kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 16,252
- 16,171
Nafahamu vyuo vikuu ni vichache nchini na kila mtu anapenda kusoma chuo kikuu. Lakini kama wewe au familia yako hamna uwezo wa kulipa kwa wakati tafadhali sana usichague kwenda kusoma Vyuo vikuu vya binafsi binafsi (private private) hutaweza au utanyanyasika mnooooooo.
Asilimia 99% ya vyuo hivi huwa vinategemea 99% ada ya wanafunzi kujiendesha, hivyo hawana mzaha na wasiolipita ada hata kidogo.
Hivi ni vile vyuo ambavyo hata ukipewa 3,100,000 na bodi ya mikopo lazima pia uongeze hadi 4,000,000 kutoka mfukoni kwako kuongezea kwenye fee.
Jiulize mara tatu tatu kama familia yako itamudu kulipa kwa wakati 7,000,000 kwa mwaka bila mkopo au 4,000,000 kwa kuchanganya na mkopo vinginevyo tafuta chuo cha kusoma Diploma tu yaishe.
Baadhi ya karaha utazozipata kama huna hela hizo ni pamoja na:
1. Kukataliwa kujiandikisha kuwa mwanafunzi hata kama umechaguliwa chuo hicho.
2. Kuzuiwa kuingia darasani kama hujawalipa
3. Kutolewa darasani kila wakati
4. Jina lako kusomwa na kubandikwa kwenye mbao za matangazo kama mtu anayeidaiwa
5. Kuzuiwa kupata chumba kwenye hostel za chuo hicho
6. Kuzuiwa kufanya mitihani
7. Kukosa muda wa kujisomea wakati unahangaikia deni la chuo
8. Kudhalilika mbele ya wanachuo wenzako na watu wengine
9. Ni rahisi mno kujiingiza kwenye vitendo usivyovipenda
10.Uhusiano wako na uongozi/walimu wa taasisi unakuwa mbaya. Hutatamani kurudi tena hapo baada ya kumaliza.
11.
12.