Kwa wanaotafuta wenza wa ndoto zao: Unachotakiwa kuzingatia kwenye mapenzi ya mtandaoni na kuwa salama

myplusbee

JF-Expert Member
Jul 8, 2016
3,612
6,153
Sie Old Timers tunakumbuka enzi za Yahoo na MSN Messengers! Hii ni miaka kadhaa iliyopita kabla ya uwepo wa social media kama Facebook.

Moja ya majukwaa maarufu enzi hizo, huku yakiitwa Windows, yalikuwa ni majukwaa ya Blind Date! Yaani, majukwaa ya kupigiana misele huku wahusika wakiwa hawajawahi kuonana! Yaani, ni kama wanavyofanya watumiaji wa mtandao wa Dating Tanzania unaoweza kujiunga kupitia Peruzi, Chati, Date - Dating.co.tz au kama ilivyo hapa JF!

Msingi wa Blind Date sio kuua mfumo wa Regular Date ambao ni misele kwa watu waliowahi kuonana kabla na kupanga “date”! Lengo la Blind Date ni kuondokana na ule u-primitive wa kuviziana barabarani au wa kwenda kutega “malishoni”! Mbali na hapo, kila kitu kinabaki kama ilivyokuwa enzi hakuna Intanet.

Matatizo wanayopata wale wanaotafuta wenza mtandaoni huku wakiwa na nia thabiti ya kupata mwenza wa ndoto zao ni kwa sababu wameacha kutumia mfumo wa Regular Date kwenye Blind Date.

Unless kama unatafuta mapenzi ya muda mfupi, kwenye First Regular Date (FRD) watu hawakutani Guest House au Ghetto ambalo chumba na sebule ni hapo hapo au hata Bar bali mnakutana sehemu za kawaida kama vile restaurant, Cold Drinks/Ice Cream Parlor n.k! Na kwa mwanamke aliye na lengo la kweli la kupata mwenza wa ndoto zake, katu hawezi kukubali ukutane nae sehemu hatarishi kwa kiuongo chake cha uzazi wakati hiyo ni FRD.

Hivyo basi, kama lengo lako ni seriously kupata mwenza wa ndoto zako mtandaoni basi zingatia yafuatayo:-

BLIND DATE PHASE:

1. Especially kwa wanawake, kama una lengo la kupata mwenza wa ndoto zako, HUNA SABABU ya kupotezea inbox za watu kwa sababu you never know, huyo unayempotezea anaweza kuwa ndio best match kwako! Humjui, therefore you can’t judge him bila “kumsikiliza” kwa texts zake chache za awali zinazoweza kukupa picha anatafuta mahusiano ya aina gani!

2. Mkishaanza kutumiana ujumbe kadhaa na kukuta hajaleta mambo ya kuvuana chupi mapema, hiyo ni dalili ya kwanza njema kwako! Hapa hata akikuomba namba ya simu unaweza kumpa huku ukiendelea kumsoma taratibu! Huko mbeleni akikuzingua, unam-block; SIMPLE!

3. Make sure mnatumia angalau wiki moja ya Blind Dating huku mkiendelea kufahamiana taratibu!! Mwanaume aliye serious hawezi kuona taabu hata kama mtatumia mwezi mzima kwa sababu haongozwi na matamanio ya ngono!

REGULAR DATE:

4. Baada ya hatua hiyo hapo juu kupita, sasa ni wakati wa Regular Date kutoka kwenye Blind Date. Huu ni wakati wa kuonana ana kwa ana. Lakini kama nilivyosema kwenye utangulizi hapo juu, Regular Date watu hawakutani sehemu hatarishi kwa viungo vya uzazi! Na kama imekuwa lazima mkutane bar, make sure you drink lesser or nothing at all. Bia zingine badala ya kuelekea kichwani, huwa zinashuka chini to the origin!

5. Kwenye First Regular Date (FRD), mtu anaweza kupata picha ya ikiwa kile alichokuwa anaki-feel kwenye Blind Date ni kweli kina-exist kwa mwenza wake! Tumieni hii FRD kufurahi pamoja kama marafiki. Pigeni story na chekeni pamoja kwa furaha ya kuonana kwa mara ya kwanza!

6. Fanyeni Regular Date nyingine ya ziada, au za ziada ikiwa hujakiona sawa sawa kile ulichokuwa unaki-feel kwenye Blind Date.

7. KUMBUKA kwamba, Regular Date ni hatua muhimu sana. Ni hatua unayotakiwa kuitumia kana kwamba mwenza wako hukukutana nae mtandaoni. Usipoitumia kwa umakini hatua hii, na kwa mwanamke ukaishia kuvuliwa nguo ya ndani na kukimbiwa, hapo usisingizie mapenzi ya mtandaoni kwa sababu, hata kama msingekutana mtandaoni yangekuwa hayo hayo!

TUJADILIANE!
 
Kwenye Tinder huwa tunaangalia umbali kutoka nilipo, maana unaweza ombwa hela ya Uber kutoka magomeni hadi Mapinga.
Vyuma vimekaza, inabidi uwe mbunifu.



Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Kwa uelewa wangu katika mitandao hiyo wengi wapo kibiashara zaidi kuuza na kununua
nishawahi jaribu kujiunga
Mara pap text d mi nimekupenda
Mimi nikajibu sijakupenda

Men,tuachane na hayo ya kupendana utanifanyia sh ngapi hapo ndo nilichoka ,nikamuhoji 2,3 akanambia aaaa huku wote unaowaona ni wauza mbunye na wato.....

Nilifuta na account yenyewe,dating sites uchafu mtupu unafanyika kule.

Sihitaji maswali nilijiunga kufanya uchunguzi ×××.
 
Kwa uelewa wangu katika mitandao hiyo wengi wapo kibiashara zaidi kuuza na kununua
nishawahi jaribu kujiunga
Mara pap text d mi nimekupenda
Mimi nikajibu sijakupenda

Men,tuachane na hayo ya kupendana utanifanyia sh ngapi hapo ndo nilichoka ,nikamuhoji 2,3 akanambia aaaa huku wote unaowaona ni wauza mbunye na wato.....

Nilifuta na account yenyewe,dating sites uchafu mtupu unafanyika kule.

Sihitaji maswali nilijiunga kufanya uchunguzi ×××.
Hata kama umesema hutaki maswali, mi naomba nikuulize Dinnah!! Mtu kama huyo endapo kukutana kwenu ingekuwa mmekutana physically, labda kwenye daladala, restaurant au sehemu nyingine yoyote ile except mtandaoni; je unadhani angeweza point black maneno kama hayo?!
 
Maelezo yako sahihi mkuu. Tatizo hawa watoto wa kike wepesi wa kuchojoa chupi. Hasa akimpata mwanaume anayemwambia nataka nikuoe anaona kama kweli vile. Sio kila anaesema nitakuoa anamaanisha,badilikeni.
Hapo kwenye gia za kuoa umeongea jambo la msingi sana! Kuna mmoja nilipata kumwambia unatakiwa kuwa makini sana unapo-deal na mwanaume mpenda kutafuna na kutema regardless umekutana nae wapi!! Kwamba, mwanaume mpenda kutafuna na kutema kama amegundua udhaifu wako ni kutaka ndoa; kwake wala haoni taabu kutangaza uchumba na kutoa hadi mahari!! Wala haoni taabu kukutambulisha kwao na yeye kujitambulisha kwenu!

Kwani mahari sh'ngapi bhana! Mahari ya laki 5, anatanguliza 2, hapo unamwamini kwa 100% kiasi kwamba huoni taabu hata kwenda kulala kwake! Si mchumba bhana, hadi mahari ametoa! Akishatafuna na kutosheka, NDUKI!!
 
Back
Top Bottom