Kwa wenye ujuzi na XBINARY

Unknown2

JF-Expert Member
Oct 16, 2016
2,344
4,981
Wakuu, nikiwa mmojawapo kati ya wale wanaojihusisha na XBINARY kwa siku za karibuni imekuwa ngumu kutoa hela M-wallet. Na hii imetokea baada ya kuwa kwenye matengenezo ila hali hii imeendelea kuwapo hata baada ya matengenezo kuisha.
Hii inaweza kuwa inaashiria nini ? Au ndo kusema tumetapeliwa??!!
 
Mkuu hiyo XBINARY na M WALLET ndio kitu gani? Tafadhali nipe elimu kidogo
 
XBINARY ni kampuni inayojihusisha na uwekezaji wa mtandaoni. Kwamba unafungua account kama unavyofungua acount ktk mitandao ya kijamii afu unawekeza. Kiwango cha chini cha uwekezaji ni dola kumi ambapo ukishawekeza wanakuwa wanakupa asilimia mbili kila siku kwa siku tano za kazi kila wiki na wanafanya hivyo kwa siku 100 hivyo mpaka muda unaisha utakuwa umepata mara mbili ya kile ulichowekeza. Ina ofa mbalimbali kama ikitokea ukawekeza dola mia, elfu au ukiingiza mtu.

M-wallet ndo sehemu zile asilimia mbili zako zinakuwa zinawekwa. Hela zilizo katika waleti hii unaweza kuzitoa kumtumia mtu alojiunga, kuzihamishia B-Wallet au kuziweka bitcoin wallet yako. Njia ya kuziweka Bitcoin wallet ndo nzuri kwani unaweza kuzitoa kupitia Bitpesa na kupokea hela yako mpesa. Kwa sasa kiwango cha chini cha kutoa hela m-wallet ni dola tano. Hata hivyo kuanzia wiki ilopita imekuwa ngumu kutoa hela kwenye hii wallet jambo ambalo limeleteleza kuleta uzi humu kwani naamini wapo wenye kujua zaidi.

NB:
B-WALLET hapa ndo zile hela unazopata kama ofa zinawekwa. Huwezi kuzitoa kwenda Bitcoin, huwezi kuzihamishia M-wallet bali unaweza kuzituma kwenye account ya mtu mwingine anayetaka kuwekeza au kutunisha account yake nae akakurushia hela yako kulingana na bei ulomuuzia Mpesa.
 
Wakuu, nikiwa mmojawapo kati ya wale wanaojihusisha na XBINARY kwa siku za karibuni imekuwa ngumu kutoa hela M-wallet. Na hii imetokea baada ya kuwa kwenye matengenezo ila hali hii imeendelea kuwapo hata baada ya matengenezo kuisha.
Hii inaweza kuwa inaashiria nini ? Au ndo kusema tumetapeliwa??!!
Mkuu walianza lin hiyo biashara yao ( x-binary) na ww tangu uanze nao mna muda gan mpaka sasa
 
XBINARY ni kampuni inayojihusisha na uwekezaji wa mtandaoni. Kwamba unafungua account kama unavyofungua acount ktk mitandao ya kijamii afu unawekeza. Kiwango cha chini cha uwekezaji ni dola kumi ambapo ukishawekeza wanakuwa wanakupa asilimia mbili kila siku kwa siku tano za kazi kila wiki na wanafanya hivyo kwa siku 100 hivyo mpaka muda unaisha utakuwa umepata mara mbili ya kile ulichowekeza. Ina ofa mbalimbali kama ikitokea ukawekeza dola mia, elfu au ukiingiza mtu.

M-wallet ndo sehemu zile asilimia mbili zako zinakuwa zinawekwa. Hela zilizo katika waleti hii unaweza kuzitoa kumtumia mtu alojiunga, kuzihamishia B-Wallet au kuziweka bitcoin wallet yako. Njia ya kuziweka Bitcoin wallet ndo nzuri kwani unaweza kuzitoa kupitia Bitpesa na kupokea hela yako mpesa. Kwa sasa kiwango cha chini cha kutoa hela m-wallet ni dola tano. Hata hivyo kuanzia wiki ilopita imekuwa ngumu kutoa hela kwenye hii wallet jambo ambalo limeleteleza kuleta uzi humu kwani naamini wapo wenye kujua zaidi.

NB:
B-WALLET hapa ndo zile hela unazopata kama ofa zinawekwa. Huwezi kuzitoa kwenda Bitcoin, huwezi kuzihamishia M-wallet bali unaweza kuzituma kwenye account ya mtu mwingine anayetaka kuwekeza au kutunisha account yake nae akakurushia hela yako kulingana na bei ulomuuzia Mpesa.

XBINARY is a registered company in UK - where are you based, you can claim back your refund; hujapoteza - if you dont want to participate you can withdraw your deposit (T and Cs applied)
 
Hakuna namna yoyote unaweza toa hela ulowekeza. Mpaka ile inayozaliwa napo kwa sisi tuliojiunga zamani hatuwezi toa hela kwa namna yoyote ile. Zipo km namba tu
 
XBINARY is a registered company in UK - where are you based, you can claim back your refund; hujapoteza - if you dont want to participate you can withdraw your deposit (T and Cs applied)
Nisaidie mkuu niipate hela yangu kama inawezekana. How can I claim it?
 
Back
Top Bottom