Kwa waliobobea kwenye lugha msaada kwa hili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa waliobobea kwenye lugha msaada kwa hili

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Babarita, Sep 3, 2012.

 1. Babarita

  Babarita JF-Expert Member

  #1
  Sep 3, 2012
  Joined: Dec 14, 2011
  Messages: 374
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Wana jamvi tusaidiane LUGHA MAMA(lugha ya kikabila) inaathiri vipi maendeleo ya mwanafunzi kujifunza?
   
 2. Gurta

  Gurta JF-Expert Member

  #2
  Sep 3, 2012
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 2,246
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Babarita Swali lako haliko wazi; kujifunza nini? Lugha nyingine mf. Kiingereza, au kujifunza masomo mengine lakini yanayofunzwa kwa kutumia lugha tofauti na ya mama?
   
 3. Babarita

  Babarita JF-Expert Member

  #3
  Sep 3, 2012
  Joined: Dec 14, 2011
  Messages: 374
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Kujifunza masomo mf.Lugha mama ya mwanafunzi ni kihaya alafu darasani mwalimu anatumia kiswahili kufundishia
   
 4. Blue G

  Blue G JF-Expert Member

  #4
  Sep 3, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 4,883
  Likes Received: 424
  Trophy Points: 180
  Sijabobea katika lugha ila nahisi naweza kukusaidia. Ni hivi Babarita,lugha mama ni lugha ambayo mtu amekua akiiongea na hivyo kujikusanyia misamiati mingi ya lugha hiyo,sasa linapokuja swala la kujifunza kwa mtu ambaye amekuwa akitumia lugha mama tu kwa mawasiliano,na akatakiwa ajifunze kwa lugha tofauti hapo inakuwa ngumu kwa sababu mtu huyo hana misamiati ya kutosha ya ile lugha nyingine na hivyo kujikuta akishindwa kuelewa baadhi ya mambo katika kujifunza kwa sababu ya upungufu wa misamiati wa lugha ya kujifunzia.
   
 5. Babarita

  Babarita JF-Expert Member

  #5
  Sep 3, 2012
  Joined: Dec 14, 2011
  Messages: 374
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Mdau asante kwa majibu mazuri. Blue G, je kuna athari nyingine kijamii mwanafunzi atazopata?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. Blue G

  Blue G JF-Expert Member

  #6
  Sep 3, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 4,883
  Likes Received: 424
  Trophy Points: 180
  Ndio kijamii pia zipo.kwa mfano ikiwa alizoelea kukaa katika jamii iliyo na watu wanaozungumza lughamama kama yake hatopata athari zozote hasa za mawasiliano.Lakini pindi ikitokea amelazimka kuhamia ene jingine ambapo watu hawzungumzi lugha mama kama yake,kijamii atapata athari kwani atashindwa kuwasiliana na wengine,mpaka kipindi fulani cha wakati kipite.sijui umenielewa Babarita?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. Babarita

  Babarita JF-Expert Member

  #7
  Sep 3, 2012
  Joined: Dec 14, 2011
  Messages: 374
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Nimekuelewa mkuu.Rejea kwenye athari za kimasomo alafu onesha uhalisia kwenye jamii za kitanzania
   
 8. Iron Lady

  Iron Lady JF-Expert Member

  #8
  Sep 20, 2012
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 4,079
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  lugha mama humuathiri mtu anayetaka kujifunza lugha nyingine katika
  matamshi, na sarufi yani (grammar) hapa ndio utaona mtu anahangaika kubadilisha tensi ya kiswahili kwenda kingereza
  mfano mzungumzaji wa kiswahili kama lugha mama akitaka kuuliza kingereeza are you calling me? atasema you are calling me eehhh? hii ni athari ya sarufi ya lugha yake mama
  haya ndio matatizo makubwa ya lugha mama katika kujifunza lugha nyingine.
   
 9. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #9
  Sep 20, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  To do you do you......to say you say me lol
   
 10. K

  Kilembwe JF-Expert Member

  #10
  Sep 20, 2012
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 1,132
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Nakubaliana na wachangiaji wa mwanzo ni kweli lugha mama huathiri sana katika kujifunza na hasa katika uelewa wa mambo, na athari hii tunaiona sasa kwa wanafunzi wetu wanapoingia shule ya upili wakitokea shule ya msingi! kule chini masomo karibu yote isipokuwa kiingereza tu, hufundishwa kwa lugha ya kiswahili, wanapofika shule ya upili mara ghafla masomo yote hufundishwa kwa kiingereza isipokuwa kiswahili tu! hapo ndio uelewa wa wanafunzi unaanza kudumaa, maana wote walimu na wanafunzi hawana misamiati tosha ya kuelezea kile wanachosoma na kusomeshwa! Nilipokuwa shule ya msingi mjini Mwanza, maeneo ya Nyakato ( siku hizi ni wilaya ya Ilemela), siku moja tulikuwa darasani wakati huo niko darasa la Tatu! mwalimu wa somo la kiswahili alimtaka mwanafunzi mmoja atunge sentensi kuhusiana na neno"Tango"; yule mwanafunzi alisimama na kusema" jana usiku nilikuwa wali na matango ya kuku" wengi mule darasani walicheka sana, mimi sikuelewa alimaanisha nini, ila baadae nilipouliza niliambiwa neno matango kwa lugha ya kisukuma lina maanisha mapaja! so yule mwanafunzi alikuwa na maana ya kusema jana usiku alikuwa wali na mapaja ya kuku!
   
Loading...