Kwa wanandoa tuu

Dr. Wansegamila

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2012
Posts
3,036
Reaction score
8,395
Kundi la wake za watu walikuwa kwenye semina kuhusu namna ya kuishi kwa upendo katika ndoa. Muwezeshaji akauliza, wangapi wanawapenda waume zao? Wote wakanyoosha mikono. Akauliza tena, ‘Mara ya mwisho umemwambia mumeo nakupenda lini?. Majibu mbalimbali yalitolewa, Wengine wakisema Leo, wengine Jana, wengine hawakumbuki. Kisha akawaambia, kila mtu achukue simu yake halafu amtumie mumewe text yenye maneno. NAKUPENDA MPENZI, kisha wabadilishane simu. Wakaambiwa kila moja asome majibu kwenye simu aliyoshika, majibu yalikuwa kama ifuatavyo;
Simu 1- Samahani nani mwenzangu?
Simu 2- He Mama Joji unaumwa?
Simu 3- Nami pia daima
Simu 4- Nini tena umeshagonga gari?
Simu 5- Sijakuelewa una maana gani
Simu 7- Umefanya nini tena? Leo sitakusamehe
Simu 8-Chukua taim yako
Simu 9-?!?
Simu 10- Acha kuzunguka unataka shilingi ngapi?
Simu 11 – Hivi naota?
Simu 12 – Kwa kweli leo usiponieleza hii mesej ulikuwa unampelekea nani atakufa mtu shenzi mkubwa
Simu 13 – Nilishakwambia usirudie kunywa pombe au ntakuacha naona umechoka kuishi na mimI
TAFAKARI, CHUKUA HATUA!!
 
Mimi mke wangu huwa namwita mpenzi na yeye ananiita hivyo, na huu mwaka wa 10 kwenye ndoa. Pole zao ambao hawaitani hivyo na kupendana
 
Nimecheka kama mwehu nimeipenda sana hii thread.
 
Mbona ilishaletwa hapa jamvini siku chache zilizopita!!!!!
 
Huu uzi umekuwa malay. hadi kero kaaaaa..


Too much copy n paste!

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…