Habari za leo
Nitakujibu maswali yako kwa mtililiko
Naannza na swali la kwanza kuhusu Transmission.
Umeme unapozalishwa na Generators ether ziwe za Hydro electric au Diesel engine au za Natural gas huwa katika muundo wa Three phase yaani kunakuwa na nyaya tatu ambazo zote ni live
L1 = Red
L2= Yellow
L3 = Blue
Zile line huwa zinatofautishwa kwa Rangi na hupangwa kwa mtindo huo toka kushoto kwenda kulia au Juu kwenda Chini.
Pia ili uelewe hili somo inakubidi kujua aina ua Mifungo/ Connection ya AC machine ya DELTA na STAR
Umeme ikisha Zalishwa ukaingia kwenye Transformer, Itategemea transformer imeundwa vipi output yake either Delta au Star.
Kama ni Delta jua hapo utapata 3 phase tuu na kama ni Star utapata 3 phase na Neutral au kifupi tunaita 3PN yaani 3Phase Neutral.
Kwa hiyo ukiziona zile waya za Overhead Metal Tower zile Tatu za kwenye Nguzo za chuma ujue zile zote ni LIVE na zina colour code kama nilivyo eleza hapo juu pia zaidi utaona kuna waya moja au mbili nyembamba hiviii zile huwa zinakuwa ni Earth.
Pia kumbukwa umeme unaposafirishwa/ Transmission Huongezwa Voltage ili uweze kusafiri kwa Umbali mrefu sana. Na unaposambazwa/ Distribution hupunguzwa kwa ajili ya matumizi.
Mara nyingi Transformer yenye output ya Delta hutumika kufanya transmission kwa sababu Tunakuwa na Tuahitaji 3phase tu kusafirisha wala hatuhitaji neutral. Ila neutral tunaweza kuitengeneza kwa kutumia transformer yenye Star output. Kwa kutumia Dead point.
Swali la 2
Umeme tunaovuta majumbani ni kweli ni nyaya mbili yaani either L1 or L2 or L3 pamoja na Neutral. Yani lazima TANESCO wakupe moja ya hizo Live pia wakupe na Neutral ambapo tunapata 220/240 Volts
Je earth inapatikana Vipi??
Earth inapatikana Kuanzia kwenye Transformer yenye Mfungo/ Connection ya Star ( Nitaweka mchoro wa Star ili uone earth/ Neutral inavyo patikana)
Ile neutral kwenye Transformer hufikiwa chini pale pale kwenye transformer na hivyo kufanya Ardhi kuwa Conductor ya umeme
vivyo hivyo kwenye kwenye wiring ya majumbani inabidi tufukie earth Rod chini ili kuipata connection ile tuliyoifukia chini kwenye transformer.
Kwa hiyo sasa kunakuwa na uhusiano kati ya Earth iliyofukiwa kwenye Transformer na hii tulio fukia kwenye nyumba ya kushi.
Lengo ni kwamba, kama kuna umeme wowote utavuja(Leakage) Toka kwenye kifaa cha umeme basi upelekwe ardhini na kisha urudi hadi kwenye Transformer.
Umeme unaovuja kwenye vifaa vya umeme Eg. Fridge, Deck, Pasi, na vingine inabid Urudishwe ardhini kupitia earth. Na kama ukiona pasi au fridge au deki inapiga shoti ukiigusa basi ujue haipo connected na earth.
Na kama kiwango cha umeme kinachovuja ni kikubwa basi itabidi Circuit breaker yako iwe Earth leakage Circuit breaker (ELCB) au Residual Current Circuit breaker (RCCB) Izime au I trip ili kulinda madhara ambayo yanaweza tokea
Chunguza kwa makini hiyo picha. Mchoro wa kwanza ni Delta connection ambayo ina Terminal tatu yaani L1, L2 na L3 na mchoro wa pili ni Star connection ambao una Output nne yaani L1, L2, L3 na Earth/ Neutral
Naomba kuwasilisha