Kwa wanao tafuta wachumba tu!!!!!!!!!!

Kwa wanao tafuta wachumba tu!!!!!!!!!!

julius mahinya

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
1,152
Reaction score
384
Uchumba ni hatua ambayo kijana (mvulana au msichana) anapitia akiwa na matarajio ya kuoana. Unapo tafuta mchumba hizi ni sifa muhimu sana:-
1. Dini (Awe mtu mwenye imani juu ya Mungu hii utaona faida yake baadae)
2. Tabia njema
3. Afya (Lazima ujue afya ya mwenzio kabla ya kuoana hii ni pamoja na magonjwa ya kurithi kama vile kifafa)
4. Kazi (Hata Mungu alipotuumba alitutaka tukafanye kazi na asiyefanya kazi asile, Lazima mwenzio awe na kazi au frusa ya kazi mbele yake)
5. Usafi (ukitaka kujua kwa haraka haraka mtu ni msafi au la tazama kucha zake, ila kimsingi usafi ni jambo muhimu sana)
6. Asiwe Mlevi
Mengine yaliyobaki mnaweza kurekebishana.

N.B
"Mheshimu mchumba wako maana hutogombea tendo la ndoa"
maana ya nukuu hiyo hapo juu ni hii, mtu unayemheshimu huwezi mtaka akuvulie nguo ili ufanye nae tendo la ndoa huku nyie si wana ndoa, na hilo halitawafanya mgombane. akikuomba tendo la ndoa kabla ya ndoa huyo hakufai piga chini. Kama anataka tendo la ndoa piga chini!
Muulize ni Mapenzi ya Mungu sisi kufanya hivi kabla ya ndoa? kama ni mcha Mungu atakujibu ukweli!
Ila kingine jamani aanzieni kwenye urafiki, uchumba then ndoa!!!!!!!!!!!
 
Naona unajaribu kuyapa mapenzi macho...!

Love is blind my friend... In that sense, you cant get such a 'perfect' spouse!

Na akija kubadilikia ndoani ?

Vipi akikuigizia kwa lengo la kusaka ndoa ?

Wachumba wenyewe hawa wa bebi naomba laki 2 nikasuke! Kazi ipo!
 
Hii umekopi toka kwa fr. D.Hukumu Mbiku (Phd) wa pale udsm
 
Naona unajaribu kuyapa mapenzi macho...!

Love is blind my friend... In that sense, you cant get such a 'perfect' spouse!

Na akija kubadilikia ndoani ?

Vipi akikuigizia kwa lengo la kusaka ndoa ?

Wachumba wenyewe hawa wa bebi naomba laki 2 nikasuke! Kazi ipo!

ahahahaaaa mapenzi hayana macho kweeeelii
 
Sijui kama kwenye karne hii ya kizazi cha nyoka kuna watu wa aina hii. Waoane kabla ya kujuana???
 
love doesn't ask why.......its not conditional either
 
Sijui kama kwenye karne hii ya kizazi cha nyoka kuna watu wa aina hii. Waoane kabla ya kujuana???

.kwa upande mwingine inawezekana kuna wadada wengine hadi upate nafasi ya kumjua itakugharimu PESA ambayo ni bora ungefunga naye ndoa..but ni wachache, wengi kwa maisha ya leo kujaribu ufanisi wa vyombo ni muhimu hiyo ndoa itakuja tu..
 
Na hii ya kujuana ndio inashusha thamani yetu. Kungonoka limekuwa jambo ambalo asiyefanya huonekana kapitwa na mda.
 
Tungekuwa tunazfata sheria za dini wala tusinge hitaji ku test kabla ya ndoa. Ila sasa hata mtoto wa kike miaka 14 kesha harbika. Cha muhmu kwa sasa ni mtu kutulia na kumuomba sana mungu akupe mwenza aliye tohara.
 
Back
Top Bottom