Kwa Wanawake wa CHADEMA

Kwa Wanawake wa CHADEMA

FredKavishe

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2010
Posts
1,090
Reaction score
322
Habari zenu wandugu baada ya kutafakari sana jinsi ya mbinu za CCM nikamua kuja na wazo hili.vijana wa CCM na wajumbe sasa wanapita kila nyumba kuvutia vijana wajiunge na chama chao kwamba watapata mikopo bank ya vijana ikianza na ni lazima uwe mwana ccm kujiunga na chama chao.

Sasa tujikite kwenye hoja yangu lengo ni kuvutia wanawake kujiunga kwa njia ya pekee na chadema bado mpaka sasa hatujavutia kina mama wengi kujiunga ya chama chetu ratio ni ndogo sana unaweza kusema katika kila watu 10 mikutanoni kwa chadema ni mwanamke mmoja tu 9 wote ni wanaume hii hali inatisha.

Lakini pia tukitumia matokeo ya sensa iliyopita kuna idadi kubwa ya wanawake na hata ya sasa haitakuwa tofauti idadi yao itazidi maradufu hata katika daftari la kupiga kura idadi nyingi ya wapiga kura ni wanawake lakini bado utokezi wa wanawake kwenye siasa umekua mdogo sana haswa kwa chadema hilo jambo liko wazi kabisa.

Mpango wangu huu napenda kusema nishauanza sasa nimetengeneza katimu cha wanawake wa chadema 30 idadi itakuwa wengi ni wanachuo lengo ni kupata wanachuo wanawake 1000 kabla ya mwezi wa tano 2015.wawe tayari kukitumikia chama chao na kufanya mengine kwa ajili ya uchaguzi.

Lengo langu ni kuvutia kina mama na wasichana kujiunga na CHADEMA kwa wingi na mimi nimejiwekea kuvutia wanawake wasomi wa vyuo vikuu 1000 mpaka itakapofika 2015,baadhi wako ndani ya Tanzania nishawapatia kadi zao za uanachama baada ya kukidhi vigezo nivyotaka.

VIGEZO:
1:Kwanza Uielewe CHADEMA ni nini
Hapa ninawapatia elimu ndogo hawa wanawake wa vyuoni kuilewa CHADEMA historia yake toka kuanzishwa na je inasimama kwenye siasa za mkondo gani,nini malengo ya CHADEMA, je mwanamke akiingia na CHADEMA atanufaika na nini tofauti na akiwa CCM kupewa na khanga

2:Nawapatia Katiba Ya chama Wakaisome Ndani ya Wiki Mbili
Nawapatia katiba ya chama waisome waielewe kabla sijawapa kadi zao za kuwa wanachama wa CHADEMA sasa kuna tatizo wanachama wengi wanajiunga kwenye vyama bila kujua katiba za vyama husika mtu anakua hajui mipaka yake kikatiba.Wakishakubaliana na malengo ya katiba ndo wanapata kadi ya uanachama.

3:Kuelewa Sera,mlengo,Ilani zilizopita za CHADEMA

4:Kuchukizwa kweli na ufisadi,rushwa
Hapa kidogo inakua ngumu kwasababu huwezi kujua malengo na mawazo ya mtu kutoka moyoni lakini tunaweza mbadili mtu tukiona hafai.

Nini haswa lengo la kuanzisha hii:
1:kupata nguvu ya wanawake ambao kimsingi ni wengi na ndo wapiga kura

2:Ukikubalika na wanawake basi jamii itakukubali wakinamama wako tayari kwa ujenzi wa chama kujitolea kwa chochote kile

3:Kuvutia wanawake wengi kujiunga na mapambano ya kukijenga chama na kuhakikisha kinashika hatamu ya nchi 2015.

Nini faida ya kuwa kwenye hii kwa wanawake wa vyuoni
1:Kutakua na elimu ya uraia

2:Elimu ya ujasilia mali itatolewa kwa wanawake wote jinsi wanavyoweza kutumia akili zao kujiajiri.

3:kuhamasisha wanawake wengi kujiunga na CHADEMA

Lengo la hii hoja ni kuwa nikitimiza lengo langu la kupata wasomi 1000 kujiunga na CHADEMA hawa wasomi 1000 watapaswa watuletee wanachama 100 kila mmoja kwa wanawake nitakuwa nimefanikiwa kupata kina mama 100000 mpaka mwezi wa 5 2015 ambao watakua wapiga kura kwenye majimbo mbalimbali na kulinda kura.

Pili ni kuwapa Elimu kuwa unaweza kuwa mpambanaji lakini usiwe kiongozi ndani ya chama ukatoa mawazo ukasidia kwenye ujenzi wa chama.lakini pia unaweza ukawa muajiriwa hata serikali lakini ukausika kuwa mwanachama wa chadema.

Shime kina mama mjiunge na chama kitakacho wakomboa
1:kuwaboreshea huduma za maji kuwa karibu
Mfano karatu,arumeru visima vinachimbwa na bado hatuna serikali

2:kuwaletea mbinu mbadala za kuweza kujiajiri kwa mitaji midogo

3:kuwafanya wanawake muthaminiwe muheshimiwe mupate msaada wa kisheria pale mnaponyanyaswa kuvunjiwa mabanda yenu na mgambo.

4:kuwapa watoto wenu elimu bure

N.B:Nimekuwa nikuuliza na baadhi ya watu kuhusu yale matembezi kutunisha mfuko wa M4C ni kwamba wazo liko ndani ya chama sasa linaandaliwa mchakato vizuri kama wataona linafaa watalileta tena kwenu msife moyo mapambano yanaendelea.

F.K
 
Bifu la Josephina na Halima mdee la kugombea jimbo la kawe 2015 limefikia wapi naomba update
 
Njoo na ID yenye jina lako kamili kwanza, watu tunaangalia profile tujue background yako inasemaje. Msije baadae mkataka kugawana mpaka mbao ya mwisho eti na wewe umeshiriki kukijenga chama
 
Sasa ndugu yangu kabla hujaanza kutatua tatizo ulipaswa kwanza kujua chanzo cha tatizo.wewe chanzo cha tatizo hukijui. Hivyo njia ya kutatua tatizo nayo inakuwa si sahihi.

Wewe unadhani mpaka sasa hivi kwa nini wana CHADEMA wengi ni wanaume ukilinganisha na wanawake?sababu ni hii; kimaumbile wanawake wengi ni watiifu na wanaopenda kufuata utaratibu pale wanapoelekezwa. kadhalika huwa hawapendi fujo fujo.

Kwa kuwa CHADEMA kimekuwa ni chama cha kuandamana;maandamano ambayo mara nyingi hayafuati utaratibu na hivyo kusababisha fujo; ndo maana wanawake wengi wanakiogopa hiki chama.
 
Njoo na ID yenye jina lako kamili kwanza, watu tunaangalia profile tujue background yako inasemaje. Msije baadae mkataka kugawana mpaka mbao ya mwisho eti na wewe umeshiriki kukijenga chama

Wewe unataka kujua background yangu naitwa fred kavishe haya kapekenyue
 
sasa ndugu yangu kabla hujaanza kutatua tatizo ulipaswa kwanza kujua chanzo cha tatizo.wewe chanzo cha tatizo hukijui.hivyo njia ya kutatua tatizo nayo inakuwa si sahihi.wewe unadhani mpaka sasa hivi kwa nini wana chadema wengi ni wanaume ukilinganisha na wanawake?sababu ni hii; kimaumbile wanawake wengi ni watiifu na wanaopenda kufuata utaratibu pale wanapoelekezwa.kadhalika huwa hawapendi fujo fujo.kwa kuwa chadema kimekuwa ni chama cha kuandamana;maandamano ambayo mara nyingi hayafuati utaratibu na hivyo kusababisha fujo; ndo maana wanawake wengi wanakiogopa hiki chama.

Najua chazo cha tatizo ndo maana nikajaa na hivi kusaidia chama,wala usipate shida watakuja tu tena kwa kasi kubwa sana.huwa nafanya research kwanza ndugu kabla ya kuja na kitu kama hiki ukiona hivi ujue nishauliza maswali wa kina dada,kina mama ndo maana nikaja na wazo hili najua mbinu ya kuwavutia.
 
Habari zenu wandugu baada ya kutafakari sana jinsi ya mbinu za ccm nikamua kuja na wazo hili.vijana wa ccm na wajumbe sasa wanapita kila nyumba kuvutia vijana wajiunge na chama chao kwamba watapata mikopo bank ya vijana ikianza na ni lazima uwe mwana ccm kujiunga na chama chao.

Sasa tujikite kwenye hoja yangu lengo ni kuvutia wanawake kujiunga kwa njia ya pekee na chadema bado mpaka sasa hatujavutia kina mama wengi kujiunga ya chama chetu ratio ni ndogo sana unaweza kusema katika kila watu 10 mikutanoni kwa chadema ni mwanamke mmoja tu 9 wote ni wanaume hii hali inatisha.

Lakini pia tukitumia matokeo ya sensa iliyopita kuna idadi kubwa ya wanawake na hata ya sasa haitakuwa tofauti idadi yao itazidi maradufu hata katika daftari la kupiga kura idadi nyingi ya wapiga kura ni wanawake lakini bado utokezi wa wanawake kwenye siasa umekua mdogo sana haswa kwa chadema hilo jambo liko wazi kabisa.

Mpango wangu huu napenda kusema nishauanza sasa nimetengeneza katimu cha wanawake wa chadema 30 idadi itakuwa wengi ni wanachuo lengo ni kupata wanachuo wanawake 1000 kabla ya mwezi wa tano 2015.wawe tayari kukitumikia chama chao na kufanya mengine kwa ajili ya uchaguzi......K

Niambie nitajiungaje na chadema na mimi niko changombe temeke nimeona tawi liko njia panda ya kwenda TCC lakini sijaona ofisi je unadhani nitaweza kwenda huko mbali kiasi hicho?
Kweli naipaenda chadema na ninatamani kujiunga lakini tawi la njia panda TCC sijaona ofisi zake nifdanye nini?
asante
 
Nisaidie No yako PM utaletewa kadi hadi hapo ulipo.
 
Nisaidie No yako PM utaletewa kadi hadi hapo ulipo.
kweli CHADOMO mnachezea akili za watu, unaulizwa ofisi iko wapi unamwambia utampelekea kadi huko aliko kwani imekuwa lambalamba za azam. Kweli CDM ni briefcase company
 
kweli CHADOMO mnachezea akili za watu, unaulizwa ofisi iko wapi unamwambia utampelekea kadi huko aliko kwani imekuwa lambalamba za azam. Kweli CDM ni briefcase company

Kwani kupelekewa kadi kuna matatizo mimi sio mkazi wa hayo maeneo kwahiyo sina geographia nzuri ya hapo alipo jikite kwenye hoja sio kuleta kashfa hapa.
 
umejitahidi kamanda songa mbele ..ila ujitahidi kushirikisha viongozi ucje baadae kusema awa wangu na wale ndo wenu
 
umejitahidi kamanda songa mbele ..ila ujitahidi kushirikisha viongozi ucje baadae kusema awa wangu na wale ndo wenu

Wala usihofu mkuu hili wazo nitamshirikisha dada yangu mdee akipata nafasi tutakuwa tunawaandalia semina ndogo za kujenga mawazo yao na uwezo wao.tutafika
 
Kwa kukusaidia tu ni kwamba, Chadema hakina wanawake wengi kwa kuwa mageuzi mahali popote duniani hasa ktk nchi zetu hizi za kiafrika yanahitaji ukakamavu na ujasiri, na wakati mwingine kujitolea mhanga. Jambo ambalo si rahisi sana kwa wanawake wengi na hata kwa wanaume pia kuna wale ambao bado wanatawaliwa na falsafa ya woga. Na hawathubutu hata kutetea kile ambacho ni haki yao.
 
Back
Top Bottom