Kwa wenye ujuzi wa kilimo, msaada tafadhali

nanya

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2016
Posts
672
Reaction score
523
Habari,

nafahamu uwepo wa manguli wa kilimo humu JF, itakua faraja kama nitapata msaada wenu. nimenunua shamba la heka mbili miezi sita iliyopita, nataka kujua utaratibu wa shamba boy kulipwa mshahara, mazao gani yanalipa, na mbegu bora nitapata wapi.

Msaada tafadhali.
 
1) Utaratibu wa kumlipa Shamba Boy unatofautiana ila wengine hupenda Kumlipa baada ya kuvuna, hapo katikati utanunulia tu chakula na kutibia kama akiumwa. Binafsi namlipa Tshs 120,000 kwa mwezi ila ndio namuwekea mpaka nikivuna nikauza mazao nampa.

2) Mazao gani yanalipa hujasema shamba liko wapi, maana Kuna azao hukubali eneo na eneo, hayakubali kila mahali. Lakini pia inategemea na wewe una uzoefu na mazao yepi.

3) Mbegu bora utapata wapi nayo itatategemea na zao utakaloamua kulilima hapo juu
 
>> hio 120,000 unayomlipa kila mwisho wa mwezi na ukivuna mnagawana mafao au? hapo kidogo sijakuelewa.

>> shamba lipo chanika kwa mbele kidogo, ukubwa wa hekali 2. nataka kulima mazao yasiyochukua mda mrefu kuvuna. kama mwezi, mwezi na nusu navuna.
 
Simpi kila mwezi, namuwekea mshahara wake kisha nikishavuna ndio natoa mshahara wake kwenye mavuno nampa. Ikitokea amejituma sana basi naweza kumuongeza bonus.

Kuhusu cha kulima bado siwezi kukushauri based on available information. Sababu pia sifahamu watu wa Chanika wanalima nini hasa, pia sifahau kama una maji ya kutosha ama lah
 
maji yapo ya kutosha, itakua vizuri ukinitajia mazao ambayo hayachukui mda kukomaa
 
Back
Top Bottom