Kwa Wanawake Walioolewa/Watakaoolewa....

Kwa Wanawake Walioolewa/Watakaoolewa....

Kingsmann

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2018
Posts
5,582
Reaction score
21,143
Pamoja na mikiki mikiki yote ya maisha lakini tenga muda wa kuwa mtamu. Angalau kwa wiki mara moja tafuta siku ambayo mwanamke unaamua tu kuwa mtamu, huna kisirani, hulalamiki, unaweka shida chini, unaoga vizuri unakaa kwenye kioo unajikwatua, unajipulizia marashi kama yapo unanukia na kuvaa vizuri.

Hata kama hutatoka lakini siku hiyo vaa Braa basi, mume wako auone utamu wako ule ambao ulimfanya akakutongoza na ule ambao akipita mtaani na kuona wanawake wa namna hiyo anageuka mara mbili.

Tatizo dada zangu mna katabia kakuwazoea wanaume na kudhani kuwa mizuka ya wanaume nayo inazoea. Kwamba ukishaolewa kuvaa Braa ndiyo basi, kujipulizia marashi ndiyo basi, kushinda na khanga moja kila siku na dera lilelile ambalo kujua linatakiwa kufuliwa ni lazima unuse kwanza.

Unataka mwanaume akukumbatie wakati akikusogelea unanuka vitunguu swaumu au maziwa ya mtoto! Najua si kila siku unaweza kuwa mtamu lakini mara moja moja mpaka mwanaume aulize unaenda wapi?

Sio ukitoka, hapana unaoga, unavaa, unanukia na unakua mtamu halafu unashinda sebuleni akuone. Unakua wale wanawake ambao wakipita mtaani au ukiwaona wamesimama na mume wako basi unachanganyikiwa.

Akili ya mwanaume inapenda vitu kama hivyo sasa badala ya kukaa kulalamika hakujali badilika na kuwa mtamu. Hata asipokuona lakini wewe mwenyewe utafurahia utamu wako, ukipendeza na kunukia vizuri hata wewe unajipenda na ukijipenda basi jua kuwa kila mtu anakupenda.

Nishamaliza sasa wewe kazana kila siku kuwa wife material uone kama hata huo u-wife hautapotea.
 
Naomba mwenye shida ya mke anioe nifanye haya na mavuzi nitamnyoa karibu pm
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]Maneno sio vitendo. Demiss anaweza kuwa bonge la mshamba
[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]
sio mshamba bwana. Ni mjanja janja fulani hivi. Namfahamu vizuri tu.
 
Back
Top Bottom