Kwa wanaopenda kuiinua sanaa ya filamu Tanzania

Socw

JF-Expert Member
Aug 27, 2016
1,304
2,583
WASAALAM………..

Wakuu najua sasa hivi jukwaa lipo bize kujadili mara hallelujah, mara vevo mara youtube mara zamaradi mara ruge mara nini sijui…lakini nakuombeni mpite hapa pia ili kama kuna chochote unaweza kuchangia kwa namna yoyote itakuwa vizuri sana.

Kwanza binafsi naumia sana kuona sanaa ya muziki ikipewa kipaumbele kuliko sanaa nyingine ikiwamo filamu. Si kana kwamba sipendi mafanikio yao, hapana. Kinachoniuma ni kuwa naona kabisa sanaa ya filamu ina uwezo mkubwa sana wa kuitangaza Tanzania kama ilivyo kwenye muziki kwa sasa.

Musiki umetawala sehemu, ikitoka nyimbo mpya ya msanii yoyote lazima ipostiwe jukwaani lakini ni mara chache sana kuona filamu ya kibongo ikatoka na kupostiwa jukwaani (mwaka huu nimeona mara moja tu, ni ile ya wema). Hii inachangiwa na kudharaulika kwa sanaa ya filamu na watanzania kutokana na kuwa wadau walioko ndani ya filamu kutokuonyesha kuwa wanataka kufanya kitu cha tofauti.

Sasa mimi binafsi ni mtu ninayetamani kujaribu kufanya kitu Fulani katika bongo muvies. Sijawahi kujihusisha na filamu hapo kabla ndo nimeanza rasmi mwaka huu. Na katika kuyafanya haya nilazima kuwe na watu wa kufanya nao kazi. Tayari nimeanza na jitihada zangu binafsi za kutafuta watu katika Nyanja mbalimbali huku niliko. Lakini naamini kuwa humu ndani kuna watu wajuzi na wanauelewa na haya mambo.

Tafadhali kama una chochote cha kuchangia, nitashukuru sana.

Michango na mawazo yainayohitajika ni ya na kiutaalamu katika Nyanja mbalimbali na sio pesa. Kwa kuwa naamini kama yapo mawazo ya na mikakati bora..pesa zitapatikana tu kwa namna yoyote.

Kwa mawasiliano zaidi unaweza ni pm…
 
Filamu za Tanzania zimekosa ukweli. Wamekuwa kama wauza dawa za kienyeji.. Waongo na waigaji..

Soko hili lina opportunities nyiiingi maana kama watunzi mahiri tunao... Vifaa kwa soko letu tunavyo.. Tunachohitaji ni commitment..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom