Kwa walimu wote | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa walimu wote

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by kobe mzee, Jan 6, 2012.

 1. k

  kobe mzee Member

  #1
  Jan 6, 2012
  Joined: Dec 18, 2011
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  SHAIRI HILI LINAITWA "KWA WALIMU WOTE" LIMEANDIKWA NA PROFESA KEZILAHABI MWALIMU NA RAFIKI YANGU.

  sikilizeni wimbo huu:
  nilipokuwa mtoto niliitwa
  Chacha
  kwa matamshi yangu ya sasa
  nilipokuwa kijana niliitwa Chaupele
  nilipokuwa mtu mzima niliitwa manywele
  nilipokuwa mwalimu niliitwa BURE.

  Huu utakuwa wimbo wako
  utakapostaafu urudipo nyumbani
  umelewa kangara na nyayo zako
  zikishindwa kulenga njia nyembamba vijijini.
  utakuwa kichekesho kwa watoto
  watapokuita, ticha! popote upitapo.

  kumbuka mwalimu utakapostaafu.
  mijusi watataga mayai ndani ya viatu
  vyako vilivyokwisha visigino
  na ndani ya sidiria chakavu
  zilizoshikizwa kamba kwa pini.
  mende watazaliana ndani ya chupa tupu
  za marashi na za bia.

  na manyigu yatajenga ndani ya kofia
  zilizosahaulika kutani.
  utakapokufa nge watazaliana
  chini ya jiwe juu ya kaburi lako,
  na mlevi fulani akipita atapenga
  na kupangusa vidole kwenye jiwe pweke.
  mwanzo na mwisho wako ndio huo.

  lakini wakati ungali hai
  unaweza kubadili mkondo wa maji.
  lakini kwanza tuzungumze. wewe na mimi.
  acha mioyo yetu izungumze.
  baada ya kunyanyaswa
  na kisha nusu mshahara,

  utafundisha tena nyimbo za kusifu viongozi?
  utafundisha tena ngonjera?
  utapeleka tena wanafunzi asubuhi
  wakajipange barabarani kusubiri
  mgeni afikaye saa kumi, an apitapo
  apunga tu mkono kuwatia kichaa cha shangwe
  na huku nyuma mwasambaa na njaa?

  tazama rundo la daftari mezani
  utalimaliza kwa mshahara wa mkia wa mbuzi?
  tuzungumze. ninyi na mimi.
  acha mioyo yetu izungumze.
  mkiwa waoga na kujikunya kama jongoo
  mtawekwa kwenye kijiti na kutupwa
  nje ya ua, na ndani mtawaacha
  wacheza ngoma wakitunga nyimbo mpya.

  sikilizeni walimu.
  anzeni kufundisha hesabu mpya:
  mjinga mmoja kujumlisha wezi ishirini
  ni sawa na sifuri.
  fundisheni historia mpya:
  hapo zamani za sasa
  hapakuwa na serikali.

  sikilizeni kwa makini.
  umoja hatuna:
  twasambaratika kama nyumbu.
  tulichonacho ni woga,
  na kinachotuangusha ni unafiki.
  lakini tusikate tamaa kama mbuni.
  tukiupata umoja bado tunayo silaha.
  KURA.
  SHAIRI HILI LINAPATIKANA KATIKA KITABU CHA "DHIFA"
   
 2. M

  Mr.creative JF-Expert Member

  #2
  Jan 7, 2012
  Joined: Aug 8, 2011
  Messages: 504
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  mh kuna kaukweli ukifumba macho yatatimia
   
 3. Pukudu

  Pukudu JF-Expert Member

  #3
  Jan 7, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 2,970
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  swadakta hamna mtu mwenye e mail ya mkoba rais wa cwt tumtumie ujumbe mahsusi na usambazwe kwa walimu
   
Loading...