Kwa walio ndani ya mjengoni (NDOA) tujuzeni nasisi

The Only Kilo

JF-Expert Member
Joined
Jul 16, 2010
Posts
352
Reaction score
87
Kabla hujaingia ndani ya ndoa kwa wanaume kitu ambacho huvutia ni uzuri wa kimuonekano i.e physical appearence na kwa wanawake ni jinsi gani mwanaume anavyojali na usmart wa akili pamoja na parsonality kwa ujumla..... Swali linakuja Je, kwa sasa mkiwa kwenye ndoa tayari, ni kipi ambacho unafikiri unakipata kinachosababisha uzidi kumpenda au ni kipi alichokosa baada ya kuingia kwenye ndoa kinacho sababisha umkinai mzazi mwenzio...tupia hapa utupe upana na urefu wa kufanya maamuzi sahihi kabla hatujaoana!
 
Mi sijaoa na hata mpango sina maana hawa mabinti ni matatizo tu. Ni vyema umeuliza kwa waliooa japo naamini hawatakueleza yote maana wengi wao wanasema NINGELIJUA...
 
Niko kwenye ndoa na mkuu BUCHANAGANDE sijafikia kusema ningelijua wala sitarajii
naamini kila nitakalo kwa mwenza wangu linapatikana na wala sijawahi kusema kuwa nilichotarajia kukipata sijakipata
Muhimu ni kuwa wapaswa kufanya uchaguzi makini kwa yule umtakaye na kwa kile utakacho na usifanye kwa majaribio
 
Last edited by a moderator:
MaAla (mambo) ya nje ya nyumba asimamie Bwana (mume) na Mambo ya ndani ya nyumba asimamie bibiye (mke)..hapo !!
Nilisomaga quote :- " It takes a man tu build a house , and takes a woman to make a home " kama sijakosea
 
Kuoa jambo muhimu, wa kuoa sasa, aaahhhh!!!!
 
Kabla hujaingia ndani ya ndoa kwa wanaume kitu ambacho huvutia ni uzuri wa kimuonekano i.e physical appearence na kwa wanawake ni jinsi gani mwanaume anavyojali na usmart wa akili pamoja na parsonality kwa ujumla..... Swali linakuja Je, kwa sasa mkiwa kwenye ndoa tayari, ni kipi ambacho unafikiri unakipata kinachosababisha uzidi kumpenda au ni kipi alichokosa baada ya kuingia kwenye ndoa kinacho sababisha umkinai mzazi mwenzio...tupia hapa utupe upana na urefu wa kufanya maamuzi sahihi kabla hatujaoana!

Ndoa nyingi zinafungwa bila hizo sababu ulizozitaja kuzingatiwa. kila mtu hufunga ndoa kwa sababu zake na pia hujutia ndoa kwa sababu zake. Kanuni ya kufunga ndoa huwa ni upendo wa dhati na wale wanaofunga ndoa kwa kuzingatia kanuni hii kamwe hawajutii.
 
Matokeo ya kwenye ndoa huwa hayafanani, Maana watu hatufanani hivyo piga magoti upate mwenzi mwema katika maisha yako.
 
Umeuliza swali zuri anyway ngoja nijaribu kulijibu kwa mtazamo wangu.
Nipo kwenye ndoa kwa muda mrefu sasa sijawahi kujutia kuwa kwenye ndoa hii na hata kutamani kuachwa au kuishi peke yangu. Kama ndoa imejengwa ktk misingi ya upendo hapo huwezi kumchoka mwanandoa mwenzio . Unajua kuna tofauti kati ya kutamani na kupenda. Tamaa ina sababu nyingi tu na huwa hailast longer inadumu kwa muda mfupi na ndio maana wengine wanakinai ndoa mapema. Sasa kama ulimpenda ulienae na hauko nae kwa sababu ulikutana nae baada ya kua broken hearted au mali alizo nazo n.k . Kumbuka Love sio feeling ni actions and you have to work on it. Mimi sio mtaalam wa ndoa lkn hayo niliyoainisha hapo juu nadhani ni moja kati ya sababu nyingi zonazopelekea watu kuishi bila kuchokana. Chukulia mfano wa mzazi unaempenda haina maana kua hakosei au yote atendayo unakubaliana nayo la hasha lkn huangalii hayo bali unampenda tu.
Nikijibu swali lako kua ni kipi unachokipata kinachokufanya uendelee kumpenda mwenzi wako hapa jibu ni upendo. Kama mwenzako bado anakupenda nasio kwa mdomo bali wewe unajua toka moyoni kua anakupenda basi hilo ndilo linalosababisha uendelee kumpenda kumbuka love ni two way traffic ingawa mara nyingi vipimo havilingani lazima upande mmoja utazidi .

Maamuzi sahihi kabla hujaoa au kuolewa ni kumuomba Mungu akupe mtu wa ndoto yako hapo utaishi kwa amani watu watasema ndoa ndoano wewe hautawaelewa na wengine watasema ndoa ni kuvumilia kila kitu bado hautawaelewa, wengine watasema sitaki kuoa au kuolewa bado hautawaelewa. Mke/Mume mwema mtu hupewa na Bwana.
 
Ableesed nimependa mtazamo wako. Asante nyingi zikufikie popote ulipo
 
Kuoa jambo muhimu, wa kuoa sasa, aaahhhh!!!!
Wa kuoa wapo tatizo wrong choice kutokana na kufuata vigezo vilivyowekwa na jamii na si muoaji mwenyewe, hata mbinu zinazotumika kum-approach mrembo wakati mwingine zina shida maana mtu anapomfuata binti mara ya kwanza anatumia resources nyingi kiasi kwamba hata binti ana ku-rank wa huko huko juu kumbe wewe lengo lako lilikuwa ni kushindana na hali ya soko (kama ni mrembo tu wewe ni kipanga alafu baadae unakimbia hapo sawa lakini kama unategemea huyu kuwa mke wako lazima itakuwa shida kwa kuwa hakuna maana baadae lazima atakushangaa na kukuona haupo organised na kuanza vituko)All in all, mke / mume mwema huletwa na mungu
 
Swali lako ni zuri nami kama mmoja kati ya tulio ndani ya ndoa nina mchango wangu ktk hii post.Utulivu kabla ya kuoa na baada ya kuoa ni muhimu sana.Unaweza ukawa na mpenzi ambaye hauna mpango wa kuishi nae zaidi ya kukata kiu lkn anajua mapenzi mno baadae ukaoa mwingine mwadilifu ila ujuzi wake kitandani ni mdogo.Hapo utahisi unakosa kitu kwa kuwa umelinganisha na uwezo wa yule wa awali.Ukimpata aliyekamilika idara zote shukuru MUNGU ila utawafanyia usaili wangapi ili kujua uwezo wao kitandani?
 
Umeuliza swali zuri anyway ngoja nijaribu kulijibu kwa mtazamo wangu.
Nipo kwenye ndoa kwa muda mrefu sasa sijawahi kujutia kuwa kwenye ndoa hii na hata kutamani kuachwa au kuishi peke yangu. Kama ndoa imejengwa ktk misingi ya upendo hapo huwezi kumchoka mwanandoa mwenzio . Unajua kuna tofauti kati ya kutamani na kupenda. Tamaa ina sababu nyingi tu na huwa hailast longer inadumu kwa muda mfupi na ndio maana wengine wanakinai ndoa mapema. Sasa kama ulimpenda ulienae na hauko nae kwa sababu ulikutana nae baada ya kua broken hearted au mali alizo nazo n.k . Kumbuka Love sio feeling ni actions and you have to work on it. Mimi sio mtaalam wa ndoa lkn hayo niliyoainisha hapo juu nadhani ni moja kati ya sababu nyingi zonazopelekea watu kuishi bila kuchokana. Chukulia mfano wa mzazi unaempenda haina maana kua hakosei au yote atendayo unakubaliana nayo la hasha lkn huangalii hayo bali unampenda tu.
Nikijibu swali lako kua ni kipi unachokipata kinachokufanya uendelee kumpenda mwenzi wako hapa jibu ni upendo. Kama mwenzako bado anakupenda nasio kwa mdomo bali wewe unajua toka moyoni kua anakupenda basi hilo ndilo linalosababisha uendelee kumpenda kumbuka love ni two way traffic ingawa mara nyingi vipimo havilingani lazima upande mmoja utazidi .

Maamuzi sahihi kabla hujaoa au kuolewa ni kumuomba Mungu akupe mtu wa ndoto yako hapo utaishi kwa amani watu watasema ndoa ndoano wewe hautawaelewa na wengine watasema ndoa ni kuvumilia kila kitu bado hautawaelewa, wengine watasema sitaki kuoa au kuolewa bado hautawaelewa. Mke/Mume mwema mtu hupewa na Bwana.

Ablessed,
Be blessed kwa ushauri mzuri, nimeupenda.
 
Back
Top Bottom