Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
Habari wanaJF,
Huko Shinyanga mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Rehema Tumbo amenyongwa na mumewe Raphael Kazembe tena kwa kutumia Khanga kisa kikuu kikiwa ni wivu wa mapenzi.
Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Graiftoni Mushi, amethibitisha kutokea kwa tukio hili, na inadaiwa kuwa mwanamke huyo alichelewa kurudi na alipomgongea mumewe chumbani wanakolala hakumfungulia ndipo alipoamua kwenda kulala katika chumba cha watoto ndipo mwanaume huyo alipoamua kufuata na kuanza kumpiga na kumnyonga hatimae kumsababishia mauti.
Mtuhumiwa alikimbia baada ya tukio hili na mpaka sasa polisi wanaendelea na juhudi za kusaka kokote aliko, Mwenyekiti wa mtaa huo bwana Edward Mihayo anasema taarifa zilimfikia kutoka kwa wanamtaa waliomfuata kumwambia mara baada ya kushuhudia maiti ya rehema ikiwa imenyongwa kwa Khanga.
Sasa wanaJF, yaani wivu mpaka usababishe mauti?