Mkuu, Kanda ya kaskazini! Natanguliza shukurani katika hili.
CHAMA CHA KUFA NA KUZIKANA ndiyo mmdudu gani tena huyo Mkuu? Huwa siendekezi sana masuala ya ukanda na ukabila, kama mtu ni kabila langu tukikutana tunachat tu haina haja ya kuwa na chama. Chama pekee ni jamii inayonizunguka, marafiki zangu ndiyo ndugu zangu wa kufa na kuzikana. Kwetu ni mbali sana na ninapoishi, lakini nipo na amani ya kudumu.
Dah kumbe humu JF tuna watoto sana eti mtu hajui chama cha 'maafa' huyo bwana anayeomba aelekezwe anaonekana ni mtu mzima mwenye majukumu, na ndio maana haulizii chama cha starehe kama ulivyotaka mkuu Amoeba, we bado mdogo sana hujapatwa na matatizo. Mkuu Ntu ntaku-pm kukuelekeza ofisi ya umoja huo.