kwa wanandoa wanawake-kwa nini ujichoshe na mume?

Smile

JF-Expert Member
Jul 18, 2011
15,347
11,611
156505_145088328957847_767406285_n.jpg
 
Unajua haya mambo ni magumu sana, coz yanasababishwa na mambo mengi so kuyashinda yote ni ngumu bana kwa binadamu. Unaweza kujitaidi ukapunguza ila siyo kuacha kabisaaaa! Mi najua wewe hujakamatwa tu, ila unafanya!
 
Mume hawezi kunichosha...eti mtu avumilia 10years wating for someone to change, I have my tolerance level above that mmmh hapakaliki!

Ukifikia 10 years sio tolerance/uvumilivu tena, bali unakuwa permeable/ mazoea
 
Ukifikia 10 year sio tolerance/uvumilivu tena, bali unakuwa permeable/ mazoea

Na kweli, kama umevumilia mia 10, huyo anakua chronic wa mauza uza ya mumewe. Wengine hadi wanawatafutia dogo dogo ili wasiende kuchunwa na watu wasiowajua wakaletewa mifupa tu
 
Mume hawezi kunichosha...eti mtu avumilia 10years wating for someone to change, I have my tolerance level above that mmmh hapakaliki!
ndo ivo mlete hapo centre yangu nimefungua
 
Na kweli, kama umevumilia mia 10, huyo anakua chronic wa mauza uza ya mumewe. Wengine hadi wanawatafutia dogo dogo ili wasiende kuchunwa na watu wasiowajua wakaletewa mifupa tu

Naunga mkono hoja yako. Kwanza Ndoa ni kama mtoto mchanga (infant) wanaugua sana wakiwa under 5, baada ya hapo mtoto anazoea mazingira na anakuwa sugu kwa magonjwa maana chonjo sasa zimeingia mwilini. Ndoa nayo ikishazidi miaka mitano ni vigumu kuvunjika, kila mmoja kesha mzoea mwenzake.
 
Ndoa inapitia vipindi tofauti, labda kwa faida ya wasomaji nijaribu kuelezea in a nutshell;

Siku ya harusi mpaka miaka mitatu baadae, hapo kuna mtoto kama mmebahatika ila hata kama hakuna mtoto hapo bado wanandoa hampati stress mkiamini mtapata tu. Ndoa kipindi hiki huwa tamu, mke na mume hupitiana kazini, kama wana magari mawili wao hutumia gari moja, wanatoka out for dinner, hakuna anaemhisi mwenzie anacheat, mapenzi motomoto na home shopping za pamoja, kila uendako wamjulisha mwenzio nk nk nk!

Mwaka wa tatu mpaka wa saba; mshaelezana misimamo ya ndoa yenu, kila mmja sasa keshafahamu true colors za mwenzake! Mke kajua mumewe huwa hafui c.h.pi, mume kajua mkewe haogi jioni etc etc etc, ndugu wameanza kuja, ndugu wa mkeo wanakuja zaidi, ndugu wa mume wakija wanaingia kama kwao hawaogopi, mke kaanza kupunguza outing, mke kaanza kuchukia marafiki baadhi wa mumewe, mke kaanza kuficha kipato chake kwa kisingizio mwanamke lazima awe na akiba. Mume anagundua mke hapendi kwenda ukweni kwani hapatani na baadhi ya mawifi zake. Ugomvi wa mara kwa mara kwani mshazoeana mnaishi kama haitatokea mmoja kumtaliki mwenzake pamoja na maudhi yote. Mke ndo anakuwa msemaji, mume hukaa kimya kwani yeye keshaboreka so anasubiri jioni ifike aende kuangalia futbol kwenye pub pamoja kwake ana DSTV ila haipandi, na wakati huo kanyumba ndogo hakakosekani ka kuchangamsha damu maana mke hujisahau au hukosa hamu kwa kisingizio cha ugomvi au uchovu, etc etc etc.

Miaka tisa kuendelea; mshazoeana, mshasameheana sana, mke keshafuma msg za mapenzi kibao, mume keshafuma nae, either mmebahatika kudumu na kupita, mnajikuta mnaanza kukua kiakili, mnajali watoto, mnajali maendeleo hapo hata mke akijua kuna katoto cha nje, hukasirika ila huwa mpole na anaweza kukuambia umlete nyumbani amfahamu etc etc etc! Hapo kama hamkutalikiana, mapenzi hurudi kwa kasi na mnapofikisha miaka 15 mnatamani mfikishe JUBILEE!

Wandugu NDOA SI LELEMAMA ESPECIALLY NYIE WADADA.
 
Umenena vyema mkuu, kweli ndoa ni safari ndefu na si lelemama .Cha ajabu ndoa nyingi za siku hizi zinavunjika hata kabla ya miaka 3 waliyopaswa kuenjoy.
 
ndo ivo mlete hapo centre yangu nimefungua
smile, nimetoka kuongea na wife muda si mrefu kuhusu hiyo centre yako uliyofungua. Kaniruhusu nije. Natakiwa nije na nini huko au kila kitu nitakuta huko huko?
 
Back
Top Bottom