Mathanzua
JF-Expert Member
- Jan 4, 2017
- 15,810
- 20,654
Sio siri kwamba Rais na Waziri Mkuu wanafanya kazi nzuri sana ya kuwatumikia wananchi,na wote hatuna budi kuwapa pongezi.Kote walipokwenda tumeona wakitatua matatizo ya wananchi on the spot,kukemea watejdaji wabovu na wakati mwingine kuwasimamisha kazi.
Watendaji wengi wa serikali kuu na halimashauri ni kama wapo wapo,tu hawana kabisa nia ya kweli ya kuwatumikia wananchi.Nia yao kubwa ni kujineemesha binafsi,familia zao na ndugu zao.Tatizo ni kubwa katika kila Mkoa na Wilaya.Hii inawapa shida sana Rais na Waziri Mkuu katika kutekeleza maono yao ya kuwaletea Watanzania maendeleo.
Ni hivi karibuni tu Waziri mkuu alitembelea Wilaya za Ifakara,Kilombero na Malinyi.Wote tulishuhudia madudu Waziri Mkuu aliyokutana nayo kule,hata ikabidi viongozi mbali mbali wa Wilaya hizo waondolewa katika nafasi zao.Ni hivi majuzi tu tumeshuhudia pia utendaji mbovu kabisa wa viongozi kule Rukwa,hata ikabidi Rais aingilie kati kisa cha mama mmoja aliyenyang'anywa mifugo yake kwa hila na viongozi waliopewa dhamana ya kuwatumikia wananchi,huku viongozi wa Wilaya na Mkoa wakishindwa kabisa kumsaidia mama yule.
Jambo linalo onekana dhahiri katika matukio ya Morogoro na Rukwa ni kwamba viongozi ni sehemu ya matatizo ya wananchi.Je mpaka Rais au Waziri Mkuu aje ndio matatizo ya wananchi yapate ufumbuzi?Je Rais na Waziri Mkuu wataweza kweli kutembelea kila Mkoa na Wilaya ili kutatua matatizo ya wananchi?Jibu ni kwamba haiwezekani.Ni nini hasa kinasababisha viongozi wetu wengi kutopenda kuwahudumia wananchi inavyopaswa kiasi hiki,ni kukosa weledi,mgomo baridi,ni nini hasa.Jambo moja ni dhahiri,nalo ni kwamba lipo tatizo kubwa la kiuongozi,ambalo kama halikutatuliwa Watanzania kupata "maendeleo ya kweli" itakuwa vigumu sana.
Napenda nimalizie kwa kusema kwamba tunao viongozi Tanzania,lakini bado tuna ombwe la uongozi.Mungu isaidie nchi yetu.