hizi wanaotakiwa kurekebishwa ni Wabunge wenyewe, hata wa CCM. hapo uwakilishi wa wananchi unadhoofishwa.

Pia awamu hii viongozi wana nidhamu ya woga sana. na kwa kuwa Rais anafuata hisia tu, ni vigumu kwa viongozi kufuata taratibu za kawaida. kila mara hujiuliza, hapa mkuu atafurahi???
Sasa huo sio mfumo mkuu,hayo ni maamuzi binafsi ya kiongozi husika.
 
Kwann tunakimbilia kubadili katiba!!!wakati hii ya mwanzo Tu imekosa political will?
Kwa hoja yako mi nadhani tuanze na political will Kwa wanasiasa wetu,then tugundue wap panavuja afu ndo turekebishe!!!
Hivi kuna sehemu kwenye katiba pamesema raisi Yuko juu ya katiba?kama sehemu hiyo ipo basi ni vema tudai katiba mpya!ila kama hakuna mahala panapoonesha hivo basi hata raisi inabidi aifuate!!
Watanzania hatujui nini cha kufanya ikiwa RAISI atavunja katiba,tunabaki kumuachia Mungu Tu😊😊😊😊
Tunakimbilia katiba mpya mpya mkuu kwa sababu tunatataka Rais mwenye "political will" aikute ili asichelewe kushuhulikia maswala muhimu.Kutengeneza katiba inachukua muda!

Niseme pia kwamba Katiba ya sasa inamfunga Rais mikono kufanya mambo ambayo yangeweza kuwabana zaidi mafisadi,wauza unga,wahujumu uchumi,vibaraka wa mabeberu,watakatishaji fedha nk.nk.kwa hiyo mabadiliko ya katiba ni muhimu ili kumsaidia Rais katika utendaji.Hata hivyo kwa mara nyingine nikiri kwamba hiyo inawezekana only when there is political will.
 
Hakuna kizuri kisicho na kasoro mkuu.Hatujajawahi kusema awamu ya tano kumejaa malaika,hapana.Na wala hatuja wahi kusema awamu ya tano watu wote ni wabaya,hapana.Ninachosema ni kwamba bado tuna kazi kubwa ya kufanya kuhakikisha kwamba viongozi wote wabovu wanaondolewa.

Unayemtegemea kuondoa viongozi wabovu yeye anachezea box la kura na kutaka kuwaweka viongozi anaowataka yeye, na sio wanaowekwa kwa ridhaa ya wananchi.
 
Unayemtegemea kuondoa viongozi wabovu yeye anachezea box la kura na kutaka kuwaweka viongozi anaowataka yeye, na sio wanaowekwa kwa ridhaa ya wananchi.
Watendaji wa serikali hawapigiwi kura na wananchi mkuu wanateuliwa,na hawa ndio wenye matatizo makubwa.Kwa hiyo kuchezea box la kura has nothing to do with government employees.Hata hivyo unaweza kuchezea box la kura kwa nia njema kabisa:ili kuhakikisha kwamba nchi haiangukii kwenye mikono ya vibaraka,wauza ngada na matapeli.Hivi Lissu au Mbowe wakabidhiwe nchi kweli,I can't imagine.
 
Watendaji wa serikali hawapigiwi kura na wananchi mkuu wanateuliwa,na hawa ndio wenye matatizo makubwa.Kwa hiyo kuchezea box la kura has nothing to do with government employees.Hata hivyo unaweza kuchezea box la kura kwa nia njema kabisa:ili kuhakikisha kwamba nchi haiangukii kwenye mikono ya vibaraka,wauza ngada na matapeli.Hivi Lissu au Mbowe wakabidhiwe nchi kweli,I can't imagine.

Hizo ni propaganda za kitoto ile mbaya. JK alikuwa anashinda ulaya na kuamkia
America, tena akiwa na maamuzi yote ya nchi hajaweza kuuza nchi ndio itakuwa hao kina Mbowe? Rudi shule ukajifunze propaganda.
 
Hizo ni propaganda za kitoto ile mbaya. JK alikuwa anashinda ulaya na kuamkia
America, tena akiwa na maamuzi yote ya nchi hajaweza kuuza nchi ndio itakuwa hao kina Mbowe? Rudi shule ukajifunze propaganda.
Mimi sio mtu wa propaganda ni mtu wa action.
 
Back
Top Bottom