Kwa walioajiriwa tu: Ni mkwepe vipi huyu boss wangu?

Kwa walioajiriwa tu: Ni mkwepe vipi huyu boss wangu?

kamusi

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2012
Posts
1,079
Reaction score
753
Ninafanya kazi, nashukuru ni kazi nzuri kiasi, imeniwezesha kufanya mambo mengi ya maendeleo..

Siku za nyuma kidogo tulikuwa na kazi ya ofisi ambayo ilitulazimu kufanyia nje ya ofisi(special task)..tulikuwa wafanyakazi wengi kama 18 ivi pamoja na boss wetu yaani CEO. Japo CEO wakati mwingine mchana alikuwa anatoka na kwenda ofisini na baadae jioni anarudi kuendelea na task force.. tulikaa hotel moja ivi nje kidogo ya mji..ilikuwa ni kazi mpaka usiku kutokana na uzito wa kazi yenyewe

baada ya siku kama 4-5 ivi tukiwa tunaendelea na kazi na kulala hapo hapo hotelini.. siku moja asubuhi sana(alfajiri) nikasikia simu yangu inaita, nikashituka kuangalia nikaona ni boss wangu (CEO) ananipigia..akaniita fulani, nikamjibu ndio boss, akasema samahani nimekuamsha nafikiri ulikuwa bado umelala...

Nikamwambia ni kweli nilkuwa sijaamka lkn haina shina boss,..akaanza kusema, samahani fulani (akanitaja jina langu, na mara nyingi ofisini tunaitana kwa vyeo au sir name lkn sio first name..yeye aliniita first name) unajua leo usiku mzima sijalala nakufikiria tu wewe...akaendela kusema wewe ni mrembo sana yaani ile nguo uliyovaa jana ilikupendeza sana..leo sijalala kabisa na na...na... na..akasita kidogo..mimi nikamkatisha nikamwambia boss itakuwa uchovu wa kazi za jana, na stress mana deadline imekaribia lkn kazi inaonekana bado...nikamuuliza kuhusu habari zingine tu za kazi ilimradi kumtoa kwenye ile mada yake aliyoniamshia...basi tukaongea kuhusu kazi na hakuendelea tena na mada yake..ila mwishoni akasema sawa mrembo na asante kwa kunikumbusha..

Mmmh ile simu ya boss ilinisitua sana, na ikanipa mawazo sana mana ilikuwa saa 11 alfajiri na sikulala tena...
kwa kawaida mimi namuheshimu sana boss wangu, na sio tu kumuheshimu lakini pia namuogopa sana, kwani ni mkali sana na yupo serious muda wote...hapa ofisini anaogopwa na kila mtu..yaani kuingia ofisini kwake mtu unajiuliza mara mbili mbili...lakini ni mchapa kazi mzuri kwani tumepata mafanikio makubwa chini ya uongozi wake..

Muda wa chai ukafika nikaenda na hapo nilikuwa bado na mawazo..nikawa nikimuona boss namkwepa sitaki kukutana nae uso kwa uso, na nikikutana nae naangalia chini.. na hapo akaanza kunitumia na vimeseji vya kunitakia usiku mwema, mara jioni njema, mara ananipigia tu simu kunisalimia, mara msg za kufowardiana n.k..na huko nyuma haikuwa hivyo, ilikuwa ni kazi na maongezi au mawasiliano yetu yote yalikuwa ni ya kazi tu... au labda kam mtu anaumwa/kafiwa ndio tunajuliana hali kupitia simu..hakukuwa na cha zaidi zaidi ya mazingira ya kazi ....

Pia nilinotice kwamba aliongeza kunitizama, nikiongea, nikitembea, nikila etc..na mara moja moja aliponikuta mwenyewe aliniita mrembo!! nimefanya nae miaka mingi lkn hakuwahi kuniitaga hivyo huko nyuma..

Kazi ikaisha tukarudi ofisini, tukaendelea na kazi kama kawaida..ila mimi nikawa nimepunguza sana kwenda ofisini kwake kwani pamoja na kuwa ni CEO lkn pia ni immediate boss wangu..kwa hivo wakati mwingine badala ya kwenda kumuona nikawa naandika vimemo ili nipate maelezo yake au nampigia simu ya ofisini..ila yeye ndio akawa ananiita ili kupata clarification au kunipa maelkezo n.k.. binafsi sikutaka kujiweka karibu yake kwa namna yeyote ile..na heshima imekuwepo na kazi zinaedna vizuri..japo bado ameendelea kuniita mrembo pale tunapokuwa wawili ofisini kwake kama kaniita kwa kazi. na bado vimeseji ananitumia ambavyo si vya kikazi...nk..mimi nachukulia kama utani tu

Sasa majuzi hapa nimepigiwa simu na mtu wa HR ananiambia nipeleke pasport na picha 2 kwa ajili ya visa..nikashangaa, nikamwambia, visa ya nini? akaniambia kwani hujui kama unasafiri kwenda nchi fulani? nikamwambia mi mbona siijui hiyo safari..akasema we si unaenda na boss(CEO) kwenye mkutano ...........akataja nchi..nikamwambia mimi sijui chochote kuhus hiyo safari..yule HR akaniambia basi ndio nakutaarifu hivyo uanenda ...........akataja nchi kuanzia tarehe.........mpka ..........kwenye mkutano..na boss kwa hivyo jiandae..na ulete hizo nilizokwambia kwa maandalizi ya safari...nikamuuliza pamoja na boss tuko na nani tena wengine? akasema ni nyie wawili tu..boss ndio kasema..

Yeleuwiii....nikabaki mdomo wazi, mmh yaani nisafiri na boss nje ya nchi tuko wawili tu? kwa zaidi ya siku 10? nikaanza kukumbuka alivyonipigia simu ile alfajiri kule hotelini..na vimeseji vilivyofuata baada ya pale..nikasejisemea mwenyewe moyoni si bure, kuna jambo..nimekaa hii ofisi kwa miaka lkn sijawahi kusafiri na CEO tukiwa wawili tu, mara nyingi tunakuwa na watu wengine..sasa hii ya sisi wawili tu? mmh kwanza hata huo mkutano haunihusu kwenye kazi zangu za kila siku, unamuhusu yeye CEO..mimi naingiaje hapa? na hata kama ni mtu wa kufatana nae angechukua watu kutoka idara 2-3 ambazo huo mkutano na semina ungewafaa zaidi kwa kazi zao kuliko mimi..

Sasa jamani wadau, nisaidieni nifanyeje? binafsi sipendi kuharibu kazi yangu kabisa, na wala sina mpango kabisa wa kutembea na bos wangu...KIUFUPI SITAKI mahusiano kazini...ninaheshimu kazi yangu, na ninafata maadili yote niwapo kazini..hata kama ni upuuzi nitaufanya nje lakini sio kazini..infact nilishawahi kumcheat mume wangu lkn sio na mtu wa kazini..(msinipige mawe wadau, huyo shemeji yenu alizidi kuwa na vimwana nje ya ndoa hadi akazaa nje..nikalipiza kisasi na mimi, ila sijazaa mtoto wa nje) lkn kwa sasa sina tena uhusiano wa nje..

Najua hii safari sio bure..sasa nifanyeje ili niweze kumtolea nje huyu boss wangu kistaarabu? mwisho wa siku anabaki kuwa boss wangu kazini sasa nifanyaje ili asinichukie nikimkatalia? nahofia nisje kupata wakati mgumu badae kwani na yeye akimchukia mtu mwishowe huwa anashinda tu, si unajua tena CEO..

Mambo ya mapenzi kazini mi sitaki kabisa na wala sipendi..mapenzi hayana siri, na siri si watu wawili..ipo siku tu yatajulikana..na ubaya wa mapenzi ni pale mnapogombana halafu mkaachana tena mpo ofisi moja!!! na hapo huyo mpenzi ndio boss/supervisor wako sijui inakuwaje? sitaki hata kufikiri...kifupi sitaki lkn ss nitamkataliaje na wakati huo huo nisiharibu kazi yangu? sitaki kuweka uhasama kwa hii ishu..

Anajua nimeolewa na mume wangu anamjua vizuri, na mimi namjua mke wake vizuri..sasa hii kitu ni hatari sana kwa kweli...kwanza ni aibu, mi hata sitaki mtu yeyote ajue hata hizi preliminaries tu..

Cha ajabu hapa ofisini ana kasekretari kadogo kadogo kazuuri, tena kako single hakajaolewa..na pia tuna vireceptionist vizuuri vinavutia na vinyonyo vyao saa 6...sasa sijui anatafuta nini kwa mimi ambaye nimenyonyesha 4 times..

Au sijui ni safari ya heri tu labda uoga wangu, any way nitajua huko huko tukifika...
 
Aisee!! Wanawake wana kazi sana . Hii issue sio ndogo usipokuwa makini utaipoteza Na kazi yenyewe.
 
wewe nenda lakini mimkuwa makini katika mazungumzo yenu namna utakavyokuwa unamtreat can help................. take it as joke na we mjibu as a joke can help tooo...... awezi kukubaa ukimpa ni kwa iyari yako mwenyewe....
 
yaani hivi vibosi vina tabia hizi kweli........kikipita kinakuangalia kumbe kina lake jambo

na ukikikataa tu kinaanza kukuwekea ngumu...I think you should understand the risks at hand.

hiyo safari ana lake jambo anataka akakukule vizuri huko......maana ingekuwa ya kheri si angekwambia kabisaa

you do have a choice ............. Be the temporary plaything of a user, or be a person with self-respect.kazi kwako
 
Mbona unawasi wasi sana, kwani ameshakutongoza?? wew fanya kazi yako Ukiskia changamoto ndio hizo wew ulijua ni chakula..

asante kwa kunitoa wasiwasi..nafikiri ni uoga wangu tu...lkn sasa hivo vimeseji anavyonitumia ndio vinanipa wasiwasi.. mara umependeza!!!!! mara i miss u!!!! mara you are so ..............mara dear wangu.......mmh vinanitia shaka...anajitahidi kuwa karibu na mimi zaidi ya kazi........kitu ambacho hakuwa nacho kabisa........hebu nifocus kwenye kazi niache wasi wasi wa kijinga...
 
yaani hivi vibosi vina tabia hizi kweli........kikipita kinakuangalia kumbe kina lake jambo

na ukikikataa tu kinaanza kukuwekea ngumu...I think you should understand the risks at hand.

hiyo safari ana lake jambo anataka akakukule vizuri huko......maana ingekuwa ya kheri si angekwambia kabisaa

you do have a choice ............. Be the temporary plaything of a user, or be a person with self-respect.kazi kwako


mmhh mbona unaintisha my dear, hebu nishauri basi nifanyaje..kazi yangu ni muhimu kuliko chochote..
yaani nimejikuta tu na mawazo yasio na kichwa wala miguu
 
we safiri naye kwanza, ukisharudi ndio utupe YALIYOJIRI HUKO ili tujue TUKUSHAURI VIPI....maana mpaka usawa huu hiyo safari ni lazima uende nae. Please be in touch!

mmh nitawapa feedback, ila sina amani moyoni na hii safari japo nitaenda
 
nenda nae tu
Kwani ukimvulia pichu wlau mara moja kuna ubaya gani kwanza ushasema ulishawahi kungonoka nje ya ndoa sasa tatizo liko wapi?
Changamkia fulsa mtoto wa kike alaaaa......!
Ila chondechonde adabu kwa mumeo iwepo sio ukisharudi sasa wewe ndo jike dume vinginevyo kamuulize ufosaro
 
ninafanya kazi, nashukuru ni kazi nzuri kiasi, imeniwezesha kufanya mambo mengi ya maendeleo..

siku za nyuma kidogo tulikuwa na kazi ya ofisi ambayo ilitulazimu kufanyia nje ya ofisi(special task)..tulikuwa wafanyakazi wengi kama 18 ivi pamoja na boss wetu yaani CEO. Japo CEO wakati mwingine mchana alikuwa anatoka na kwenda ofisini na baadae jioni anarudi kuendelea na task force.. tulikaa hotel moja ivi nje kidogo ya mji..ilikuwa ni kazi mpaka usiku kutokana na uzito wa kazi yenyewe

baada ya siku kama 4-5 ivi tukiwa tunaendelea na kazi na kulala hapo hapo hotelini.. siku moja asubuhi sana(alfajiri) nikasikia simu yangu inaita, nikashituka kuangalia nikaona ni boss wangu (CEO) ananipigia..akaniita fulani, nikamjibu ndio boss, akasema samahani nimekuamsha nafikiri ulikuwa bado umelala...

nikamwambia ni kweli nilkuwa sijaamka lkn haina shina boss,..akaanza kusema, samahani fulani (akanitaja jina langu, na mara nyingi ofisini tunaitana kwa vyeo au sir name lkn sio first name..yeye aliniita first name) unajua leo usiku mzima sijalala nakufikiria tu wewe...akaendela kusema wewe ni mrembo sana yaani ile nguo uliyovaa jana ilikupendeza sana..leo sijalala kabisa na na...na... na..akasita kidogo..mimi nikamkatisha nikamwambia boss itakuwa uchovu wa kazi za jana, na stress mana deadline imekaribia lkn kazi inaonekana bado...nikamuuliza kuhusu habari zingine tu za kazi ilimradi kumtoa kwenye ile mada yake aliyoniamshia...basi tukaongea kuhusu kazi na hakuendelea tena na mada yake..ila mwishoni akasema sawa mrembo na asante kwa kunikumbusha..

mmmh ile simu ya boss ilinisitua sana, na ikanipa mawazo sana mana ilikuwa saa 11 alfajiri na sikulala tena...
kwa kawaida mimi namuheshimu sana boss wangu, na sio tu kumuheshimu lakini pia namuogopa sana, kwani ni mkali sana na yupo serious muda wote...hapa ofisini anaogopwa na kila mtu..yaani kuingia ofisini kwake mtu unajiuliza mara mbili mbili...lakini ni mchapa kazi mzuri kwani tumepata mafanikio makubwa chini ya uongozi wake..

muda wa chai ukafika nikaenda na hapo nilikuwa bado na mawazo..nikawa nikimuona boss namkwepa sitaki kukutana nae uso kwa uso, na nikikutana nae naangalia chini.. na hapo akaanza kunitumia na vimeseji vya kunitakia usiku mwema, mara jioni njema, mara ananipigia tu simu kunisalimia, mara msg za kufowardiana n.k..na huko nyuma haikuwa hivyo, ilikuwa ni kazi na maongezi au mawasiliano yetu yote yalikuwa ni ya kazi tu... au labda kam mtu anaumwa/kafiwa ndio tunajuliana hali kupitia simu..hakukuwa na cha zaidi zaidi ya mazingira ya kazi ....

Pia nilinotice kwamba aliongeza kunitizama, nikiongea, nikitembea, nikila etc..na mara moja moja aliponikuta mwenyewe aliniita mrembo!! nimefanya nae miaka mingi lkn hakuwahi kuniitaga hivyo huko nyuma..

kazi ikaisha tukarudi ofisini, tukaendelea na kazi kama kawaida..ila mimi nikawa nimepunguza sana kwenda ofisini kwake kwani pamoja na kuwa ni CEO lkn pia ni immediate boss wangu..kwa hivo wakati mwingine badala ya kwenda kumuona nikawa naandika vimemo ili nipate maelezo yake au nampigia simu ya ofisini..ila yeye ndio akawa ananiita ili kupata clarification au kunipa maelkezo n.k.. binafsi sikutaka kujiweka karibu yake kwa namna yeyote ile..na heshima imekuwepo na kazi zinaedna vizuri..japo bado ameendelea kuniita mrembo pale tunapokuwa wawili ofisini kwake kama kaniita kwa kazi. na bado vimeseji ananitumia ambavyo si vya kikazi...nk..mimi nachukulia kama utani tu

Sasa majuzi hapa nimepigiwa simu na mtu wa HR ananiambia nipeleke pasport na picha 2 kwa ajili ya visa..nikashangaa, nikamwambia, visa ya nini? akaniambia kwani hujui kama unasafiri kwenda nchi fulani? nikamwambia mi mbona siijui hiyo safari..akasema we si unaenda na boss(CEO) kwenye mkutano ...........akataja nchi..nikamwambia mimi sijui chochote kuhus hiyo safari..yule HR akaniambia basi ndio nakutaarifu hivyo uanenda ...........akataja nchi kuanzia tarehe.........mpka ..........kwenye mkutano..na boss kwa hivyo jiandae..na ulete hizo nilizokwambia kwa maandalizi ya safari...nikamuuliza pamoja na boss tuko na nani tena wengine? akasema ni nyie wawili tu..boss ndio kasema..

Yeleuwiii....nikabaki mdomo wazi, mmh yaani nisafiri na boss nje ya nchi tuko wawili tu? kwa zaidi ya siku 10? nikaanza kukumbuka alivyonipigia simu ile alfajiri kule hotelini..na vimeseji vilivyofuata baada ya pale..nikasejisemea mwenyewe moyoni si bure, kuna jambo..nimekaa hii ofisi kwa miaka lkn sijawahi kusafiri na CEO tukiwa wawili tu, mara nyingi tunakuwa na watu wengine..sasa hii ya sisi wawili tu? mmh kwanza hata huo mkutano haunihusu kwenye kazi zangu za kila siku, unamuhusu yeye CEO..mimi naingiaje hapa? na hata kama ni mtu wa kufatana nae angechukua watu kutoka idara 2-3 ambazo huo mkutano na semina ungewafaa zaidi kwa kazi zao kuliko mimi..

Sasa jamani wadau, nisaidieni nifanyeje? binafsi sipendi kuharibu kazi yangu kabisa, na wala sina mpango kabisa wa kutembea na bos wangu...KIUFUPI SITAKI mahusiano kazini...ninaheshimu kazi yangu, na ninafata maadili yote niwapo kazini..hata kama ni upuuzi nitaufanya nje lakini sio kazini..infact nilishawahi kumcheat mume wangu lkn sio na mtu wa kazini..(msinipige mawe wadau, huyo shemeji yenu alizidi kuwa na vimwana nje ya ndoa hadi akazaa nje..nikalipiza kisasi na mimi, ila sijazaa mtoto wa nje) lkn kwa sasa sina tena uhusiano wa nje..

Najua hii safari sio bure..sasa nifanyeje ili niweze kumtolea nje huyu boss wangu kistaarabu? mwisho wa siku anabaki kuwa boss wangu kazini sasa nifanyaje ili asinichukie nikimkatalia? nahofia nisje kupata wakati mgumu badae kwani na yeye akimchukia mtu mwishowe huwa anashinda tu, si unajua tena CEO..

Mambo ya mapenzi kazini mi sitaki kabisa na wala sipendi..mapenzi hayana siri, na siri si watu wawili..ipo siku tu yatajulikana..na ubaya wa mapenzi ni pale mnapogombana halafu mkaachana tena mpo ofisi moja!!! na hapo huyo mpenzi ndio boss/supervisor wako sijui inakuwaje? sitaki hata kufikiri...kifupi sitaki lkn ss nitamkataliaje na wakati huo huo nisiharibu kazi yangu? sitaki kuweka uhasama kwa hii ishu..

Anajua nimeolewa na mume wangu anamjua vizuri, na mimi namjua mke wake vizuri..sasa hii kitu ni hatari sana kwa kweli...kwanza ni aibu, mi hata sitaki mtu yeyote ajue hata hizi preliminaries tu..

cha ajabu hapa ofisini ana kasekretari kadogo kadogo kazuuri, tena kako single hakajaolewa..na pia tuna vireceptionist vizuuri vinavutia na vinyonyo vyao saa 6...sasa sijui anatafuta nini kwa mimi ambaye nimenyonyesha 4 times..

au sijui ni safari ya heri tu labda uoga wangu, any way nitajua huko huko tukifika...
kula raha utajutia chance hii..
 
wewe nenda lakini mimkuwa makini katika mazungumzo yenu namna utakavyokuwa unamtreat can help................. take it as joke na we mjibu as a joke can help tooo...... awezi kukubaa ukimpa ni kwa iyari yako mwenyewe....

yaani labda nichukulie utani kama unavyosema...ishu ni kazi,.. yaani naona kama kazi ndio inakaribia kuyoyoma hivyo
 
asante kwa kunitoa wasiwasi..nafikiri ni uoga wangu tu...lkn sasa hivo vimeseji anavyonitumia ndio vinanipa wasiwasi.. mara umependeza!!!!! mara i miss u!!!! mara you are so ..............mara dear wangu.......mmh vinanitia shaka...anajitahidi kuwa karibu na mimi zaidi ya kazi........kitu ambacho hakuwa nacho kabisa........hebu nifocus kwenye kazi niache wasi wasi wa kijinga...

Dada ndio changamoto hizo, wew nimekuambia deal nazo tu trust me utashinda
 
kula raha utajutia chance hii..

you cant be serious... nile raha halafu baadae kazi inakuwaje? hivi mtu ulale na boss halafu kazini inakuwaje? khaaa mi hata sitaki huo ujinga..
 
Msimamo unatoka nao huku sio oooonh ntajua huko huko nikifika!!!!!!!!!

Kama bosi "mtu wa kazi" kwa hiyo statement yako maana yake matokeo yanategemea na.muandamo wa mwezi!!!!!
 
Huo mtihani best.
Ni dhahiri kuwa hawezi kukubaka,ila kama ni mtu wa visasi jiandae tu na bifu zisokwisha na pengine kibarua kuota nyasi.
Anza sasa kumshirikisha Mungu na ikiwezekana andaa plan B.
Mumeo umemshirikisha au ndio kibarua kitasitishwa kabla hata visa haijatoka?
 
you cant be serious... nile raha halafu baadae kazi inakuwaje? hivi mtu ulale na boss halafu kazini inakuwaje? khaaa mi hata sitaki huo ujinga..

Kama sikuelewi vile!!!!!

Hutaki sababu umeolewa au sababu ni bosi wako???!!!
 
Aaaa!
Umekuja kuninanga huku ee!
Tutaonana Jumatatu!

bora tu ujue, yaani kwa nini usiwachukue wale kina nahii wa department fulani ndio wanafaa lkn? ujue huko ni kuchezea hela na mimi hunipati
 
Back
Top Bottom