Kwa wanaozitaka nyumba za NHC-Posta

Danniair

JF-Expert Member
Feb 18, 2011
360
0
Ninayo hesabu ya uhakika kwa wanaozihitaji nyumba za NHC - Posta.
  1. Pango kwa mwezi ni Tshs. 350,000.00
  2. VAT 18% = 63,000.00
  3. Huduma za maji (yenye chumvi kibao),ulinzi, nk. approx 200,000.00
  4. maegesho ya kutwa (kwani hazina maegesho kwa wapangaji wa NHC ila kwa wapangaji wa wabia) Tsh. 2,700.00 sawa na Tsh. 64,800.00
Upo hapo wewe m-tz wa kawaida? Sabodo hajakosea.
Jisogeze.
 
Lambardi

JF-Expert Member
Feb 7, 2008
11,913
2,000
NHC wamepandisha nyumba zao asilimia zaidi ya 300...mfano nyumba ya vyumba 3 pale ilala...ilikuwa 169,000 kwa mwezi sasa anatakiwa kulipa 540,000 sidhani kama kuna watu watamudu bei hiyo duuu bei kali sana
 
Yericko Nyerere

Verified Member
Dec 22, 2010
16,852
2,000
Halafu kipato cha mtanzania kipo palepale huku gharama ya maisha inazidi kupaa!!
Hili ni bomu linalowasubiri ccm 2015
 
ipogolo

JF-Expert Member
Aug 15, 2011
6,133
2,000
Ninayo hesabu ya uhakika kwa wanaozihitaji nyumba za NHC - Posta.
  1. Pango kwa mwezi ni Tshs. 350,000.00
  2. VAT 18% = 63,000.00
  3. Huduma za maji (yenye chumvi kibao),ulinzi, nk. approx 200,000.00
  4. maegesho ya kutwa (kwani hazina maegesho kwa wapangaji wa NHC ila kwa wapangaji wa wabia) Tsh. 2,700.00 sawa na Tsh. 64,800.00
Upo hapo wewe m-tz wa kawaida? Sabodo hajakosea.
Jisogeze.
Hebu nifahamishe hizo nyumba zipo wapi? Maana umesema NHC Posta.Je ni Libya Posta au Ubungo? au Upanga? je ni Msasani maana kote huko NHC wanazo nyumba. Au ni Posta Mpya?tufafanulie tafadhali.
 
Rejao

JF-Expert Member
May 4, 2010
9,237
2,000
Bora hiyo kodi imepanda.
Afadhali bei imereflect market price. Shirika lilikuwa linapoteza kiasi kikubwa sana cha mapato.
 
IGWE

JF-Expert Member
Feb 3, 2011
9,324
2,000
Bora hiyo kodi imepanda.
Afadhali bei imereflect market place. Shirika lilikuwa linapoteza kiasi kikubwa sana cha mapato.

Markert price kwani serikali inafanya biashara?...halafu hicho kiasi kikubwa cha mapato sidhani kama kinakwenda serikalini navyojua mimi hizi nyumba nyingi za NHC-Posta(na hasa maeneo ya kisutu) ziko mikononi mwa wahindi ndio wanaokodisha kwa waswahili...refer mhindi kama Baghdad
 
Mamndenyi

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
32,411
2,000
mimi nahitaji za bei ndogo, nimechoka na foleni ya morogoro road, ukisikia za kilo moja na nusu, please nakuomba niko chini ya miguu yako.
 
happiness win

JF-Expert Member
Aug 30, 2011
2,463
0
Hizo nyumba si kwa ajili ya walalahoi. Zimelenga wale wale wahindi wafanyabiashara. Sie tutaendelea kubanana hapa hapa kwa mtogole.
 
CHE GUEVARA-II

JF-Expert Member
Jun 17, 2010
571
250
mimi nahitaji za bei ndogo, nimechoka na foleni ya morogoro road, ukisikia za kilo moja na nusu, please nakuomba niko chini ya miguu yako.

Mimi nimeuliza wadau wanisaidie kupata nyumba nzuri Kibaha town (au hat maeneo yoyote Kibaha), hata Visiga; na ikiwa Visiga itakuwa safi sana. Lkn nashangaa hakuna jubu. Yaani hata mtu kufanya udalali hata mara moja anshindwa? Tafuta nyumba kula pesa yako ya udalali mimi nipate nyumba nilipie mwaka mmoja, unaofuata niingie kwenye nyumba yangu! Nitapanga Hotelini mimi kwa hasira! Ooh!
 
Mamaya

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
3,984

njoo upange movenpick hotel,vyumba ni vingi sana
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom